Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Inategemea na imani yako. Kisayansi wanasema ni uchovu wa fikra pengine upande wa kazini kwako kuna stress hivyo ndoto hiyo inaakisi fikra zako.
Kijadi hiyo ndoto inaashiria uadui maana nyoka daima anawakilisha uadui kiasili. Kwa vile umeota upo kazini hivyo moja kwa moja inaakisi uadui unaokuzunguka kazini ama unapopatia riziki yako inawezekana usiwe wa dhahiri, inaweza ika hata wa wivu tu. Kitendo cha kujihudumia mwenye kunamaanisha umevuka uadui huo na pia kuambiwa kwako juu ya kung'atwa kunamaanisha wapo walio wema kwako.
Narudia tena kulingana na imani yako basi utajua jinsi gani ya kuichukulia ndoto yako. Cha muhimu ni kumuweka Mungu mbele ili akuepushe na mabalaa uyaonayo na usiyoyaona.
Kwa kijadi hapo ndo kuna ukweli
Je nifanyeje mkuu
 
Mkuu freedom tomorrow haya ndo mambo yake kama vip mtimbie inbox akutatulie utata
 
Funga na kuomba ili uepuke mawe ndani ya fuko la sandarusi hata kama watakuua.
 
Huyo nyoka aliyekuuma ni yule wa kijani....na ungeendelea Kulala ungejikuta uko kwenye mfuko shukuru sana umeshituka kabla hujaingia kwenye mfuko.
 
Kuna ndoto huwa zinajirudia ila nikiri hii ndio mara yangu ya kwanza naota hii ndoto.
Usiku wa kuamkia leo nimeota nimekufa na kuwekwa kwenye jeneza, chanzo cha kifo sijakifahamu ila mwili ulikuwa umeharibika vibaya kama MTU aliyekufa maji, kuna wakati jeneza liliwaponyoka wabebaji na kujipigiza chini na hayo yote nimeyashuhudia kama mtazamaji wakati mwili ulikuwa wangu.

Mwili ulizikwa kama mlimani hivi na kulikuwa na mawe mengi kiasi hata shimo lilikuwa fupi na hata udongo wa kufukia ulikosa na ikawalazimu kunifukia kwa mawe tu! Jambo la ajabu wakati yote yanatokea sikuwa naogopa na badala yake nilikuwa natafakari juu ya eneo nilipozikwa, nilifurahi zaidi pale nilipoona jirani kabisa na nilipozikwa kulikuwa na sanamu kubwa ya Bikira Maria(kwa wakatoliki wanafahamu zaidi) likiwa limeiangalia kaburi hiyo.

Sikuwa na hofu hata kidogo, jambo lililonifanya nine kuomba ushauri au tafsiri hapa ni jinsi ndoto ikivyokuwa "clear" kiasi kwamba hadi muda huu naandika hapa bado nakumbuka kila picha hadi rangi, waombolezaji hawakuwepo!
 
Ndoto nadhani ni maisha tunayoishi tukiwa usingizini.....mm uwa naota nchi inavamiwa na inataka pinduliwa naiokoa....mara nkimbizwa na wachawi.....ndoto hizi ujirudia mara nyingi.....zaidi kuliko zote ni ndoto za nyoka.....na uwa hawanig'ati!
 
Hapa ndio simuelewi Freud, dreams are a fulfilment of a wish- really?
 
Hongera kwa kufa na kuzikwa jirani na sanamu ya Bikira Maria mkuu.
Tafsiri ya ndoto ngoja watakuja akina mshan jr
 
Ukiota unakimbizwa na nyoka kaa vizuri na Mungu wako shetani anakuwinda atakuletea mabaya. Kufukuzwa na wachawi ina maana wabaya wanakuchunguza nyendo zako kukuharibia. Unatakiwa kuzuia hio hali kwa maombi ya vita.
 
Kwanza mkuu, tuanze kukifaham chanzo cha ndoto. Nyingi huja kwa sababu ya mawazo fulani, nyengine huja kwa ulaji fulani, nyengine huja kwa maneno mengi, nyengine ni maonyo kuhusu mambo yajayo.
Sasa tuseme hivi;
Zile nyingi tunaota kwa sababu ya vyakula tulivuokula. Ugali kwa kabichi utaota tu. Viazi mbatata kwa nyam chom lazima utaota tu. Hizi ndoto hazina maana yeyote kwako.
Zile za mawazo fulani au maneno mengi. Unakuwa una mawazo kichwani mwako. Mawazo makubwa, mazito na au ya kukukera. Unaenda kulala huku una haya mawazo. Utaota tu jambo linaloshabihiana na ulichokuwa unawaza/unanena.
Zile za kuhusu mambo yajayo. Hizi huoteshwa mtu, akaambiwa habari flani ijayo. Utaona wazi wazi kuhusu jambo flani. Huwa inajirudia usiku huo huo. Yaweza kuja kama mwanzo au ikakuletea kitu kingine ila kinashabihiana.
Hii ndoto yako, yaweza kuwa inakuhusu. Kifo chako kwa kuwa hukuogopa wala kufadhaika inamaanisha kuwa utabadilika kabisa baadhi ya tabia zako kuu.
Mfano;
Kama weye ni mlevi wa kitu chochote, pombe, bangi, uzinzi, picha chafu etc. Kutatokea kitu, utaacha kabisa tabia hiyo. Utaizika mwenyewe tabia yako chafu.
Sababu itakuwa ni kuwa umejulikana na aibu itakayokupata utaacha tu. Muda utatokana na kama hii ndoto itakurudia tena.
 
