Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Umefungishwa ndoa na majini katika ulimwengu wa roho,

Hakikisha unaomba lasivyo kuolewa kwako itakuwa shida, cz kila mwanaume anayekuja kwako atakuta umewahiwa na mtu na atakuacha,

Au ukiolewa ndoa itakuwa na migogoro

Hivyo vunja hiyo ndoa yote
Msubirie Heaven Sent akuelekeze vipengele vya kufuata



In ua Presence Jesus is where I belong
Sawa nasubiriaa
 
Je ukiota unaongea na mtu ambaye alishakufa ina maana gani labda anakuonya usifanye hichi na hichi hua ina maana gani manake mm nmewah ota nazungumza na baba alishafariki mm nkawa namwogopa namwambia ww si ulishakufa lakini akawa anasema usiogope we karibu huku ndo nyumban kwangu ati ananiambia hivyo alafu palikua na uwanja mkubwa tu ila nkawa naona kamba ndefu ya kupanda unaenda juu nikawa najisemea kimya kimya apa akigeuka tu nakimbilia kamba nimtoroke nlishituka dahh jasho kila mahali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amina nashukuru sana kwa muda wako.
Nimekuelewa kiongozi nityafanya hivyo.
Kwanza miaka ya 2009 -2010 ilikuwa ni magari madogo ila meupe na nilikuwa napanda sigombanii ila ninaokuwa nao maranyingi sikuwa nawatambua na sifiki mwisho wa safari.
Kwenye mabasi Mara nyingi nagombania na ndugu
Mazingira huwa ni ya Miji Mikubwa.
Kwenye bus nimewahi kufanikiwa kuingia na kuanza safari mara moja ila nilikaa na mama mmoja mnene kavaa ushungi ila simfahamu na sikufanikiwa kufika nilipokuwa naenda na sijui nilikuiwa naenda wapi.
Yaani kwa kifupi tu hapo wewe umuombe Mungu akufanikishe safari yako. Ukichunguza maisha yako katika yale uliyopanga kutimiza na hii ndoto vina uhusiano. Ni wazi una ndoto za kufika sehemu katika maisha japo huenda Mungu anataka kukufikisha mahali ambapo hata uwezo wa akili yako haujafikiria bado. Pia wapinzani ni wengi unaowajua na usiowajua. Mwangalie Mungu zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi huwa naota nipo shule nafanya mtihani au nipo nawahi mtihani nakimbia sana au nipo nasoma katika mazingira magum katika hofu ya kufeli mtihani hyo ndoto huwa inajirudia toka 2014 na mim shule nilsha maliza muda mrefu sana
Kwa mtazamo wako unaona kama umemaliza shule lakini kiukweli bado hujamaliza! Wakati mwingine ukitaka kuhakikisha hili angalia baada ya kumaliza elimu yako umeajiriwa? Na je? Hiyo ajira inakulipa sawa na kiwango cha elimu yako? Pia usisahau mitihani mbalimbali ya maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoto no2 tafuta somo la malango nilijibu vizur hiyo sehemu. Na nilielekeza jins ya kuomba na kuna mahali Heaven Sent alielekeza

Darasa ni hatua ya maandaliz fulan ktk maisha

Darasa ni ngazi ya kupanda daraja ili ufikie hatua nyingine. Huwez kuvuka darasa had ufahuru mtihani vizuri

Tuliangalia daniel 1 yote ( soma) maelezo nitakutag somo la malango


Hayo maneno mene mene tekeli na peresi unayapata daniel 5:25

Soma tano yote ( daniel 5 yote)
Huyu mfalme Beltshaza alitumia vyombo vya hekalun vibaya na kuisifu miungu yao bila kujal kuwa wanatumia vyombo vitakatifu vya Mungu

Hayo maneno ukisoma ktk Biblia
Mene=Mungu ameuhesabia ufalme wako na kuukomesha.

