Ndoa ina mwezi mmoja, nishaanza kukosa amani

hata tako hana
Pole sana.

Hili janga kila mahali. Wanaume wengi mno wanapitia hiyo shida, hata washkaji zangu wanalalamika mno. Wake zao wananuna bila sababu, wanawake wana gubu mno, kisirani na wanawanyima tendo kabisa. Kuna mkurya mmoja mwenye pesa na kazi nzuri, mke wake alimnunia bila sababu na alimnyima tendo, jamaa aliachana na mwanamke ndani ya miezi miwili.
 
Jaman ndoa ndo zilivo.
Yaan tangu nimuoe nimuweke ndani naanza kuona tabia zinazoanza kuninyima aman.Had natamani nimwambie bana tumeshindwana

Tabia anazoonesha
1. Kisiran
2. Kununa
3. Kuzalisha migogoro

Haya yote alivyokuwa kwao sikua nayaona aisee nishachoka.Nimeukumbuka uhuru wangu
Kasha concieve huyo mkuu ni mabadiliko tu ya hormones....ila wanaume mmekua walalamishi sana siku hizi mmhhhh mhuuuuu🙌🙌
 
Jaman ndoa ndo zilivo.
Yaan tangu nimuoe nimuweke ndani naanza kuona tabia zinazoanza kuninyima aman.Had natamani nimwambie bana tumeshindwana

Tabia anazoonesha
1. Kisiran
2. Kununa
3. Kuzalisha migogoro

Haya yote alivyokuwa kwao sikua nayaona aisee nishachoka.Nimeukumbuka uhuru wangu
Welcome to the party bro.
Sasa hapo ndio pa kutumia uanae wako, mkalishe chini mkanye, usimwombe ila mkanye, asipo sikia mrudishe kwao
 
Kwani ulilazimishwa kuingia ndoani BWASHE?

Sikia Kama kweli ulikubali kwa moyo mmoja pambana na huyo dada angu mtazoeana tu ,,

Sokoni kugumu Sana mzee
 
kitu kimoja nakushauri, ndoa yangu inakaribia miaka 20 huko. kwenye ndoa, mkaribishe Yesu atawale maisha yenu, utaenjoy sana. Mimi ndoa yangu sikuanza na Mungu, ndani ya mwaka mmoja tulikuwa tunavurugana hadi najuta kuoa, nilikuwa hadi nampiga mke wangu ngumi na mateke kama mbwa, nakumbuka kuna mwaka niliwahi kumpiga mke wangu tukiwa na first born wetu akiwa na miaka kama mmoja. katoto kalivyo kadogo vilevile kalilia sana kakawa kanamsaidia mamake. ilinipa uchungu mno. zamani niliamini labda ni ile story kwamba mkiwa wote mmekutana ukubwani, kila mtu amelelewa na tabia zake, mkizichanganya lazima miaka miwili mitatu ya mwanzo mvurugane na mtakuja kuwa compatible baadaye. THIS IS VERY WRONG.

NIlikuja kuthibitisha hili ni la uongo baada ya kumpa Yesu maisha, ghafla kila kitu kilibadilika, upendo kwa mke wangu ulijaa, naye kwangu ulijaa, hadi tendo la ndoa hamu iliongezeka na utamu hata wa tendo la ndoa ukawa wa ajabu na yeye upande wake nikaona amebadilika nikimfanya anaonekana anaenjoy zaidi na anaonyesha kuridhika, tukawa kama mapacha hadi leo. sikatai, kumekuwa na ups and down kwenye hilo kwamba hatujakaa kama malaika, ila hata tukigombana kidogo tu kwa kauli, haipiti siku, tumeshapatana na tumekumbatiana. sisi huwa tunalala kwa kukumbatiana hadi leo, nilichojifunza ni hiki;

1. shetani ni roho, huwa anaweza kuingia kwa mmoja na kumtumia mgombane, hadi huwezi jua why mnagombana ila mnagombana tu, yeye shetani anawagongesha vichwa, anakaa pembeni anafurahia mnavyoumizana mioyo tena bila sababu za msingi, na kwa njia hiyo, anawarudisha sana nyuma kimaendeleo na kifamilia, anasababisha hadi magonjwa, hadi kuchepuka kwa silaha yake hii.

2. ukimpa Yesu Maisha yako (ukiokoka) akaondoka, kuna kuwa hakuna kugombana na ndoa inabadilika, manake kila mtu anamhofu Mungu, na kuchepuka kunapotea. ELEWA HILI, sisemi wote waliookoka hawagombani, no, hata ukiokoka unaweza kugombana na kuwa na ndoa mbaya, KAMA UMEOKOKA KWA JINA TU SIO KWA ROHO, wokovu wa Mungu ni wa uhakika, kama kweli umempa Yesu maisha na HUNA MICHANGANYO, Mungu akiwa maishani mwako shetani anafanya nini hapo? ataondoka tu, na kama ukienenda kiroho, shetani anaondoka. hao walokole unaona wanahangaika na ndoa, wamefanya michanganyo na wanafungua milango wao wenyewe shetani anaingia na kuwasumbua.

3. hata unyumba, unakuwa mzuri sana kama nyote mmeokoka kwa kweli. why? shetani huwa anaweza kuharibu chochote kama umemruhusu akaingia maishani mwako, kuna pepo mahaba, huwa yanawaingia wanaume kwa wanawake, hao ni maajenti wa shetani, ukiwa nalo utakuta mkeo wa kawaida tu, unaweza hata kulala naye kitanda kimoja ukaenda mzunguko mmoja tu, ila ukitoka unaenda mizunguko mingi na unaenjoy sana, ndio lengo la shetani, anaweza kukukosesha hamu ya tendo kwa mwenza wako ila nje upo fresh tu.

4. kuna watu wanakosa watoto, kumbe shetani amekaa kwenye vizazi vyao, mapepo ambayo ndio maajenti wa shetani, wanakaa kwako, wanakuoa, wanakuotesha mandoto unazini nao, na kiroho unayazalia hadi watoto. hayo ndiyo yanazuia mimba usipate, au mbegu zako zisizalishe. jaribu kwa Mungu, okoka kwa kweli, sio kwa dini, uone. Mungu atakushangaza.

5. kuna mengi naweza kuongea, mwenye shida ajaribu kumtafuta Mungu. Mungu anasema onjeni muone kuwa Bwana ni mwema, heri mtu yule anayemtumaini Bwana, jaribu tu wala usisimuliwe.

Mwenye kunielewa amenielewa.
Mambo mengne tunayatafuta sis wenyewe tu asilimia kubwa wanaume ndio tunaofanya Wanawake kubadilika.usipojua thaman ya mkeo kuna wana nje watajua thaman ya mkeo.msome mkeo mjue njia zake anapenda nini!!!! NB Ndoa ni kwa wanaume waliokomaaa kiakili haswaa kama hujakomaaa kiakili huwez kuish Na mwanamke
 
Amen mtumishi wa Mungu
 
Uchumba wa miezi nane mwaka siyo afya kwenye mahusiano yatakayozalisha ndoa na familia.

Ilivyo binadamu hawezi ku-pretend kitu fulani kwa muda mrefu so kama mtu ana tabia zake mbaya ni rahisi kuzijua mapema na kujua namna ya kuziepuka kama mtakaa kwenye mahusiano ya kawaida zaidi ya miaka miwili,kijana kabla hujamuweka mwanamke wako ndani jipe muda hata miaka mitatu kumchunguza haraka haraka hazina baraka.
 
Back
Top Bottom