Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Naombeni muandike ndoto humu kwenye post sababu kuna watu wengi wanafahamu ndoto na wanaweza kuwajibu ila upembue ndoto unavyo ambiwa nini maana yake,

Haina maana kujua maana ya ndoto kama hujui kuombea hiyo ndoto itakuwa bure

Wote mkija PM nitashindwa wajibu sababu na utakuta ndoto zingine zinafanana majibu yakitolewa humu atleast utapata mwanga

Na sijui kila kitu nafahamu kidogo sana

Kama unaona ndoto huelewi kabisa na inajirudia tu

Kaa mahal pa utulivu omba
Achilia damu ya Yesu ipite humo katika kila eneo ya ndoto yako tamka tu napeleka damu ya Yesu ipite kwenye ndoto

Ipangue vyote ambavyo sio vya ki Mungu, naachilia malaika wa vita wapite

Kila kipengele ulicho kiota peleka damu ya Yesu
Mfano nimeota simba ananikimbiza,
Tuna simba wa Yuda mwambie Yesu pita kama Simba wa Yuda pigana na simba huyu wa kipepo, namwaga damu ya Yesu ipigane naye.ipite kama mito, ipite kama bahari ya damu ya Yesu

Au nimeona samaki sijui baharini

Mwambie Roho Mtakatifu sijui.maana yake lakini wewe wajua nabadilisha hayo maji yawe damu ya Yesu ya baharini kama hao samaki sio wa Mungu damu ya Yesu itajua huko

Au nimeota nakimbizwa, mwambie Mungu mimi sijui.ni nini hiki lakin wewe Roho Mtakatifu wajua,

Watu wote wanao nifanya mawindo watakuwa mawindo wao,
Yeremia 30:16
Basi,watu wote wakulao wataliwa, na adui zako wote watakwenda kufungwa, kila mmoja wao, na hao waliokuteka nyara watatekwa,

na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo

[emoji115] [emoji115] hiyo ni Yeremia 30:16

Unakimbizwa achilia malaika wawakimbize wao, wanakuwinda Mungu kasema watawindwa wao,

Mungu katika isaya 55:11-

Neno lake halitomrudia bure bali litatimiza mapenzi yake ...... na litafanikisha mambo yote alilo lituma hilo neno lake

Hivyo simama na neno

[HASHTAG]#andika[/HASHTAG] hiyo ndoto ili hata wakati unaomba pitia kipengele kimoja kimoja peleka damu ya Yesu

Au umeota mtu kafa, futa kwa damu ya Yesu sawa sawa na

isaya 7:7 Bwana MUNGU asema hivi neno hili halitakuwa wala halitasimama
[emoji115] [emoji115]

Hivyo kama ndoto ni mbaya futa kwa damu ya Yesu
Sababu damu ya Yesu inanena mema kuliko ile ya Habili

Hivyo tamka neno la uzima kwa damu ya Yesu na litatimia.

Kama umeota umeng'atwa na chochote awe nge nyoka

Anza na toba vile vile anza kuachilia damu ya Yesu katika hilo eneo damu ya Yesu ikaondoe mapando yote

Neno linasema kila pando asilo lipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa mathayi 15:13

Hivyo tamka nang'oa pando lolote lililo wekwa humu kwangu nang'oa kwa Damu ya Yesu na kwa jina la Yesu

Na kama ni nyoka au nge kakung'ata

Kwa uchache

[emoji115] [emoji115] sema pepo nge toka kwa jina la Yesu, au pepo nyoka toka kwa jina la Yesu

Kemea kwa kumaanisha sio kilegevu sababu hiyo ni vita

Kama uking'atwa kuna madhara

Damu ya Yesu ina ponya achilia damu ya Yesu katika hilo eneo ikakuponye ikaondoe jeraha zote.

Kama kuna alama imebaki ambayo itampa shetani uhalal wa kukurudia tena mimina damu ya Yesu ikayeyushe hiyo alama katika mwili wangu kwa damu ya Yesu

Utamke kuwa nipo huru sasa

In ua Presence Jesus is where I belong
 
Kusafiri huku ukipaa ni ishara ya ulinzi wa malaika dhidi ya maisha yako kwa achawi.
Kuwaona samaki na ukawaona ngombe Mungu anataka uwabadilishe watu wenye roho za kutoelewa waswagwao kama ngombe wawe samaki kisha uwavue wawe wafuasi wa Mungu (rejea maelezo ya yesu kwa petro kuanzia sasa hutakuwa mvuvi wa samaki bali utakuwa mvuvi wa watu).
Ninatafsiri nusu nusu kwa kuwa yako mengi uliyoandika.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nakuelewa neno kwa neno
 
