Ndoto No 8 na 4 ni ndoto moja ila imekuja kwa aina tofauti ila ina maana moja.
Nitakuelezea ila neno linasema tumeketishwa pamoja na Kristo .
Na Kristo ameketi juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia
22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwaajili ya kanisa ambalo ..23 mwili wake, ...
Efeso 1:20-23
## kanisa ni sisi
Sisi ni mwil wa KRISTO ndio maana anasema tutoe miili yetu iwe dhabihu timilifu
Ufunuo 3:21
Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika chake cha enzi
Kama Kristo yupo juu hata sisi tunatawala pamoja naye
Lakini lazima ushinde ndipo utaketi
Sijui nikueelezee vip
Ila ni aina ya ndoto kuwa upo juu ya wa wengine
Naweza unganisha pia na ndoto ya uongozi.( ukijichunguza angalia watu wanakuchukuliaje na kama haupo hivyo)
Turudi ktk ndoto ya hiyi ng'ombe
Ng'ombe ni miungu .
Turud kipindi cha Musa wakat Musa yupo mlimani( Sinai). Haruni na wengine walitengeneza mungu kwa muundo wa ndama
Kutoka 32:1-8( soma)
2 Haruni akawaambia zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu mkaniletee.
4b akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha, nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israel, iliyo kutoa katika nchi ya Misri
Ndama( ng'ombe) ni miungu/ mizimu
Sijajua kuna nini lakini rudi nyuma angalia familia ukute kuna maagano
Ndio maana unakwama mahali hata Mungu akitaka kuongea kuna vitu vingone hasemi sababu kuna miungu mingine( inahitajika toba ili Mungu akae katika nafasi yake. Toba inampa Mungu uhalali wa kumiliki familia au eneo kwa nguvu zaidi)
Soma habar yote ya Musa sura ya 32 yote
** samaki sijaua. Huyo samaki umeota kwa kivipi wanafanyaje
Nyoka. Nyoka turejee mwazo
Nyoka ni Ibilisi, nyoka anatumiwa na shetani au watu wa nguvu za giza
Nyoka ni sumu kila mara unapoota nyoka ujue kuna vita unavyo hivyo lazima ujue kuomba maombi ya vita ili Mungu akushindie
Soma ufunuo 12 Yote.( Mungu akufungue macho ya kuomba viziuri tumia Neno ili kufanya maombi kuhusu kuhusu huyo nyoka
Mungu aingilie kati Mikael malaika waingilie kati kupigana na huyo nyoka
Na Mwana Kondoo wa Mungu akushindie.
Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana Kondoo ufunuo 12:11
Tumia damu Ya Yesu kuomba pia
Nielezee vizur hiyo kucheza mpira imekuwaje?
Sijui umepata kitu hapo.
Palipo pungua Roho Mtakatifu akuongezee zaid