Habari ya uzima kwa wote, Mungu ni mwema atujaliae uzima,mwenye nguvu na mamlaka ni yeye.
Niende kwa maada yenyewe
Maada.
Mimi ni kijana ambae natarajia kuoa hivi karibuni kama Mungu akinipa kibali cha kufanya hivyo, wapendwa mimi kuna maombi ambayo nilikuwa nikiifanya kwa Mungu wangu kwa ajili ya kupata mke mwema maana mi nipo nasali ni mlokole,, sasa cha kushangaza siku moja nilikuja kuota ndoto nikiwa nimekaa ndani tupo mezani na mabinti wawili,mmoja tunasali nae mwingine anasali Aic, tupo tumekaa watatu tumekaa nawengine walikuwepo pembeni yetu lakini wao sikuwatambua kisura,, tukiwa katika kukaa pale tulianza kuzungumzia maswala ya kuoana na yule binti anaye sali Aic tulielewana kuwa tutaoana kila mtu akatoka pale anaamani moyoni kuwa baadae tukutana kwa mipango zaidi ya ndoa,basi tukawa tumeondoka na ndoto akaaishia pale.
Kilichofuata baada ya siku chache.
Kuna binti alikuja kama mgeni kanisani alitokea pande za Ukerewe hapo sasa tayari ile ndoto naota yule binti mgeni alikuwa tayari alisha kuja kanisani kwetu kama week hivi, huyu binti anahuduma ya kuimba nami pia vilevile, chakushangaza nilishaangaa namba ngeni imetuma "mambo",baadae nikaifuatilia akaanza kama kunikwepa mara mi dada yako mara nini,,
kwakufupisha
Baadae nilihisi tu huyu atakuwa furani na kweli alikuwa yeye na wakati huo namba yangu sikuwahi kumpa labda alichukua kwa wapendwa, alijitambulisha nami pia waoooh kumbe ni wewe basi tuliendelea hivo kama marafiki mara aniite kaka, basi mwisho wa siku ananitamkia ananipenda anataka siku moja niwe mmewe naye mke wangu,, mi nikamwambia ombi lako limekubaliwa.
Ntaendelea kujibu tokana na comment zenu, mwisho nimalizie
Nipo njia panda je ile ndoto niyoota ya binti yule wa Aic na hiki kilicho tokea mbele yangu nini nini, maana bashindwa kung'amua wapi nisimamie je, ndoto inamlenga yule binti au huyu wa kanisani?.Halafu kingine wote siwajui tabia zao kiundani labda huyu wa kanisani ndo nishaanza kumsoma.
Isije ikawa ni shetani kaingia kati kuharibu maombi yangu, nahitaji msaa wa kiroho kwa wataalamu wa ndoto,, Mungu ni mwema atawatia nguvu kwa msaada zaidi.
Mungu awabariki.
Bin Shaib Official 2021