27 TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka

28 PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi

## baada ya kuambiwa hayo maneno huyo mfalme usiku aliuawa.

# ni kuwa mtu mwenye cheo au mamlaka anavuliwa mamlaka yake yote na wanapewa watu wengine


Umeweza kuwa ww ni kiongozi halafu uvuliwe madaraka.

*** ukitaka kuomba kama eneo lina shida nilifundishwa hichi kitu

Kama wachawi wanakusumbua / waganga ktk eneo . omba toba vizur baadaye tamka au andika ktk ardhi waganga wotee au wachaw wote MENE MENE TEKELI NA PERESI

Inamaana umeandika kuwa hawatomiliki hapo hawata tawala na hawawez kulala hapo lazima wahame( ukiwa na imani. Maandiko yanasema sawa sawa na imani yako pokea)

Bt lazima uombe toba vzr ya hilo eneo na ardhi.
## turud ktk ndoto hayo maneno uliyaona ktk mazingira gani nashindwa kufafanua kwa upande wako sababu ndoto lazima iwe na mwanzo.

Lakin natumain umepata kitu kidogo.

Tuje hiyo ya vitani

Kiongozi lazima awe mstar wa mbele kuongoza kundi katika vita au amani

Tuangalie Yoshua 8:1-19( soma upate kitu cha kukuvusha)

Kisha BWANA akamwambia Yoshua, Usiache, wala usifadhaike, wachukue watu wote wa vita waende pamoja nawe, nanyi inukeni, mwende Ai, angalia, mimi nimemtia mkononi mwako huyo mfalme wa Ai, na watu wake, na mji wake, na nchi yake, ...

## hiyo ni Yosh 8:1
Unaona alikua kiongozi hivyo ukiwa kiongoz vita huwez kuviepuka vya kiroho au kimwili

Lakini lazima ujifunze kuwa Vita ni Bwana yeye ndiye anayetupigania vita na si kwaakil zetu

Ktk ndoto yako hiyo vita unashinda au hushindi?

Kama hushindi rud kwa Mungu mwambie kama ulivyo mshindia vita Daudi na mimi naomba nishindie

1Samwel17:47
Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba BWANA haokoi kwa upanga wala kwa mkuki, maana vita ni vya BWANA, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.

Mungu ni BWANA WA MAJESHI( ndiye anayeongoza vita)

## kuna kitu ndani cha uongozi lakin lazima ukae ktk mapenz ya Mungu ilo uvuke

Muulize Mungu mapenzi yako ni yepi kwangu. Atakuambia


Naendelea...
Divine mimi nataka niku follow sijui namna ya kufanya, maana nimepima maelezo ya majibu yako nimeona wewe siyo msanii ni mtumishi Wa Mungu kweli, ni mtu wa imani kweli siyo mbabaishaji. Napenda kujifunza zaidi kupitia watu wa aina kama yako. Thanks

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoto No 8 na 4 ni ndoto moja ila imekuja kwa aina tofauti ila ina maana moja.

Nitakuelezea ila neno linasema tumeketishwa pamoja na Kristo .

Na Kristo ameketi juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia

22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwaajili ya kanisa ambalo ..23 mwili wake, ...

Efeso 1:20-23


## kanisa ni sisi
Sisi ni mwil wa KRISTO ndio maana anasema tutoe miili yetu iwe dhabihu timilifu

Ufunuo 3:21
Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika chake cha enzi

Kama Kristo yupo juu hata sisi tunatawala pamoja naye

Lakini lazima ushinde ndipo utaketi
Sijui nikueelezee vip

Ila ni aina ya ndoto kuwa upo juu ya wa wengine
Naweza unganisha pia na ndoto ya uongozi.( ukijichunguza angalia watu wanakuchukuliaje na kama haupo hivyo)

Turudi ktk ndoto ya hiyi ng'ombe
Ng'ombe ni miungu .

Turud kipindi cha Musa wakat Musa yupo mlimani( Sinai). Haruni na wengine walitengeneza mungu kwa muundo wa ndama

Kutoka 32:1-8( soma)
2 Haruni akawaambia zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu mkaniletee.

