Ndoto: Hivi mwanasiasa wa kiume anawezaje kushinda Miss Tanzania?

Ndoto: Hivi mwanasiasa wa kiume anawezaje kushinda Miss Tanzania?

Ni ngumu kwa Mwanaume kushinda Miss Tanzania hiyo December na haiwezi kutokea.
 
Eti mwenyekiti wa ccm taifa awe mwanaume?

K for kawaida wa uvficm na r for rehema, makam wa k.
 
Yale mashindano ya Umiss ndo yanafanyika Dodoma sasa, kwahyo tusubili kuona huyo mwanaume atakayeshinda
 
Herufi sijaiweka hapa maana nikiiweka tu kila mtu atamjua,herufi naogopa kuitaja maana ntaleta taharuki kwa muhusika.Lakini sijui nini kitamtokea MAMA hausiki kabisa na hii ndoto mwacheni ale BATA bila wasi wasi
Herufi pekee Bila kupepesa macho mtu ataijua ni "JK" hizo nyinginezo sio Rahisi!
 
Herufi sijaiweka hapa maana nikiiweka tu kila mtu atamjua,herufi naogopa kuitaja maana ntaleta taharuki kwa muhusika.Lakini sijui nini kitamtokea MAMA hausiki kabisa na hii ndoto mwacheni ale BATA bila wasi wasi
Wataanza na shina kwao kumstaafisha mstaafu halafu HUYO mwingine atakaa pembeni mwenyewe!
 
Asalam aleykum!

Jamani haya maisha yanachekesha sana na ukiyafikiria sana unaweza kupasuka kichwa, basi juzi kuamkia jana bwana kama kawaida katika ndoto niko sehemu kama nimesimama hivi. Nilikuwa kama kuna mtu amenisimamisha anataka kuniambia jambo fulani, kwa mbalii nikawa kama nasikia minong'ono ya kuhusu MISS Tanzania halafu mashindano yenyewe yanafanyika mwezi wa kumi na mbili yaani December.

Basi ghafla kuna mtu akanifungulia file ananionyesha washiriki na watu watatu ambao wanaweza kushinda. File lilikuwa na picha na majina ya wagombea. Washiriki walikuwa wengi lakini nikamulikiwa taa kwenye watu watatu ikawa kama wengine hawaonekani vizuri wamezibwa na kiza.

Kuna mtu mmoja sasa katika wale watu watatu taa ikamulika sana kwenye jina na picha yake coz yeye ndio atayeshinda, ilimulika mfano wa indicator za gari zinavyoashiria kwamba gari inapita kulia au kushoto, yaani ilikuwa inafanya muli muli muli muli, jambo lililonishangaza ni:

1. Mwanasiasa wa kiume anawezaje kuja kushinda MISS TANZANIA?
2. Je ni kweli kwamba mwezi wa kumi na mbili kutakuwa na shindano la Miss Tanzania.
3. Kwanini herufi ya mwanzo ya jina lake ilikuwa inaleta majina tofautu tofauti mengi kwa staili ya kimuli muli mpaka nikashindwa kulisoma vizuri, yaani jina ni la fulani lakini likawa linajichanganya changanya na majina mengine lakini herufi ya mwanzo ni hiyohiyo?

Yaani kama ni K au R ni hiyo hiyo

NB: Haya sio maono bali ni ndoto tu ya kawaida jamani lakini inaweza kuwa na uhalisia wa jambo fulani
Jibu la swali lako lipo kwenye maana ya hii methari ya NGURUWE KAVAA HIJABU
 
Huyu mtu ndoto zake zote zinatimia! Kama ni hatari tuambie tuombee Taifa ila kama ni vinginevyo ngoja tuwe na subira. Ndio maana wenye akili nyakati hizi hazitaki ushabiki! Mambo yanaweza kubadilika ukakosa pa kuweka sura.
Kwa ujiniasi wangu ...mambo ya hatari na yakutisha ndiyo yanayo takiwa sasahivi Tanzania ...wala siyo wakati wa kuyaombea yasitokee .na yasipo tokea mambo ya hatari kwa wakati huu tuliopo basi tumekwisha narudia tumekwisha
 
Back
Top Bottom