Ndoa zinakufa kila kukicha siku hizi

Ndoa zinakufa kila kukicha siku hizi

Hazard CFC

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2015
Posts
16,627
Reaction score
38,689
Mitaani huku ndoa zinavinjika kila kukichaa, leo asubuhi nimekutana na magazeti mawili mmoja mke wa rafiki yangu na mwingine mke wa mjomba wangu wote wanataka kutundika daruga nimekosa cha kuwashauri maana mimi mwenyewe ni mhanga miezi kadhaa iliopita nimepigwa pia na kitu kizito... Sababu walizonieleza ni zile zile nilizopewa mimi kwamba tunadharau,matusi yasiovumilika wao hawana shida na michepuko yetu hata wawe mia tutajijua wenyewe ila matusi dharau mbele ya watoto kuwaona dhaifu na kawaona kama tunawafuga ndio kitu walichoshindwa kuvumilia.

Kama hujaoa kijana mwenzangu hakuna haja ya kuoa
 
Ndoa kabla hazijafungwa

Watu wapimwe afya zao za akili kwanza.

Siku hizi kuna ndoa hazifati hata msingi wa ndoa.

Imagine ndoa inafungwa mke anafanya kazi na kuishi Dar. Mume anafanya kazi na kuishi Musoma.

Imagine ni Wanandoa ila kila mtu anaishi kwake. Toka ndoa inaanza mpaka inakwisha wanandoa hawajawai hata kuishi pamoja
 
Kumbe watu wanaoa na kuolewa kwa sababu ya ngono? lazima zivunjike ... tena zisambaratike zote. kuna umuhimu wa kujua kwa nini watu wanaoa na kuolewa. ngono itawaponza mtakosa maana ya ndoa mkiendekeza mawazo ya ngono.
 
Mwaka wa kumi na moja huu nipo kwenye ndoa mimi hizo vurugu sizioni nazisoma tu Jamiiforums kama hivi.

Inaweza kuwa kuna tatizo lakini siyo kubwa kiasi hiko sometimes linachangiwa na ninyi wanandoa wenyewe,case kubwa ni kukosa uaminifu au kuonyesha dalili za kukosa uaminifu wanandoa mkiviepuka hivi na kuishi maisha ya uwazi ndoa kudumu ni kitu rahisi sana.
 
Kumbe watu wanaoa na kuolewa kwa sababu ya ngono? lazima zivunjike ... tena zisambaratike zote. kuna umuhimu wa kujua kwa nini watu wanaoa na kuolewa. ngono itawaponza mtakosa maana ya ndoa mkiendekeza mawazo ya ngono.
Kumbe sababu ya ndoa ni Nini? Ushawahi kujiuliza kwann mahanithi (wasiosimamisha mdudu ) hawaruhusiwi kufunga ndoa?

Kama unadhani sababu ya ndoa ni tofauti na ngono unajidanganya.
 
Mitaani huku ndoa zinavinjika kila kukichaa, leo asubuhi nimekutana na magazeti mawili mmoja mke wa rafiki yangu na mwingine mke wa mjomba wangu wote wanataka kutundika daruga nimekosa cha kuwashauri maana mimi mwenyewe ni mhanga miezi kadhaa iliopita nimepigwa pia na kitu kizito... Sababu walizonieleza ni zile zile nilizopewa mimi kwamba tunadharau,matusi yasiovumilika wao hawana shida na michepuko yetu hata wawe mia tutajijua wenyewe ila matusi dharau mbele ya watoto kuwaona dhaifu na kawaona kama tunawafuga ndio kitu walichoshindwa kuvumilia.

Kama hujaoa kijana mwenzangu hakuna haja ya kuoa
Kwa hiyo wazee wa kataa NDOA wako sawa? 🤣🤣
 
Back
Top Bottom