4b akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha, nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israel, iliyo kutoa katika nchi ya Misri

Ndama( ng'ombe) ni miungu/ mizimu
Sijajua kuna nini lakini rudi nyuma angalia familia ukute kuna maagano
Ndio maana unakwama mahali hata Mungu akitaka kuongea kuna vitu vingone hasemi sababu kuna miungu mingine( inahitajika toba ili Mungu akae katika nafasi yake. Toba inampa Mungu uhalali wa kumiliki familia au eneo kwa nguvu zaidi)

Soma habar yote ya Musa sura ya 32 yote

** samaki sijaua. Huyo samaki umeota kwa kivipi wanafanyaje



Nyoka. Nyoka turejee mwazo
Nyoka ni Ibilisi, nyoka anatumiwa na shetani au watu wa nguvu za giza

Nyoka ni sumu kila mara unapoota nyoka ujue kuna vita unavyo hivyo lazima ujue kuomba maombi ya vita ili Mungu akushindie
Soma ufunuo 12 Yote.( Mungu akufungue macho ya kuomba viziuri tumia Neno ili kufanya maombi kuhusu kuhusu huyo nyoka

Mungu aingilie kati Mikael malaika waingilie kati kupigana na huyo nyoka

Na Mwana Kondoo wa Mungu akushindie.

Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana Kondoo ufunuo 12:11
Tumia damu Ya Yesu kuomba pia

Nielezee vizur hiyo kucheza mpira imekuwaje?


Sijui umepata kitu hapo.
Palipo pungua Roho Mtakatifu akuongezee zaid
Kama anamsingi wa Neno japo kidogo tu ni rahisi kukuelewa, maana unafafanua vizuri sana sitegemei kusikia kuna mtu hayaelewi maelezo ya majibu yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dada divine naomba uiangalie hii na nitakuja PM pia.

Nimeota mara nyingin nakimbizwa na n'gombe mweusi mkubwa sana ana pembe Kali mno.
Mara nyingi nimekuwa nikimkimbia sana sana na pia siku moja aligeuka na kuwa kijana wa kiume simfahamu akaanza kunirushia mishale mikali mingi sana lakini haukunipata hata mmoja yani. Alirusha mara nyingi sana approximately mara 20 kisha akaja bibi mmoja rafiki yake na bibi yangu akasimama akamuangalia akaacha kurusha mishale akapotea .(mazingira ni kwetu kijijini)

Mara nyingine nimeota ng'ombe hiyo akitaka kuniingilia ( mazingira hapa sijajui)

Baada ya kuota mara nyingi juzi nimemuota huyo ng'ombe mweusi amekuja akiwa anajipanga kuanza kunikimbiza nikachukua fimbo ya ufagio nikampiga hadi akatoka kichwa minofu inadondoka chini.



Ndoto nyingine naota nakimbizwa na nyoka
Mszingira siyafahamu kabisa

Kuna siku mtoto wangu alikuwa amekaa ghafla nikaona nyoka mdogo kaja nikamkata yule nyoka!
Tena nikaona nyoka mwingine amekomaa hadi ana manyoya anapita pale pale nikataka kumzuru kwani mwanangu yuko pale ila akapita, wkt name gang as nikaona nyoka mwingine amejibanza pembeni nikamuangalia tu..


Vipi kuota marehemu mzazi kbs anaumwa sana yupo hoi alafu usafiri wa kumfikisha hospitali ni changamoto?

Mara marehemu anelala nyumbani anaumwa
Mara nyingine naota MTU ambae bado hajafa namuota amekufa

Kuna siku nimeota kuwa binti yangu amekufa kwa kuangushwa chini na dada wa kazi na nilipomuuliza akawa kiburi tu kujibu ndio hataki.


Naota nakula minyama mimi na binti yangu..


Naomba unitafsirie kwa uwezo ulionao. Najua nipo vitani na nine shanks finish a YESU awe bwana wa jeshi langu.



Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani vita ipo wazi hapo mpendwa, hata ukirejea moja ya jibu kuhusu ng'ombe unaona wazi ni mizimu na pia wachawi wanakutafuta. Uzuri neema Ya Mungu imekufunika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama anamsingi wa Neno japo kidogo tu ni rahisi kukuelewa, maana unafafanua vizuri sana sitegemei kusikia kuna mtu hayaelewi maelezo ya majibu yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Ijapokuwa ni Imani tofauti na Mkuu DIVINE lakini namwelewa vizuri sana.

Kwani muda mwingi huwa napenda kuunganisha dot za vitabu vya dini mbalimbali.
 
Dada divine naomba uiangalie hii na nitakuja PM pia.

Nimeota mara nyingin nakimbizwa na n'gombe mweusi mkubwa sana ana pembe Kali mno.
Mara nyingi nimekuwa nikimkimbia sana sana na pia siku moja aligeuka na kuwa kijana wa kiume simfahamu akaanza kunirushia mishale mikali mingi sana lakini haukunipata hata mmoja yani. Alirusha mara nyingi sana approximately mara 20 kisha akaja bibi mmoja rafiki yake na bibi yangu akasimama akamuangalia akaacha kurusha mishale akapotea .(mazingira ni kwetu kijijini)

Mara nyingine nimeota ng'ombe hiyo akitaka kuniingilia ( mazingira hapa sijajui)

Baada ya kuota mara nyingi juzi nimemuota huyo ng'ombe mweusi amekuja akiwa anajipanga kuanza kunikimbiza nikachukua fimbo ya ufagio nikampiga hadi akatoka kichwa minofu inadondoka chini.



Ndoto nyingine naota nakimbizwa na nyoka
Mszingira siyafahamu kabisa

Kuna siku mtoto wangu alikuwa amekaa ghafla nikaona nyoka mdogo kaja nikamkata yule nyoka!
Tena nikaona nyoka mwingine amekomaa hadi ana manyoya anapita pale pale nikataka kumzuru kwani mwanangu yuko pale ila akapita, wkt name gang as nikaona nyoka mwingine amejibanza pembeni nikamuangalia tu..


Vipi kuota marehemu mzazi kbs anaumwa sana yupo hoi alafu usafiri wa kumfikisha hospitali ni changamoto?

Mara marehemu anelala nyumbani anaumwa
Mara nyingine naota MTU ambae bado hajafa namuota amekufa

Kuna siku nimeota kuwa binti yangu amekufa kwa kuangushwa chini na dada wa kazi na nilipomuuliza akawa kiburi tu kujibu ndio hataki.


Naota nakula minyama mimi na binti yangu..


Naomba unitafsirie kwa uwezo ulionao. Najua nipo vitani na nine shanks finish a YESU awe bwana wa jeshi langu.



Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba nianze na hiyo kula chakula

Chakula kinaweza kuwa sadaka, au maagano unaingizwa katk maagano ya kichawi au unalishwa nyama za kichawi katika ndoto

Ndoto ni hali halisi katika ulimwengu wa roho

HeSabu 25:1
Basi Israel akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake, wa Moabu

2 kwakuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao, watu wakala, wakaisujudu hiyo miungu yao.

3 Ikawa Israel kujiunganisha na Baal-peori, unaona hapo juu

Nataka uone tu chakula kilivyo waunganisha na Israel na miungu wa wamoabu

Chakula kiliwaunganisha

Hivyo hicho chakula ni agano unaingizwa na hao wachawi au inaweza ikawa ni maagano ya kwenu

Hiyo inaweza kukufanya hata nguvu ya kuomba ukakosa ikaisha kabisa, wanamaliza kiu yako ya kumtafuta Mungu sababu wameunganisha katika maagano ya kichawi
Inaweza ikawa wanakulisha chakula na kukuingizia ugonjwa wengine hata hamu ya kula wanakosa kabisa

