Ndoa zimekuwaje? Kuna Video inatrend leo Mume akimkaba mkewe na kutaka kumuua live barabarani

Ndoa zimekuwaje? Kuna Video inatrend leo Mume akimkaba mkewe na kutaka kumuua live barabarani


Sent using Jamii Forums mobile app
20231224_095052.jpg
 
Habari wadau.

Video inatrend ya kaka mwenye gari aina ya IST namba T 290 CBR

Ambaye alisimamisha gari yake na kuanza kumkaba mkewe nusu kumuua huku akiongea maneno makali kwamba mkewe sio muaminifu

Tazameni video ya tukio

View attachment 2865754
Jamaa kachapiwa

Imemuuma

Na Huyo mama Wala Hana mpango nae

Solution ni kuachana tu
 
Sijui uhusiano wao ukoje ila angejizuia hasira zake huyo mkuu kwa tukio hili amejiweka kwenye mazingira ya kuanza kufuatiliwa maana sauti za kulaani na kutaka hatua zichukuliwe zitakuwa nyingi sana maana tutaanza kumuona Mama Gwajima and the like lkn huenda bora limefanyika hapo wazi maana hatujui wangefika nyumbani wakiwa wenyewe hali ingekuwaje huyo mwanamke amshukuru Mungu sana

Yote kwa yote changamoto zozote zinapotokea suluhisho siyo kugombana wala kujaa ghadhabu ukiona kwa wakati fulani hasira zimezidi bora utoke uende sehemu kwa rafiki, ndugu au hata guest ukakae huko siku ipite then mzungumze hata ikiwezekana na watu wenu wa karibu ili kutatua shida iliyopo
 
Huyu jamaa vipi, mbona kakosa busara namna hii?

Simu moja, meseji moja basi. Asipojibu tutakutana home na kuyajenga, either kibabe au kistaarabu kutegemeana na majibu yake.

Hizi ndio stories zinaishia kwenye kuuana, guys acheni kupenda kupitiliza, mapenzi ya kizazi hiki ni kuwa na balance ya kila unachofanya.
 
Back
Top Bottom