TUJITEGEMEE
Platinum Member
- Nov 6, 2010
- 27,646
- 28,747
Ninachokijua nikuwa waziri Mkuu anapatikana kutokana na "uwezo" wake kutekeleza majukumu ya uwaziri mkuu! Suala la jinsia kutumika kumpata waziri mkuu, ni matumizi mabaya ya maneno ya "usawa kwa wote ama haki kwa wote"!
Kutumia jinsia katika maamuzi ya kufanyai kazi nyeti ama nyinginezo ni aina fulani ya ubaguzi ! Kutekeleza jambo la msingi kuna hitaji uwezo wa kufanya jambo hilo bila kujali jinsia, kabila, rangi, na mengine kama hayo ya kibaguzi.
Nyakati hizi tuachane na ubaguzi wa namna hii katika kutafuta watu wa kulisaidia taifa hili kujitegemea kiuhalisia. Tuna mambo mengi ya kufanya hatuwezi kufanya michezo michezo ya ajabu katika suala hili ama lingine linalofanana na hili.
Kwa maneno mepesi kabisa, siungi mkono hoja ya mleta mada kwa namna yoyote ile.