Ndo nimemaliza C-section ya 6, nimechoka akili na mwili. Halafu kuna Wanasiasa kwa mwezi wanakula 11 M na bado wanajiongezea mshahara 40%

Pole sana mkuu yani hua natafakari sana hii nchi kuna mwalimu na daktari hawa watu walitakiwa wathaminiwe sana mchango wao ni mkubwa sana kwenye jamii kuliko kipato wanachopata.
 
Wao wanaingia mikataba feki ya kuliibia taifa na bado wanapata mishahara minono, marupurupu ya kibabe, huduma nzuri, malazi na vitu vyote juu ya serikali(kodi za walala hoi)
 
Hakuna kazi ya muhimu kuliko nyingine. Vipi kwa madereva ambao wapo barabarani hayo masaa nyie mlikua mnafanya operation?

Wewe masaa yote umewafanyia 6, dereva mmoja masaa yote hayo amebeba watu 60.

Sijui sababu ya kuona baadhi ya mnaofanya kitu flan ni muhimu na mnapaswa kuonewa huruma kuliko wengine
 
Mi nitakuja kuwa rais, maslahi ya Medical Doctor yatakuwa hivi;
1. Bima ya afya-maisha,
2. Kusomeshewa watoto-international mpaka chuo kikuu,
3. Mshahara minimum mil 12,
4. Makazi-bure,
5. Usafiri-unakopeshwa gari bila riba na unapewa mafuta
6. ….
Thubutuuuu [emoji41]
 
Huyu amekuwa daktari akipitia mikononi mwa wafabyakazi wengi tofauti.Sijui hii akili ya kuona madaktari wanahitaji special package ya mshahara na marupurupu huwa inatokana na nini.
 
hakuna kazi ngumu kama idara ya afya kwa kweli mara uhatalishe maisha yako,mara watu wakulaumu,mara watu wa hovyo wakupakazie unagonga wake zao wodini....dah. hakuna kilichoniuma wakati nazalisha mjamzito mfuko ukapasuka maji yaka ni mwagikia mdomoni...kaz ambayo huwezi lala kwa strahe usiku tu uko kwako una amshwa bila mpangilio
 
Kwa Msioelewa, C-section ni Upasuaji wa kumzalisha Mama (kutoa mtoto/watoto) Kwa Kizazi kwa njia ya upasuaji.

Toka Nilipolala usiku wa kuamkia Jana, mpaka Leo sijalala yaani 24 hours bila kulala.

Kuweni na Huruma Enyi Viongozi, Hivi mtu toka saa Mbili usiku uko Chumba Cha Upasuaji , ukitumia Akili yote, Taaluma yote, kuhakikisha kwamba Mama na Mtoto wanatoka salama.

Hata Chakula nilokula Jana saa 12 jion, tumboni hakipo.

Tunafanya kazi kwelikweli, tunajituma mnoo bila kulala ,bila kupoteza muda, Akili na Mwili vyote vinachoka.

Hivi kweli kazi tunayoifanya inaendana na Mshahara Huu unaokatwa na unakatika haswaa ?. Na utu tuposho tudogodogo hivi?

Eehh Mwenyezi Mungu uendelee Kuwatia Nguvu Madaktari, Wauguzi na Wafanya kazi wote wa Kada hiii, Mungu Baba, kazi hiii ilikua yako, ila kwakua uko juu mbinguni, uliamua kutuchagua tuitendee hapa Duniani, Endelea kutulinda, tuepushie Magonjwa, linda familia zetu, Muda huuu Wake na watoto Wetu tumewaacha Majumbani, Usalama wao uko mikononi mwao.

Lakini Baba Mungu, embu nena na watawala wako, uwape Moyo wa kujinyenyekeza, wakati wanapanga Kujiongeza mishahara minono ya mamilioni, Baba Mungu wakumbuke kua Kuna watu wanapambana usiku kucha kwaajili ya Watanzania.

View attachment 2751793
Nenda kairuki mtafute gyno mmoja anaitwa Dr kiswaga anafanya Cs 6 kwa masaa matatu au manne unalalamika nini sasa?
 
Hakuna kazi ya muhimu kuliko nyingine. Vipi kwa madereva ambao wapo barabarani hayo masaa nyie mlikua mnafanya operation?

Wewe masaa yote umewafanyia 6, dereva mmoja masaa yote hayo amebeba watu 60.

Sijui sababu ya kuona baadhi ya mnaofanya kitu flan ni muhimu na mnapaswa kuonewa huruma kuliko wengine
Uzito wa mambo unatofautiana mzee leo ata useme mshahara wa madaktari milioni mia sio kila mtu atatoboa kuitwa daktari ila uo mshahara wakipewa madereva mbona shangwe japo madereva ni wa muhimu pia simaanishi si wa muhimu
 
Huyu amekuwa daktari akipitia mikononi mwa wafabyakazi wengi tofauti.Sijui hii akili ya kuona madaktari wanahitaji special package ya mshahara na marupurupu huwa inatokana na nini.
Wana inferiority, kila profession ni muhimu na tunategemeana.

