Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Sawa nasubiriaa
 
Je ukiota unaongea na mtu ambaye alishakufa ina maana gani labda anakuonya usifanye hichi na hichi hua ina maana gani manake mm nmewah ota nazungumza na baba alishafariki mm nkawa namwogopa namwambia ww si ulishakufa lakini akawa anasema usiogope we karibu huku ndo nyumban kwangu ati ananiambia hivyo alafu palikua na uwanja mkubwa tu ila nkawa naona kamba ndefu ya kupanda unaenda juu nikawa najisemea kimya kimya apa akigeuka tu nakimbilia kamba nimtoroke nlishituka dahh jasho kila mahali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani kwa kifupi tu hapo wewe umuombe Mungu akufanikishe safari yako. Ukichunguza maisha yako katika yale uliyopanga kutimiza na hii ndoto vina uhusiano. Ni wazi una ndoto za kufika sehemu katika maisha japo huenda Mungu anataka kukufikisha mahali ambapo hata uwezo wa akili yako haujafikiria bado. Pia wapinzani ni wengi unaowajua na usiowajua. Mwangalie Mungu zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi huwa naota nipo shule nafanya mtihani au nipo nawahi mtihani nakimbia sana au nipo nasoma katika mazingira magum katika hofu ya kufeli mtihani hyo ndoto huwa inajirudia toka 2014 na mim shule nilsha maliza muda mrefu sana
Kwa mtazamo wako unaona kama umemaliza shule lakini kiukweli bado hujamaliza! Wakati mwingine ukitaka kuhakikisha hili angalia baada ya kumaliza elimu yako umeajiriwa? Na je? Hiyo ajira inakulipa sawa na kiwango cha elimu yako? Pia usisahau mitihani mbalimbali ya maisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Divine mimi nataka niku follow sijui namna ya kufanya, maana nimepima maelezo ya majibu yako nimeona wewe siyo msanii ni mtumishi Wa Mungu kweli, ni mtu wa imani kweli siyo mbabaishaji. Napenda kujifunza zaidi kupitia watu wa aina kama yako. Thanks

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama anamsingi wa Neno japo kidogo tu ni rahisi kukuelewa, maana unafafanua vizuri sana sitegemei kusikia kuna mtu hayaelewi maelezo ya majibu yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani vita ipo wazi hapo mpendwa, hata ukirejea moja ya jibu kuhusu ng'ombe unaona wazi ni mizimu na pia wachawi wanakutafuta. Uzuri neema Ya Mungu imekufunika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama anamsingi wa Neno japo kidogo tu ni rahisi kukuelewa, maana unafafanua vizuri sana sitegemei kusikia kuna mtu hayaelewi maelezo ya majibu yako

Sent using Jamii Forums mobile app
Ijapokuwa ni Imani tofauti na Mkuu DIVINE lakini namwelewa vizuri sana.

Kwani muda mwingi huwa napenda kuunganisha dot za vitabu vya dini mbalimbali.
 
Naomba nianze na hiyo kula chakula

Chakula kinaweza kuwa sadaka, au maagano unaingizwa katk maagano ya kichawi au unalishwa nyama za kichawi katika ndoto

Ndoto ni hali halisi katika ulimwengu wa roho

HeSabu 25:1
Basi Israel akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake, wa Moabu

2 kwakuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao, watu wakala, wakaisujudu hiyo miungu yao.

3 Ikawa Israel kujiunganisha na Baal-peori, unaona hapo juu

Nataka uone tu chakula kilivyo waunganisha na Israel na miungu wa wamoabu

Chakula kiliwaunganisha

Hivyo hicho chakula ni agano unaingizwa na hao wachawi au inaweza ikawa ni maagano ya kwenu

Hiyo inaweza kukufanya hata nguvu ya kuomba ukakosa ikaisha kabisa, wanamaliza kiu yako ya kumtafuta Mungu sababu wameunganisha katika maagano ya kichawi
Inaweza ikawa wanakulisha chakula na kukuingizia ugonjwa wengine hata hamu ya kula wanakosa kabisa

Anza na toba kwaajil yako famlia au chochote kilicho mpa uhalal kukupata ktk ndoto, omba toba kwa agano lolote ulilo ingizwa kwa kujua au kutokujua

Omba toba katika sehemu yeyote inayo mzuia Mungu kutokusikia maombi yako tumia damu ya Yesu

Tumia damu Ya Yesu kuimimina katika mwili wako ili kuvunja agano ulilo ingizwa

Ebrania 10:9
.....aondoe la kwanza ili kusudi asimamishe lile la pili( la kwanza ni agano la kale la pili ni jipya)

Hivyo sema navunja agano sawa sawa na ebrania 10:9
Nafuta hilo agano

Natengua viapo vyote kwa damu ya Yesu, nabatilisha pia.kwa damu ya Yesu

Kolosai 1:13
Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa mwana wa pendo lake

Toa jina lako katika list ya kichawi au ktk nguvu za giza lipatanishe katika madhabahu ya Mungu patanisha katika nafsi ya Mungu kwa Kristo Yesu

2corintho5:18
Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo,

Ukiwa unajitoa mtoe na mwanao ppia

Funga huo mlango wa ndoto kwa damu ya pasaka ili shetan asipate nafasi ya kupita tena

Tangaza kuwa nipo huru kwa Jina la Yesu isaya 61:1

Huyo mdada wa kazi bado unaye? Uliye muota ktk ndoto?

Kuhusu kuota walio kufa
Hakuna ushirika ktk ya walio hai na wafu mtu akifa kafa hawez kukurudia
Hiyo ni mizimu inabeba sura za marehemu kata huo muunganiko kwa damu ya Yesu

Toba ni muhimu, tafuta somo la malango nilielezea jins ya kuomba toba,

Sijaandika vyote, Mungu anisaidie nitaandika vzr tena
 
Ndoto ya kuota unapanda basi, gari ni ishara ya kuwa na muungano na Mungu au kufanikisha jambo fulani lakini maelezo ya Divine post ya 2 yanajitosheleza vizuri. Endelea kuomba Mungu na uwe mwaminifu lipo jambo la kutengeneza maishani mwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amina mtumishi wa bwana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi huwa naota nipo shule nafanya mtihani au nipo nawahi mtihani nakimbia sana au nipo nasoma katika mazingira magum katika hofu ya kufeli mtihani hyo ndoto huwa inajirudia toka 2014 na mim shule nilsha maliza muda mrefu sana
Ndoto ya kuota mambo yaliyopita ilhali ulishavuka stage hiyo ni ishara kwako kuwa mambo ufanyayo sasa yamepitwa na wakati yamezoeleka update yaani hama kimtazamo ili uweze kufanikiwa.
Unaweza ukaota hata unavuka daraja ni maaana hiyo hiyo pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yakobo ndiye aliyeota ndoto mithili ya hiyo na ninakushauri uongeze zaidi bidii ktk uaminifu wako Mungu anataka kukutumia. Yajue yaliyo mapenzi ya Mungu uyatende.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuua nyoka mweusi =ishara ya kuwa umemshinda adui yako mshrikina, hongera.
Kuona jina lako limeandikwa then kila mtu anashangaa=matendo yako yote Mungu kayanukuu na jina lako limeandikwa ktk kitabu kile.
Kuona unasoma darasani =Mungu anataka ujishushe kwake na ujifunze kwake.
Kuona unacheza mpira =pambana kwa kila hali ubadili njia zao hizo sasa zimezoeleka yaani uwe updated.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
6,7,8 na 9 Mungu anahitaji kukutumia kama alivyowatumia mitume wake wote ili ukawe mwalimu uwafundishe wengine waelewe wapate kuwa wafuasi wa Mungu waondokane na hila za kidunia (mabaka ya kijeshi ni hila same applied na mabaka ya chatu).
Unahimizwa hima kufanya hayo bila kuchelewa kwani muda ni mchache na unaenda kasi (hizo mene mene tekel)

Ni ndoto ya kinabii ktk ulimwengu wa ufalme wa Mungu majibu na maelezo zaidi soma vitabu vya Daniel, zakaria, ufunuo japo ni vigumu kueleweka ila kiroho vitakufungua na kukufunua.
Mungu akubariki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusafiri huku ukipaa ni ishara ya ulinzi wa malaika dhidi ya maisha yako kwa achawi.
Kuwaona samaki na ukawaona ngombe Mungu anataka uwabadilishe watu wenye roho za kutoelewa waswagwao kama ngombe wawe samaki kisha uwavue wawe wafuasi wa Mungu (rejea maelezo ya yesu kwa petro kuanzia sasa hutakuwa mvuvi wa samaki bali utakuwa mvuvi wa watu).
Ninatafsiri nusu nusu kwa kuwa yako mengi uliyoandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ya samaki na ngombe ni ishara ya kuwa yeye atakuwa mwalimu atafundisha watu yaani habari njema kuwabadilisha kutoka ktk imani za miungu hao ngombe na kuiamini injili ya Mungu na atawafanya wafuasi wa Mungu yaani atawavua kama samaki, rejea Yesu na petro. Ubarikiwe mtumishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…