Ndoa zinakufa kila kukicha siku hizi

Ndoa zinakufa kila kukicha siku hizi

Mwaka wa kumi na moja huu nipo chamani mimi hizo vurugu sizioni nazisoma tu Jamiiforums kama hivi.

Inaweza kuwa kuna tatizo lakini siyo kubwa kiasi hiko sometimes linachangiwa na ninyi wachezaji wenyewe
Miaka kumi na nne Toka nimjue mwamba aiseee ....katika vitu nainjoi ni hii ndoa,huyu kaka libarikiwe tumbo lililokuzaa,ananihurumiela na kunitunza sana jaman,Yuko tayari akose Mimi nipate,
 
Kumbe sababu ya ndoa ni Nini? Ushawahi kujiuliza kwann mahanithi (wasiosimamisha mdudu ) hawaruhusiwi kufunga ndoa?

Kama unadhani sababu ya ndoa ni tofauti na ngono unajidanganya.
moja ya lengo la ndoa ni kuzaliana. ili kuzaliana ndio kuna hicho kipengele cha ngono. Hatuwezi kufunga ndoa kwa ajili ya ngono tu. Lazima uangalie na malengo mengine. na ndio sababu ndoa zote zinazolenga ngono tu zinakufwaaa na kusambaratika.
 
Ndoa kabla hazijafungwa

Watu wapimwe afya zao za akili kwanza.

Siku hizi kuna ndoa hazifati hata msingi wa ndoa.

Imagine ndoa inafungwa mke anafanya kazi na kuishi Dar. Mume anafanya kazi na kuishi Musoma.

Imagine ni Wanandoa ila kila mtu anaishi kwake. Toka ndoa inaanza mpaka inakwisha wanandoa hawajawai hata kuishi pamoja
hii ndio naitaka mimi kwasasa!
 
Mitaani huku ndoa zinavinjika kila kukichaa, leo asubuhi nimekutana na magazeti mawili mmoja mke wa rafiki yangu na mwingine mke wa mjomba wangu wote wanataka kutundika daruga nimekosa cha kuwashauri maana mimi mwenyewe ni mhanga miezi kadhaa iliopita nimepigwa pia na kitu kizito... Sababu walizonieleza ni zile zile nilizopewa mimi kwamba tunadharau,matusi yasiovumilika wao hawana shida na michepuko yetu hata wawe mia tutajijua wenyewe ila matusi dharau mbele ya watoto kuwaona dhaifu na kawaona kama tunawafuga ndio kitu walichoshindwa kuvumilia.

Kama hujaoa kijana mwenzangu hakuna haja ya kuoa
acha kudanganya watu
 
Mwaka wa kumi na moja huu nipo chamani mimi hizo vurugu sizioni nazisoma tu Jamiiforums kama hivi.

Inaweza kuwa kuna tatizo lakini siyo kubwa kiasi hiko sometimes linachangiwa na ninyi wachezaji wenyewe
mdogo wangu kwa umri huo ninyi bado wachumba tu.
ila vurugu lazima zitatokea hawa viumbe wanaitwa wanawake ni watata sana kuwa mpole tu.
katika umri wako nilikuwa natongoza michepuko kwa nyodo sana na wengine nawaambia kabisa mke wangu ananipenda sana ila uloho tu ndo unaniponza na bado eti mwanamke anakubali!
 
Mitaani huku ndoa zinavinjika kila kukichaa, leo asubuhi nimekutana na magazeti mawili mmoja mke wa rafiki yangu na mwingine mke wa mjomba wangu wote wanataka kutundika daruga nimekosa cha kuwashauri maana mimi mwenyewe ni mhanga miezi kadhaa iliopita nimepigwa pia na kitu kizito... Sababu walizonieleza ni zile zile nilizopewa mimi kwamba tunadharau,matusi yasiovumilika wao hawana shida na michepuko yetu hata wawe mia tutajijua wenyewe ila matusi dharau mbele ya watoto kuwaona dhaifu na kawaona kama tunawafuga ndio kitu walichoshindwa kuvumilia.

Kama hujaoa kijana mwenzangu hakuna haja ya kuoa
Ni bora ndoa zife na watu wabakie, kuliko watu wafe na ndoa zife.
 
mdogo wangu kwa umri huo ninyi bado wachumba tu.
ila vurugu lazima zitatokea hawa viumbe wanaitwa wanawake ni watata sana kuwa
mpole tu.
katika umri wako nilikuwa natongoza michepuko kwa nyodo sana na wengine nawaambia kabisa mke wangu ananipenda sana ila uloho tu ndo unaniponza na bado eti mwanamke anakubali!
Haya nimekuwa nikiambiwa miaka yote tangu naoa hadi leo siyaoni yakinifika,sisemi ni mazuri hasha.

Mimi ni mwepesi wa kujifunza na hii yako naichukua kama lessons ukichukulia maisha hayana mwalimu,naendelea kujifunza bado sijamaliza.
 
moja ya lengo la ndoa ni kuzaliana. ili kuzaliana ndio kuna hicho kipengele cha ngono. Hatuwezi kufunga ndoa kwa ajili ya ngono tu. Lazima uangalie na malengo mengine. na ndio sababu ndoa zote zinazolenga ngono tu zinakufwaaa na kusambaratika.

Bila ndoa hatuzaliani??
 
KATAA NDOA
kwa kauli hii naomba niandike kitu kigumu kidogo kwa kadri nionavyo mimi.
pia inawezekana ipo ajenda ya siri ya kuitawala Afrika kwa njia nyingine ikiwemo kupunguza kuzaliana kwao.
kwa kuwa ndoa huongeza familia kwa kiasi kikubwa.
  1. kukataa ndoa ni nje ya maadili yetu kama waafrika na jamii kiukweli haiwezi kukuheshimu na hasa ukiwa mwanaume. unaonekana hujakamilika hataka kama unawatoto na shughuli zako wanazijua lakini lazima udharauliwe.
  2. unaonekana huwezi kuwa na majukumu na huwezi kuaminika.
  3. unawaongezea watu dhambi ya kukujadili kila kukicha.
  4. unaonekana mvivu na mchoyo kiasi kuwa umejiwekea wigo wa peke yako.
  5. yapo mazingira ya kujikataa na matokeo yake yanaweza kuwa:-
    1. kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja
    2. umalaya kupita kiasi
    3. ulevi na utumiaji wa madawa ya kulevya
    4. uvivu na malalamiko
    5. magonjwa ya kuambikiza na yasiyoambukiza
  6. kuwa mbali na ibada na kudharau imani za wengine.
yapo mengi lakini kiukweli usikubali kauli ya kukataa ndoa.
wanawake wao hawanajinsi asipotokea wanafanyaje lakini kwa kijana wa kiume kukataa ndoa ni kutokukamilika.
 
Back
Top Bottom