Hata yeye hiyo operation anafanya kuna walinzi nje kuhakikisha mazingira ya kazi yapo salama
 
Hongera na asante kwa kuendelea kuokoa maisha yetu, ndugu na jamaa zetu.

Tunaomba uendelee na moyo huo huo, one day mambo mengine yatajipa.

Sisemi kazi yako ni wito, ila naomba usichoke mkuu. Tunakutegemea.
 
Uzito wa mambo unatofautiana mzee leo ata useme mshahara wa madaktari milioni mia sio kila mtu atatoboa kuitwa daktari ila uo mshahara wakipewa madereva mbona shangwe japo madereva ni wa muhimu pia simaanishi si wa muhimu
Ukiweka mshahara wa milion 100 kwa dereva wa bus alitoe dar saa 12 asubuhi alafu afikishe mwanza saa 6 usiku kila mtu atatoboa?

Vipi kuhusu mwanajeshi kila mtu anaweza kutoboa ukiweka mshahara wa milion 100?

Unaamini engineers wote wasingetoboa kama wangeamua kusomea udaktari? Walioamua kusomea accounts unaamini wasingetoboa kama wangeamua kusomea udaktari?

IT na computer scientists nao wasingetoboa kama Kama wangeamua kusomea udaktari? Lazima watu wawe na profession tofauti
 
Mi nitakuja kuwa rais, maslahi ya Medical Doctor yatakuwa hivi;
1. Bima ya afya-maisha,
2. Kusomeshewa watoto-international mpaka chuo kikuu,
3. Mshahara minimum mil 12,
4. Makazi-bure,
5. Usafiri-unakopeshwa gari bila riba na unapewa mafuta
6. ….

Sizani kama kuna nchi inayofanya hivyo.

Wapo madaktari wanaolipwa hela nzuri hapa Tanzania wengi tu
 
Mi nitakuja kuwa rais, maslahi ya Medical Doctor yatakuwa hivi;
1. Bima ya afya-maisha,
2. Kusomeshewa watoto-international mpaka chuo kikuu,
3. Mshahara minimum mil 12,
4. Makazi-bure,
5. Usafiri-unakopeshwa gari bila riba na unapewa mafuta
6. ….
Mpuuzi kabisa wewe 😂😂
 
Kwa Msioelewa, C-section ni Upasuaji wa kumzalisha Mama (kutoa mtoto/watoto) Kwa Kizazi kwa njia ya upasuaji.

Toka Nilipolala usiku wa kuamkia Jana, mpaka Leo sijalala yaani 24 hours bila kulala.

Kuweni na Huruma Enyi Viongozi, Hivi mtu toka saa Mbili usiku uko Chumba Cha Upasuaji , ukitumia Akili yote, Taaluma yote, kuhakikisha kwamba Mama na Mtoto wanatoka salama.

Hata Chakula nilokula Jana saa 12 jion, tumboni hakipo.

Tunafanya kazi kwelikweli, tunajituma mnoo bila kulala ,bila kupoteza muda, Akili na Mwili vyote vinachoka.

Hivi kweli kazi tunayoifanya inaendana na Mshahara Huu unaokatwa na unakatika haswaa ?. Na utu tuposho tudogodogo hivi?

Eehh Mwenyezi Mungu uendelee Kuwatia Nguvu Madaktari, Wauguzi na Wafanya kazi wote wa Kada hiii, Mungu Baba, kazi hiii ilikua yako, ila kwakua uko juu mbinguni, uliamua kutuchagua tuitendee hapa Duniani, Endelea kutulinda, tuepushie Magonjwa, linda familia zetu, Muda huuu Wake na watoto Wetu tumewaacha Majumbani, Usalama wao uko mikononi mwao.

Lakini Baba Mungu, embu nena na watawala wako, uwape Moyo wa kujinyenyekeza, wakati wanapanga Kujiongeza mishahara minono ya mamilioni, Baba Mungu wakumbuke kua Kuna watu wanapambana usiku kucha kwaajili ya Watanzania.

View attachment 2751793
Ungegombea ubunge ukalipwe pesa nyingi nawewe, nani kakulazimisha kusomea udaktari? Nitajie ni mtaaluma gani anayelipwa vizuri ktk ngazi ya halmashauri kuliko daktari?

Acha kazi ukagombee ubunge, maisha hayafanani.
 
Wengi wanasomea udaktari wakitiana ujinga huko mashuleni eti ndo una hela, siyo kweli, hakuna taaluma au ajira yenye hela maana mishahara ni midogo.

Chenye hela ni kuwa mfanyabiashara mkubwa, au teuzi za Rais, kwingineko utaishia kupata hela za kula na ada za watoto, kujenga nyumba moja tu na gari moja tu la mkopo.

Gombea ubunge kama mwenzako ndugulile alivyofanya, na serikali hii itaongeza mishahara tu we subiri.
 
Back
Top Bottom