Ndoa ya mke mmoja ni maagizo potofu ya mwanadamu, sio Mungu. Ukweli huu hapa

Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuchelewa. Kuoa wake wengi ninaamini ni sawa kwa utamaduni wa mababu zangu na kwa dini
Hata maelezo mengi ya biblia ni tamaduni za Kirumi na Wayahudi harafu wapuuzi Fulani wanataka kulazimisha tamaduni zao Ili sisi Waafrika tuache zetu Tupate hasara.

Matokeo yake ni ushoga,usaganaji na umalaya.

Naunga mkono hoja.
 
Unaoweza kuwatunza,wake wangapi ndio nini? Kumtolea mfano yule Suleiman eti ni ubatili mtupu kwani alivyoshika utaratibu wa dini yake alifukuza wake zake wote?
 
Waefeso 5:31

Kwa sababu hiyo, mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja.”

Kwanini sio ataungana na wakeze? Kwanini iwe mkewe? Dhana ya mwili mmoja inaaply vipi watakapokuwa wanawake wengi?
 
Waefeso 5:31

Kwa sababu hiyo, mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja.”

Kwanini sio ataungana na wakeze? Kwanini iwe mkewe? Dhana ya mwili mmoja inaaply vipi watakapokuwa wanawake wengi?
Hii inahusianaje na Mungu kuumba mke mmoja na mume mmoja? Acha kupotosha watu mkuu. Lete hoja zenye mashiko sio hizi za kuokoteza. Hujaelewa hoja, rudia tena kusoma uzi utaelewa mkuu.
 
Abraham kuzaa tu na mjakazi aitwaye Hajir na kumpata Ishmael, matokeo yake ndo haya Israel vz Hamas... Hii ni changamoto kaa utu lie kupunguza changamoto
Hamas ni Wafilisti. Hawana undugu wote Na Ibrahimu. Wakati Ibrahimu anahamia Kanisani aliwakuta Wafilisti. Hakuna uzao wa Ismail pale Kanaani. Uzao wa Ismail upo Uarabuni. Wafilisti siyo Waarabu.
 
Hii inahusianaje na Mungu kuumba mke mmoja na mume mmoja? Acha kupotosha watu mkuu. Lete hoja zenye mashiko sio hizi za kuokoteza. Hujaelewa hoja, rudia tena kusoma uzi utaelewa mkuu.
Nimeuliza swali nipate ufahamu unasema napotosha tena boss?

Mada ni, mwanamume kuoa mke mmoja si maagizo ya MUNGU ni ya binadamu.

Swali: Biblia imetoa maelekezo kuwa mwanaume aachane na baba na mama yake aambatane na mkewe na wawe mwili mmoja(waefeso 5:31). Sasa kwanini haikusema aambatane na wake zake ikatumia neno mke? Na je wakishakuwa mke zaidi ya mmoja concept ya mwili mmoja itaaply vipi?

Naomba jibu mkuu.
 
Umeskika kiongozi sema sasa tujibebeshe wangapi?
Beba kadri utakavyoweza kuwatunza mkuu. Na biblia inaagiza uwapende wote kwa usawa na kuwatunza kwa usawa. Hapa ndipo wengi wanapofeli.

God never condemned polygamy, but rather he regulated it which means he approved of it. Some will try to point to Deuteronomy 17:15-17 where God says that a King shall not “multiply wives to himself” to say God was condemning polygamy.

Kula chuma hiko.
 
 
Hii inahusianaje na Mungu kuumba mke mmoja na mume mmoja? Acha kupotosha watu mkuu. Lete hoja zenye mashiko sio hizi za kuokoteza. Hujaelewa hoja, rudia tena kusoma uzi utaelewa mkuu.
Nimeuliza swali unasema napotosha tena boss.

Mada ni, mwanamume kuoa mke mmoja si maagizo ya MUNGU ni ya binadamu.

Swali: Biblia imetoa maelekezo kuwa mwanaume aachane na baba na mama yake aambatane na mkewe na wawe mwili mmoja. Sasa kwanini haikusema aambatane na wake zake?

Naomba jibu mkuu.
Sawa.
 
Umeona eeh? Kwa hiyo ni maamuzi ya mtu mkuu. Ukiamua kuoa wengi ni sawa na ukiamua kuoa mmoja pia ni sawa. Hata ukiamua usioe kabisa ni sawa. Hutendi dhambi yoyote. Sasa kwanini wanatupangia tuoe mmoja huku wakijua katazo lao ni baseless?
 
Mkuu hata mke wa pili, wa tatu na kadhalika kila mmoja wakati wa kutolewa ataachana na wazazi wake na kuungana na huyo mwanaume ambaye naye ataachana na wazazi wake.

Mkuu kwani ukiungana na mke wa kwanza mkawa mwili mmoja mwanaume unakuwa na vichwa viwili? au mikono minne?

Kanuni ya asili tu inakataa dume mmoja kuhudumia jike moja, tazama mazingira yaliyotuzunguka dume moja huhudumia majike mengi? Wanadamu ni wanyama iweje wawe tofauti?

Kwenye biblia maneno yaliyotoka kwa Mungu mubashara ni amri 10, hazikuzungumzia ndoa iwe ya wake wangapi na katika kauli za Yesu hakuna mahali alizungumzia ndoa iwe ya wake wangapi, hakuna!

Mitume wa Yesu walikuwa wayahudi, kwa mujibu wa desturi za wayahudi kwa wakati huo ndoa zao zilikuwa ni za wake wengi! Mitume wengi walikuwa na wake wengi!

Mungu aliwatumia manabii ambao wengi walikuwa na wake wengi mpaka na masuria! Mungu hakuona ni kosa!
 
Mkuu umemaliza kila kitu. Yesu hakuwahi popote pale kufundisha ndoa ya mke mmoja na alipokujq hapa duniani standard ilikuwa angalau wake wawili mpaka mitume. Hakuna hata sehemu moja anazungumzia neno hilo, na huyo ndio alizungumzia mambo hasa.

Kama Huna muda kabisa kabisa wa kusoma biblia na kujua kazi ya yesu na maonyo na makatazo yake aliyaunganishq kwenye mahubiri yake mashuhuri siku ile pale mlimani. Ile ndo ilikuwa summary ya dhumuni lake duniani. Soma tu ile na ujaribu kuishi yale maneno yake ya siku ile utakuwa mtu the best.

Ila na uzuri na ubora wote wa mahubiri yale na ndiyo alimaliziq kabisa maisha na lengo lake kwa mahubiri ya pale mlimani ila hakuongea hilo jambo na nakuhakikishia ingekuwq shida siku hiyo pale mlimani asingeliachq.

Wale wasoma English bible ile inaitwa "sermon on the mount", !!! Mimi nimeirudia na kuirudia na kurudia ile sermon!!

Na hata yule mwanamke kahaba hakuzuia asipigwe mawe maana kwa kuzuia angetengua torati, yeye alichosema tu ni kuwa basi aliyemsafi na awe wa kwanza kumponda jiwe. Since hakuwepo hakuna aliyemponda
 
Mkuu umemaliza kila kitu.
Suleimani alioa wake 300+ na masuria 700
Mi nna MKE 1 na michepuko 2 afu naitwa malaya[emoji26]
Hao ni waongo wakubwa mkuu. Usiwasikilize. Mitume wa Yesu walikuwa hadi na concubines. Kama ingekuwa polygamy ni dhambi Yesu asingeruhusu kuandamana na mitume waliooa mitala na hadi kuwa na nyumba ndogo za kutosha.
 
Ww unaepiga debe mitaala kasome Mathayo 19 , ndo utaelewa maana ya ndoa
 
Mungu angetaka hio polygamy system, angemuumbia Adam mke zaidi ya mmoja.
Ila hakufanya hivo, alimuumbia Adam mke mmoja tuu na Adam akarithika na kukaa naye maisha yake yote na hakuongezewa mke.
Yule ni Adam na Hawa
Na kama kuoa mke zaidi ya mmoja ingekuwa zambi basi Suleiman asingebarikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…