Ndoa yangu ya JF imenipatia mtoto

Ndoa yangu ya JF imenipatia mtoto

Kwanza namshukuru mungu kwa kweli, nina furaha usingizi umepotea, hamu ya msosi sina kabiisaa toka nilivyopata kifungua kinywa, nimebahatika kunywa chai tu usiku huu.

Ndugu zangu, allah ameniruzuku mtoto wa kiume jioni ya leo, mke wangu kazaa kwa njia ya operation, namshukuru mungu mama na mtoto wako salama

Kuna ndugu zangu walinipa support(kunipa moyo) kwenye jambo hili(kusaka mke JF) si vibaya nikiwapa mrejesho, si rahisi kuwakumbuka wote,
AKILI IKO HOVAS😂🤣

Thread 'Natafuta mke' Natafuta mke
Hongera sana Mzee mwenzangu.
 
Shukrani kaka.
Amin kwa duwa yako njema, atupe mwisho mwema sote.

Kwa To yeye mie nitakuwa mshenga
Amin Amin mkuu
Imekaa poa Sana ukiwa Mshenga pale Kati.

Binafsi natoa ushuhuda nilimpata mke Facebook katika group la Dini,tena hakuwa mtu wa Dini Sana na hata vaa yake hakuwa mtu wa kujistiri na alikuwa hajui mambo ya Dini.

Lakini nilimbadilisha akawa anajistiri na akawa anafanya ibada na tulidumu katika ndoa miaka Saba (7) na tumejaaliwa watoto wawili ingawa nimemuacha hakuna Baya lolote wala hakuwahi kunivunjia heshima Ila sikumpenda kivile nilivyotakiwa kumpenda (hakukuwa na chemistry)

Ninachojaribu kusema humu mitandaoni wapo watu Makini na wema na wenye Imani,ukiwa serious utampata mtu serious na mnaweza kujenga maisha pamoja.

Nawatakia kila la kheri wale wote wenye Nia njema wapate watu sahihi na hatimaye waishi pamoja kama wewe mkuu
 
Back
Top Bottom