Wanawake+Wanaume, tujifunze kuishi na wenza wetu kwa akili, huwezi kudeal na mtu ambaye keshapaniki kwa kumuelewesha, uyo mtu anakua refers as chizi, anaweza fanya lolote hata kama akiwa ke, kumjibu ama kujitetea ni kama unaongeza tatizo.
*Kwenye mahusiano ya ndoa usije ukachukulia poa vimakosa vidogo vidogo huwezi kujua mwenza wako anaviwaza kwa ukubwa gani.
*Ukijua umezingua usione tabu kuandaa mapema mazingira ya kumuweka sawa mwenza wako, jaribu kuwaza mapema kitu ambacho atakua kinampa mashaka alafu kitafutie ufumbuzi mapema kabla hamjakutana ili akifika tuu unampa maelezo yote vizuri sio mpaka mtu akuhoji au akuelezee kosa lako.
*Zitambue akili za mwenza wako, kila mtu anaufahamu wa tofauti, hayupo mtu aliyekamilika, kila mtu hua anakitu chake anachokhofia, ukikipenda sana kitu lazima ukikhofie, mfano kwa uyo mtu hapo (video) utagundua kawekeza sana kwa mke wake (familia), anakhofia sana kumpoteza mke ila hataki kuatreated kama bwege kisa upendo wake kwa mke so ni simple tu kwa mke kama atazielewa akili za mme wake.
Mwisho wa siku UPENDO ndo huzalisha MAPENZI, bila upendo hamfiki popote, mpende mwenza wako mpaka wenzako wakuone bwege. Kuna wale wadada saloon utawasikia asee naona nachelewa ntasuka kesho ngoja niwahi kumpikia baba changa wangu, na kuna baadhi ya wanaume pia utawasikia asee leo sijui kama ntacheki mpira maana huu muda nikizidisha wife atanuna kichizi. So unapata jawabu kabla ya mapenzi kuna upendo, hamuwezi kuenjoy mapenzi kama hamna upendo kwa wenza wenu, msichanganye vitu.