Anza na toba kwaajil yako famlia au chochote kilicho mpa uhalal kukupata ktk ndoto, omba toba kwa agano lolote ulilo ingizwa kwa kujua au kutokujua

Omba toba katika sehemu yeyote inayo mzuia Mungu kutokusikia maombi yako tumia damu ya Yesu

Tumia damu Ya Yesu kuimimina katika mwili wako ili kuvunja agano ulilo ingizwa

Ebrania 10:9
.....aondoe la kwanza ili kusudi asimamishe lile la pili( la kwanza ni agano la kale la pili ni jipya)

Hivyo sema navunja agano sawa sawa na ebrania 10:9
Nafuta hilo agano

Natengua viapo vyote kwa damu ya Yesu, nabatilisha pia.kwa damu ya Yesu

Kolosai 1:13
Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake

Toa jina lako katika list ya kichawi au ktk nguvu za giza lipatanishe katika madhabahu ya Mungu patanisha katika nafsi ya Mungu kwa Kristo Yesu

2corintho5:18
Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo,

Ukiwa unajitoa mtoe na mwanao ppia

Funga huo mlango wa ndoto kwa damu ya pasaka ili shetan asipate nafasi ya kupita tena

Tangaza kuwa nipo huru kwa Jina la Yesu isaya 61:1

Huyo mdada wa kazi bado unaye? Uliye muota ktk ndoto?

Kuhusu kuota walio kufa
Hakuna ushirika ktk ya walio hai na wafu mtu akifa kafa hawez kukurudia
Hiyo ni mizimu inabeba sura za marehemu kata huo muunganiko kwa damu ya Yesu

Toba ni muhimu, tafuta somo la malango nilielezea jins ya kuomba toba,

Sijaandika vyote, Mungu anisaidie nitaandika vzr tena
 
Habari zenu wanajamii, naimani mko salama,
Mwenzenu ninaota aina moja ya ndoto tokea 2009, haipiti siku tatu sijaota nasafiri au nagombania usafiri au nahangaika stand ya mabasi. Tafadhali mwenye uelewa anifafanulie ndoto hii tafadhali,. Naamini kuna watu humu wanauelewa na wanaweza saidia kutafakari.
Natanguliza shukrani.
Ndoto ya kuota unapanda basi, gari ni ishara ya kuwa na muungano na Mungu au kufanikisha jambo fulani lakini maelezo ya Divine post ya 2 yanajitosheleza vizuri. Endelea kuomba Mungu na uwe mwaminifu lipo jambo la kutengeneza maishani mwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safari ni hatua ya kwenda mahali fulani.
Muombe Mungu akuongoze

Kutoka13:20
Nao wakasafiri kutoka Sukothi, wakapiga kambi Ethamu, kwenye mpka wa ile jangwa

21 Bwana naye akawatangulia mchana nndani ya wingu mfano wa nguzo, ili kuwapa nuru, wapate kusafiri mchana na usiku,

22 ile nguzo ya wingu haikuondoka mchana, wala ile nguzo ya moto haikuondoka usiku, mbele ya hao watu

## unaona hapo juu hao wana wa Israel walikua na safari
Lakin aliye kuwa anawaongoza Mungu mwenyewe kupitia hizo nguzo mbili

Sasa ukiwa unaomba mwambie Mungu kama alivyo waongoza safar hao wana wa Israel na ww akuongoze

Akupitishe ktk njia ambayo aliyo kuandalia

Ukisoma vizuri hiyo kutoka 14 yote
Utakuta farao aliwafuatia hao wana wa Yakobo

Lakin Mungu aliwafanya wamezwe na maji

Mwambie Mungu nipitapo ktk hii safari wamezwe hao wanaotaka kunikwamisha

Waaibishwe wale wasio taka niifikie kanan yangu

Omba sababu Mungu anatumia Neno kukuvusha
Wakat unaomba kuwa na Imani na Mungu sababu hakuna cha kumshinda

