Mkuu hata mke wa pili, wa tatu na kadhalika kila mmoja wakati wa kutolewa ataachana na wazazi wake na kuungana na huyo mwanaume ambaye naye ataachana na wazazi wake.
Mkuu mkuu kwani ukiungana na mke wa kwanza mkawa mwili mmoja mwanaume unakuwa na vichwa viwili? au mikono minne?
Kanuni ya asili tu inakataa dume kwa jike moja, tazama mazingira yaliyotuzunguka dume moja huhudumia majike mengi? Wanadamu ni wanyama iweje wawe tofauti?
Kwenye biblia maneno yaliyotoka kwa Mungu mubashara ni amri 10, hazikuzungumzia ndoa iwe ya wake wangapi na katika kauli za Yesu hakuna mahali alizungumzia ndoa iwe ya wake wangapi, hakuna!
Mitume wa Yesu walikuwa wayahudi, kwa mujibu wa desturi za wayahudi kwa wakati huo ndoa zao zilikuwa ni za wake wengi! Mitume wengi walikuwa na wake wengi!
Mungu aliwatumia manabii ambao wengi walikuwa na wake wengi mpaka na masuria! Mungu hakuona ni kosa!