Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Asanteh sana kaka
Hali yako ya kiuchumi ikoje? Baiskeli inasimama kuonesha mtu mwenye uchumi mdogo na gari katika ndoto yako linasimama kuonesha mtu mwenye uchumi mkubwa...
Mkuu umelenga mule mule.. lakni mm ni mwanafunzi sina harakati nyingi saana zaid ya kupiga kitabu chuoni
 
Tafsiri yake ni hii, yapo matatizo makubwa ya kishirikina mbele yako na yatakuzidi nguvu hivyo fuata njia ya ufumbuzi kulingana na imani yako.
 
Na Mimi niliota ninaendesha Rolls Royce nilikutana uso kwa uso na muendesha baiskeli... daaaaah ghafla nilishtuka
 
Hali yako ya kiuchumi ikoje? Baiskeli inasimama kuonesha mtu mwenye uchumi mdogo na gari katika ndoto yako linasimama kuonesha mtu mwenye uchumi mkubwa.

Ulivyoota unataka kuovertake gari ni kuwa,kwa akiri ya kawaida ni ngumu mtu mwenye baiskeli kuovertake gari,hivyo maana ya ndoto yako ni hii:-

Katika Maisha yako unajaribu kupambana sana ili kujikwamua na hali uliyokuwa nayo katika Maisha yako,na kuna wakati unatumia nguvu nyingi sana katika kujikwamua na juhudu nyingine zinakuwa ni za hatari ambazo zinaweza kupoteza au kuhatarisha Maisha yako,


Hivyo nakusihi sana ndugu Yangu kuwa makini katika harakati zako za kujipatia riziki kwani kuna muda zaweza kukutia katika hatari (kifo)

Kwa kuongeza ni kuwa mtu hapaswi kupuuza ndoto,huwa zina ujumbe mzito sana ukizifuatilia,na kunakipindi inafikia kile ulichoota lazima kitimie
Huyuu atakuaa anajitutumua kuutaka urais 2025
 
Usiku wa kuamkia leo nimeota ndoto ambayo siyo nzuri sana na imenitisha sana.

Nimeota nimekufa niko ndani ya jeneza kwenda kuzikwa na watu wanalia sana. Ghafla nikashtuka toka usingizini. Nikajaribu kuinua kichwa kikawa kizito baada ya muda kichwa kikaniuma sana.

Naomba unipe tafsiri ya hii ndoto maana imeninyima raha kabisa.

Nawasilisha.
Hiyo ndoto inaweza kufasiliwa hivi; ipo roho ya mauti inayokufuatilia kwako, hiyo ni taaarifa kwako kwamba kuna mambo yako kiroho yanataka kuzikwa, chukka tahadhari zikae hizo roho kwa kuomba na Mungu atakusaidia
 
Mimi niko kwenye hali mbaya sana kiuchumi kwa sasa.

Usiku wa kuamkia leo nimeota kuna pesa nilikuwa naziiba sehemu na kuzifungia kwenye begi langu..kisha begi nikaenda kulificha kuchaka mbali kidogo na nyumbabi.Ghafla yalikuja mafuriko kama ya Tsunami,maji kutoka baharini yakaanza kuingia mitaani.Mimi nilikimbia hadi kwenye kile kichaka nilichoficha begi langu nililohifadhi pesa za wizi,kisha nikalichukua na kuanza kukimbilia sehemu ya juu ambapo maji hayawezi kufika.Kwenye ndoto nakumbuka nilikuwa na ndugu na marafiki wengine siwafahamu kabisa ila tulianza kuyakimbia yale maji yaliyotoka baharini.Bahati nzuri mimi nilikuwa naongoza njia na tulifanikiwa kufikia sehemu ambapo maji hayawezi kutufikia.Nilipolifungua lile begi langu nilizikuta pesa zipo salama na safarii hii nilishangaa kukuta noti za elfu kumi nyingi sana na dolla za kimarekani,nikiwa ndotoni nikajisemea hizi dolla nitaenda kuzichenji....Nikashtuka!