Naomba tafsir ya ndoto hizi
1:,Mara kwa Mara naota naokota pesa
2;Mara kwa Mara naota nimerudi kusoma madarasa ya chini
Aliye na ujuzi anitafsrie ctaki masihara
 
Naomba tafsir ya ndoto hizi
1:,Mara kwa Mara naota naokota pesa
2;Mara kwa Mara naota nimerudi kusoma madarasa ya chini
Aliye na ujuzi anitafsrie ctaki masihara
Una haraka sana ili uweze kupata mafanikio. Kikwazo kikuu cha kutokufanikiwa ni kuendelea kutumia mbinu za kizamani ktk maisha yako (kusoma madarasa ya chini wakati unatakiwa uwe juu).
Unahitaji kuapdate mipango yako ili uweze kufanikiwa(kuokota pesa).
 
halo wakuu nimetoa kuna mtu kani jerui jeraha kubwa sana kichwani kiasi kwamba ninasubiri tu kufa sasa nikashituka wakatai nina daí bima yangu ya maisha ili Jamii yangu iweze fidiwa . ukweli nilipo shituka nilijikuta na maumivu makali sana kichwani nikasali sana nini maana yake
 
Ni ishara ya kupata majaribu yatakayopelekea kutumia muda mwingi kuyawaza, yatapelekea kuathiri afya yako (kuota unajeruhiwa kichwa).
Muombe Mungu hashindwi yeremia 32:27)
 
halo wakuu nimetoa kuna mtu kani jerui jeraha kubwa sana kichwani kiasi kwamba ninasubiri tu kufa sasa nikashituka wakatai nina daí bima yangu ya maisha ili Jamii yangu iweze fidiwa . ukweli nilipo shituka nilijikuta na maumivu makali sana kichwani nikasali sana nini maana yake
Ni umeumia kweli katika ulimwengu wa roho, omba toba ina maana hadi unapigwa huyo mtu either ana uhalali wa kukupiga au kakuonea, hivyo anza toba vzr ukimaliza peleka damu ya Yesu iachilie uponyaji katika kichwa chako kwa kupigwa kwako Yesu sisi tumepona, na kiri mstari kuwa sitokufa bali nitaishi nami nitayasimulia matendo makuu ya Bwana, hakikisha unaomba vzr sio dkk 10 umamaliza. Nimeandika kifupi tu hapa
 
Pesa ni uchumi wako, hivyo angalia hizo pesa ni za aina gani? Coin or not, uchumi unaweza ukawa umefungwa hapo ila angalia mazingira ya ndoto yalivyo ielezee vzr
Mwanzo nilikua naokota noti, ila cku hizi naokota coin tu
 
Ni umeumia kweli katika ulimwengu wa roho, omba toba ina maana hadi unapigwa huyo mtu either ana uhalali wa kukupiga au kakuonea, hivyo anza toba vzr ukimaliza peleka damu ya Yesu iachilie uponyaji katika kichwa chako kwa kupigwa kwako Yesu sisi tumepona, na kiri mstari kuwa sitokufa bali nitaishi nami nitayasimulia matendo makuu ya Bwana, hakikisha unaomba vzr sio dkk 10 umamaliza. Nimeandika kifupi tu hapa
naomba ni saidie kwa kirefu ni muda nina matatizo sana nimekua nasali ila siwezi kusali zaidi ya dakika 15

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
naomba ni saidie kwa kirefu ni muda nina matatizo sana nimekua nasali ila siwezi kusali zaidi ya dakika 15

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Yesu nitie nguvu,

Rudi juu kabisa, kuna mahali nimeelekeza kwa ujumla omba toba kwa urefu rudia tu maneno kwa kumaanisha huku ukiwa na vifungu vya Bible, baadaye ndio ung'oe hilo pando la ugonjwa ndani yako, na ukiri uzima ndani yako kinywa kina nguvu
 
niliota nipo na watoto Wangu juu ya kilima tumejishikilia padogo sana halafu kuna bonde linabubujika maji meupe sana kwenye ukuta wa marumaru nzuri,pia Leo nimeota simba mkubwa anatoka darini ananifukuza mm na wanangu .naomba msaada wa tafsiri
 
Shetani anakuwinda wewe na wanao simama imara katika maombi na neno la Mungu ili uvunje na kuharibu hiyo mipango ya shetani
 
Back
Top Bottom