Na kama kuna mtu yeyote aliye pamoja nami ktk safar ambaye ananifanya nisifike.
Mungu shughulika nao kama ulivyo shughulika na Farao na jeshi lake


## sababu naona hapo kuna watu wanajaribu kukurudisha nyuma

Na omba Mungu awe dereva ktk hilo gari ili ufike ktk destination iliyo pangwa

Mungu akiwa dereva huwez ishia njian
Amina mtumishi wa bwana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi huwa naota nipo shule nafanya mtihani au nipo nawahi mtihani nakimbia sana au nipo nasoma katika mazingira magum katika hofu ya kufeli mtihani hyo ndoto huwa inajirudia toka 2014 na mim shule nilsha maliza muda mrefu sana
Ndoto ya kuota mambo yaliyopita ilhali ulishavuka stage hiyo ni ishara kwako kuwa mambo ufanyayo sasa yamepitwa na wakati yamezoeleka update yaani hama kimtazamo ili uweze kufanikiwa.
Unaweza ukaota hata unavuka daraja ni maaana hiyo hiyo pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Divine, Mimi niliota nimeitwa Usiku nikiwa nimelala, kwenda kupokea wageni. Nilipoenda nje (gizani ktk ndoto) nikaelekezwa mahali ambapo kulikuwa na ngazi ndefu kuanzia chini duniani hadi mbinguni. Ilikuwa nzuri sana ya mg'ao wa dhahabu na Mwanga mzuri uliimulika ngazi ile tokea mbinguni. Nikasimama pale chini ya hiyo ngazi, na tazama nikaona watu wanapanda na kushuka kwenye ile ngazi! Nikafurahi sana huku nikiendelea kusubiria wageni wangu wafike. Kwa mbali kidogo nikaona ngazi nyingine kama hiyo lakini kwenye hiyo sikuona watu wakipanda na kushuka. Wakati nashangaa hiyo ngazi nyingine, nikaskia sauti ikinisemesha, ndipo nikageuka kuangalia nikaona mtu aliyevalia vizuri mavazi ya dhahabu akinitazama. Alipoona nimemuona akaendelea na safari kupanda juu akiwa amebeba kitu kama kikapu.

Mara wakafika wageni wangu kutoka juu kwenye ile ngazi (mbinguni), walikuwa wawili. Tukasalimiana kisha kwa kujua Mimi ndiyo mwenyeji nikataka niwaongoze lakini wao wakanishika mikononi mwao (mmoja kushoto, na mqingine kulia) wakanambia " haya twende". Tukaondoka pale kwenye hiyo nuru(kwenye ile ngazi) na kuelekea gizani maana ilikuwa Usiku.

Sijaelewa ni kitu gani hasa kimo ndani ya ndoto ile ingawa Nina amani sana na kila niikumbuka nasikia furaha sana ndani mwangu.
Yakobo ndiye aliyeota ndoto mithili ya hiyo na ninakushauri uongeze zaidi bidii ktk uaminifu wako Mungu anataka kukutumia. Yajue yaliyo mapenzi ya Mungu uyatende.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari mkuu.


Waweza nisaidia ndoto hizi mkuu ambazo hujirudia kila mara.
1.Kucheza mpira na rafiki zako wa utotoni.
2.Kuwa darasani unasoma shule ya msingi
3.Kuua nyoka mweusi
4.Kuliona jina lako juu na kila mtu analishangaa
5.Kuwa mwanajeshi unayefunza watu mafunza jeshin au shuleni wakati mwingine unaongoza watu vitani.
6.Kuyaona maneno Mene Mene na Tekeri angani (hii ilitokea mara moja)
7.Kuwaona watu wawili ambao nafsi yako inaamini ni DAUD na YUSUFU wa katika biblia
8.Kusafiri kwa kupaa angani uku unafurahi
9.Kuwaona samaki au ng'ombe kila mara.