Mwenye upeo wa kuweza kunisaidia tafsiri ya ndoto yangu japokuwa si mwandishi mzuri au msimuliaji mzuri.

Natanguliza shukrani!

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Je ukiota unamuoa mwanamke usiyemjua ndotoni..na kabla zoezi halijakamilika ukakimbia hilo zoezi..Inaashiria nini hii kitu?
 
Habari ya uzima kwa wote, Mungu ni mwema atujaliae uzima,mwenye nguvu na mamlaka ni yeye.

Niende kwa maada yenyewe

Maada.
Mimi ni kijana ambae natarajia kuoa hivi karibuni kama Mungu akinipa kibali cha kufanya hivyo, wapendwa mimi kuna maombi ambayo nilikuwa nikiifanya kwa Mungu wangu kwa ajili ya kupata mke mwema maana mi nipo nasali ni mlokole,, sasa cha kushangaza siku moja nilikuja kuota ndoto nikiwa nimekaa ndani tupo mezani na mabinti wawili,mmoja tunasali nae mwingine anasali Aic, tupo tumekaa watatu tumekaa nawengine walikuwepo pembeni yetu lakini wao sikuwatambua kisura,, tukiwa katika kukaa pale tulianza kuzungumzia maswala ya kuoana na yule binti anaye sali Aic tulielewana kuwa tutaoana kila mtu akatoka pale anaamani moyoni kuwa baadae tukutana kwa mipango zaidi ya ndoa,basi tukawa tumeondoka na ndoto akaaishia pale.

Kilichofuata baada ya siku chache.
Kuna binti alikuja kama mgeni kanisani alitokea pande za Ukerewe hapo sasa tayari ile ndoto naota yule binti mgeni alikuwa tayari alisha kuja kanisani kwetu kama week hivi, huyu binti anahuduma ya kuimba nami pia vilevile, chakushangaza nilishaangaa namba ngeni imetuma "mambo",baadae nikaifuatilia akaanza kama kunikwepa mara mi dada yako mara nini,,

kwakufupisha
Baadae nilihisi tu huyu atakuwa furani na kweli alikuwa yeye na wakati huo namba yangu sikuwahi kumpa labda alichukua kwa wapendwa, alijitambulisha nami pia waoooh kumbe ni wewe basi tuliendelea hivo kama marafiki mara aniite kaka, basi mwisho wa siku ananitamkia ananipenda anataka siku moja niwe mmewe naye mke wangu,, mi nikamwambia ombi lako limekubaliwa.

Ntaendelea kujibu tokana na comment zenu, mwisho nimalizie

Nipo njia panda je ile ndoto niyoota ya binti yule wa Aic na hiki kilicho tokea mbele yangu nini nini, maana bashindwa kung'amua wapi nisimamie je, ndoto inamlenga yule binti au huyu wa kanisani?.Halafu kingine wote siwajui tabia zao kiundani labda huyu wa kanisani ndo nishaanza kumsoma.

Isije ikawa ni shetani kaingia kati kuharibu maombi yangu, nahitaji msaa wa kiroho kwa wataalamu wa ndoto,, Mungu ni mwema atawatia nguvu kwa msaada zaidi.

Mungu awabariki.

Bin Shaib Official 2021
 
Aisee, kumbe ukiingia kwenye maombi mke anapatikana kirahisi hivi.

Labda kuna mtu ulimsimulia hiyo ndoto yako hapo kanisani ndio maana yanajitokeza hayo. Au kwa kuwa hisia zako ni kutaka mke wa kuoa ndio maana binti unaempenda ndio anajitokeza ili kuhalalisha ulichokiota.

Kwa kuwa kwenye matukio ya ndoto umeota ukiwa na binti toka Kanisa lingine, tafsiri yake utakayemuoa ni mtu mgeni na hapo unaposali. Nakushauri umuoe tu huyo aliyejitokeza, maana Mungu tayari amejibu maombi yako.
 
"Mpendwa" unafurahisha sana...sasa si uote tena ili ujue mbivu na mbichi?
 
Back
Top Bottom