Naombeni msaada wa tafsiri ya ndoto hizi, na zote nliziota mfululizo ndani wiki 1:-
1. Nliota rafiki wa mdogo wangu wa kiume ananitaka kimapenzi nikamkatalia, kaanza kunikimbiza ndotoni akiwa kashika kisu ili anichome, ile anataka kunichoma tu nkashtuka usingizini kwa kupiga yowe hapohapo nkaanza kukemea.
2.Nliota natembea mazingira nisiyoyafahamu kabsa, ghafla akatokea kijana wa kiume akawa anataka kunibaka, na sehemu hyo tulikuwa wawili tu.Nkatumia nguvu kupigana nae, mwisho wa siku nlifanikiwa kumvunja shingo yake na mikono yangu ilitapakaa damu, baada ya hilo tukio nkakimbia kutafuta maji niweze kujisafisha mikono, Nlibahatika kusafisha mikono na kuondoka,, Sikuweza msimulia mtu hilo tukio hadi pale nlipokuja kukamatwa kuwa nimeua, na mlalamikaji akiwa ni mpenzi wa niliyemuua ndotoni, nikaitwa mahakamani kusomewa shtaka, hyo siku ya kusikiliza kesi kulikuwa na watu nlokuwa nawafahamu waliokuja kusikiliza kesi,, ila wote walionekana kuwa upande wa mleta shtaka na kati ya hao wote ni mmoja tu ndiye aliyekuwa upande wangu.
Nikahukumiwa kunyongwa, nlilia sana ndotoni, na yule aliye kuwa upande wangu nae alilia sana.. Ghafla nikajikuta nmeshikilia biblia nsijue imetoka wapi,,, nliikumbatia hadi pale nliposhtuka ndotoni, kuangalia muda ilikuwa saa 9 kasoro usku,, ndo nliponyenyuka na kuchukua biblia nkaishia kuikumbatia hadi asubuhi (Sikupata tena usingizi).