HIZI NDIO NDOTO AMBAZO KILA MARA NAOTESHWA ZINA MAANA GANI.
Kuua nyoka mweusi =ishara ya kuwa umemshinda adui yako mshrikina, hongera.
Kuona jina lako limeandikwa then kila mtu anashangaa=matendo yako yote Mungu kayanukuu na jina lako limeandikwa ktk kitabu kile.
Kuona unasoma darasani =Mungu anataka ujishushe kwake na ujifunze kwake.
Kuona unacheza mpira =pambana kwa kila hali ubadili njia zao hizo sasa zimezoeleka yaani uwe updated.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari mkuu.


Waweza nisaidia ndoto hizi mkuu ambazo hujirudia kila mara.
1.Kucheza mpira na rafiki zako wa utotoni.
2.Kuwa darasani unasoma shule ya msingi
3.Kuua nyoka mweusi
4.Kuliona jina lako juu na kila mtu analishangaa
5.Kuwa mwanajeshi unayefunza watu mafunza jeshin au shuleni wakati mwingine unaongoza watu vitani.
6.Kuyaona maneno Mene Mene na Tekeri angani (hii ilitokea mara moja)
7.Kuwaona watu wawili ambao nafsi yako inaamini ni DAUD na YUSUFU wa katika biblia
8.Kusafiri kwa kupaa angani uku unafurahi
9.Kuwaona samaki au ng'ombe kila mara.





HIZI NDIO NDOTO AMBAZO KILA MARA NAOTESHWA ZINA MAANA GANI.
6,7,8 na 9 Mungu anahitaji kukutumia kama alivyowatumia mitume wake wote ili ukawe mwalimu uwafundishe wengine waelewe wapate kuwa wafuasi wa Mungu waondokane na hila za kidunia (mabaka ya kijeshi ni hila same applied na mabaka ya chatu).
Unahimizwa hima kufanya hayo bila kuchelewa kwani muda ni mchache na unaenda kasi (hizo mene mene tekel)

Ni ndoto ya kinabii ktk ulimwengu wa ufalme wa Mungu majibu na maelezo zaidi soma vitabu vya Daniel, zakaria, ufunuo japo ni vigumu kueleweka ila kiroho vitakufungua na kukufunua.
Mungu akubariki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari mkuu.


Waweza nisaidia ndoto hizi mkuu ambazo hujirudia kila mara.
1.Kucheza mpira na rafiki zako wa utotoni.
2.Kuwa darasani unasoma shule ya msingi
3.Kuua nyoka mweusi
4.Kuliona jina lako juu na kila mtu analishangaa
5.Kuwa mwanajeshi unayefunza watu mafunza jeshin au shuleni wakati mwingine unaongoza watu vitani.
6.Kuyaona maneno Mene Mene na Tekeri angani (hii ilitokea mara moja)
7.Kuwaona watu wawili ambao nafsi yako inaamini ni DAUD na YUSUFU wa katika biblia
8.Kusafiri kwa kupaa angani uku unafurahi
9.Kuwaona samaki au ng'ombe kila mara.





HIZI NDIO NDOTO AMBAZO KILA MARA NAOTESHWA ZINA MAANA GANI.
Kusafiri huku ukipaa ni ishara ya ulinzi wa malaika dhidi ya maisha yako kwa achawi.
Kuwaona samaki na ukawaona ngombe Mungu anataka uwabadilishe watu wenye roho za kutoelewa waswagwao kama ngombe wawe samaki kisha uwavue wawe wafuasi wa Mungu (rejea maelezo ya yesu kwa petro kuanzia sasa hutakuwa mvuvi wa samaki bali utakuwa mvuvi wa watu).
Ninatafsiri nusu nusu kwa kuwa yako mengi uliyoandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ya samaki na ngombe ni ishara ya kuwa yeye atakuwa mwalimu atafundisha watu yaani habari njema kuwabadilisha kutoka ktk imani za miungu hao ngombe na kuiamini injili ya Mungu na atawafanya wafuasi wa Mungu yaani atawavua kama samaki, rejea Yesu na petro. Ubarikiwe mtumishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom