Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Pia kipindi cha umri kati ya miaka 17-18 kuna ndoto ambazo kusema kweli ninewahi kuziota zaidi ya mara 1
I. Kuangukia katika shimo refu ambalo siwezi kuona mwisho wake
II. Nakimbia ama kuendesha baiskeli na kujikuta nashtuka ghafla
III. Ndoto mbaya zinazoambatana na vitisho vikali vya madude ambayo sijawahi kuyaona zikiambatana na hisia kana kwamba napiga kelele lakini sauti haitoki ama hakuna anayezisikia kuja kunisaidia
IV.Kuota naokota maburungutu ya fedha lakini naambulia hasira za matongotongo pindi napoamka [emoji116][emoji116][emoji116]

Hizi zote ni ndoto zinazohusiana na makuzi lakini vile vile ni ndoto mshindo nyuma kutokana na harakati za siku nzima
Hizi ndoto za kuanguka kwenye shimo refu mara nyingi imethibitishwa ni denda linalotoka mdomoni ukilala mdomo wazi na ukiwa na uchovu mwingi
Ndoto za kutisha na majitu ya ajabu mara nyingi hutokana na akili ya mtoto mwenyewe kutengeneza mawazoni mwake hizi fikra mchana kutwa hivyo usiku huleta mshindo nyuma
Akili ya utotoni huwa very pure ikiwa bado haijawa contaminated na hizi changamoto za kila siku hivyo kuipa akili muda wa kutosha kufikiri vitu vya ziada
Jr[emoji769]
 
Mr Mshana
Vp kuusu msosi wa Ugali na kutoandaa usafi wa mandhar ya kulalia? Haiusishi complex dreams?
 
Nimekupata kaka
 
Mkuu naomba tafsiri ya hii ndoto,niliota mfululizo"nilalapo ninaota nikiwa nina-paa au kuelea angani kwa kutumia mikono yangu kama mabawa na ninaenda umbali mrefu tu,lakini wakati huwo nikiwa angani naelekea bondeni,na hali ya ndoto ninakuwa nafuraha na nchi au maeneo ninayopita yana kijani kibichi ila ndoto inaishia nikiwa angani sielewi ninaposhukia na nikiamka naona kama kupaa nikitu nakiweza kawaida kama ilivyo kwenye ndoto.
Natanguliza shukrani.
 
Juzi niliota nimeenda kijijini kwetu ile naingia kwenye eneo letu/ chimbuko la baba nikakuta miti yote imekatwa ikawa kama sehemu inayochomwa mkaa na pale wanaishi baba zangu wadogo nikakuta kuna maaskari wa tz na Kenya wamekuja kwa ishu hiyo ya kukatwa miti, baba zangu wadogo wamekua wapoleee.


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Ardhi ni mama dunia, maji ni uhai.. Kuna kitu kinajaribu kukutenga na hivyo viwili... Jichunge

Jr[emoji769]
Haiwezi kuwa na maana hiyo... Nadhani Taifa langu linaingia kwenye matatizo makubwa... Nasema hivi kwasababu nilishawahi ota ndoto za namna hii na taifa likaingia kwenye majonzi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok kwahiyo wewe sio sehemu ya hilo taifa?

Jr[emoji769]
usiku wa kabla kile kivuko kuzama... Niliota hii ndoto... "Watu wapo uwanjani, uwanja wa michezo mkubwa.. wakilia sana, huku mmoja kati ya watu walipokuwa pale uwanjani akasimama kuongea na watu...

Alionekana kuwa ni kiongozi... Mbele kulikuwa na jeneza... Watu walikuwa wakilia sana... Nikastuka kutoka usingizini hapo ilikuwa ni saa 10 kasorobo usiku..." Asubuhi zinakuja habari za kuzama kwa kivuko...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulimwengu wa roho ni mpana sana na ndoto zina tafsiri nyingi lakini misingi haitofautiani
Jr[emoji769]
 
Ndoto zingine bana, sijawahi kucheza hata mechi za mtaa kwa mtaa ila jana nimeota nimefunga bonge moja la goli tena kwenye mkeka kama wa OT kabisa...nimerudi kucheki video y goli lenyewe sasa πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ yani dinyo mwenyewe akasome πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…