Kuna ndoto huwa zinajirudia ila nikiri hii ndio mara yangu ya kwanza naota hii ndoto.
Usiku wa kuamkia leo nimeota nimekufa na kuwekwa kwenye jeneza, chanzo cha kifo sijakifahamu ila mwili ulikuwa umeharibika vibaya kama MTU aliyekufa maji, kuna wakati jeneza liliwaponyoka wabebaji na kujipigiza chini na hayo yote nimeyashuhudia kama mtazamaji wakati mwili ulikuwa wangu.

Mwili ulizikwa kama mlimani hivi na kulikuwa na mawe mengi kiasi hata shimo lilikuwa fupi na hata udongo wa kufukia ulikosa na ikawalazimu kunifukia kwa mawe tu! Jambo la ajabu wakati yote yanatokea sikuwa naogopa na badala yake nilikuwa natafakari juu ya eneo nilipozikwa, nilifurahi zaidi pale nilipoona jirani kabisa na nilipozikwa kulikuwa na sanamu kubwa ya Bikira Maria(kwa wakatoliki wanafahamu zaidi) likiwa limeiangalia kaburi hiyo.

Sikuwa na hofu hata kidogo, jambo lililonifanya nine kuomba ushauri au tafsiri hapa ni jinsi ndoto ikivyokuwa "clear" kiasi kwamba hadi muda huu naandika hapa bado nakumbuka kila picha hadi rangi, waombolezaji hawakuwepo!
Kwa TZ ya leo kutangaza hadharani ndoto au maono uliyoyaona ni kosa la Jinai kwa tafsiri ya sheria za serikali ya awamu ya 5!

Kama Unataka kwenda aliko Lema hivi sasa, endelea kutupa hizo story za ndoto zako...
 
Ukiota unakimbizwa na nyoka kaa vizuri na Mungu wako shetani anakuwinda atakuletea mabaya. Kufukuzwa na wachawi ina maana wabaya wanakuchunguza nyendo zako kukuharibia. Unatakiwa kuzuia hio hali kwa maombi ya vita.

Mkuu;
Acha kuwatishia watu kihivyo. Sio kila nyoka ni mbaya. Nyoka wa kijani ni bahati kubwa inakujia. Nyoka mweusi ni jaribu linakujia. Nyoka wa rangi ya udongo ni kupoteza fweza yaani utapata hasara katika biashara/shughuli. Ukubwa wa nyoka ndo ukubwa wa unachokuja pambana nacho.
 
Kwanza mkuu, tuanze kukifaham chanzo cha ndoto. Nyingi huja kwa sababu ya mawazo fulani, nyengine huja kwa ulaji fulani, nyengine huja kwa maneno mengi, nyengine ni maonyo kuhusu mambo yajayo.
Sasa tuseme hivi;
Zile nyingi tunaota kwa sababu ya vyakula tulivuokula. Ugali kwa kabichi utaota tu. Viazi mbatata kwa nyam chom lazima utaota tu. Hizi ndoto hazina maana yeyote kwako.
Zile za mawazo fulani au maneno mengi. Unakuwa una mawazo kichwani mwako. Mawazo makubwa, mazito na au ya kukukera. Unaenda kulala huku una haya mawazo. Utaota tu jambo linaloshabihiana na ulichokuwa unawaza/unanena.
Zile za kuhusu mambo yajayo. Hizi huoteshwa mtu, akaambiwa habari flani ijayo. Utaona wazi wazi kuhusu jambo flani. Huwa inajirudia usiku huo huo. Yaweza kuja kama mwanzo au ikakuletea kitu kingine ila kinashabihiana.
Hii ndoto yako, yaweza kuwa inakuhusu. Kifo chako kwa kuwa hukuogopa wala kufadhaika inamaanisha kuwa utabadilika kabisa baadhi ya tabia zako kuu.
Mfano;
Kama weye ni mlevi wa kitu chochote, pombe, bangi, uzinzi, picha chafu etc. Kutatokea kitu, utaacha kabisa tabia hiyo. Utaizika mwenyewe tabia yako chafu.
Sababu itakuwa ni kuwa umejulikana na aibu itakayokupata utaacha tu. Muda utatokana na kama hii ndoto itakurudia tena.
Asante sana mkuu angalau kuna mwanga flani kwenye maelezo yako.
 
Maana yake uache kuamini sanamu maana hayo yatakupeleka kwenye kifo cha rohoni.Utakua mzima kimwili lakini kiroho ulishazikwa.
 
Back
Top Bottom