Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Naota sana kuhusu watoto mapacha. ..Juzi niliota tena. .Pacha mmoja amezaliwa very weak tukamweka kwenye beseni lenye maji ili ashtuke. Na huyo pacha weak ana alama nyeusi mguu wa kushoto (birthmark ).
Maana yake nini?
 
Ukiota umemfumania mkeo halafu una mfukuza kwa hasira, lakini yeye wala hashtuki wa kuomba msamaha akawa anaondoka tu, ina maana gani?!
 
Umeshaota jiandae kukabiliana na hicho kitakapo tokea hakuna jinsi ya kukwepa. Iwe kufa dhiki raha jiandae ndoto ukiota hakuna jinsi ya kukwepa kama ni ya ukweli. Lkn kuna mengine mauzauza au homa nk
 
Ukiota umemfumania mkeo halafu una mfukuza kwa hasira, lakini yeye wala hashtuki wa kuomba msamaha akawa anaondoka tu, ina maana gani?!
kuna ndugu au rafiki yako atakutendea jambo baya, atakukwaza sana ila pasipo yeye kujua na hatofahamu kama amekuudhi(hatojali)
 
Naota sana kuhusu watoto mapacha. Juzi niliota tena. Pacha mmoja amezaliwa very weak tukamweka kwenye beseni lenye maji ili ashtuke. Na huyo pacha weak ana alama nyeusi mguu wa kushoto (birthmark ).

Maana yake nini?
Naendelea kuitazama, nitakupatia maana yake soon, kuna eneo limenizuia kuiona.
 
ndoto hiyo ni onyo! ujue kuwa kifo kipo! sasa umefanya nini yanayo mpendeza Mungu? assume kwamba ulikufa sasa umepewa second chance ya kumtafuta Mungu! zingatia! na inamuhusu kila mmoja wetu humu ndani! sio kumfafanulia mwenzio na wakati hata wengine tunahusika! iyo ni onyo kwako na kwawengine wote kuwa! Mungu anatukumbusha kuwa kifo kipo na kama tutakufa hatutaludi duniani tena! sasa chance hii ya mara moja tunaitumiaje katika kumtafuta Mungu??? unajua unaweza ukatafuta utajiri,elimu, ndoa! lakini mwisho wa siku sisi kama binadamu sio wakwanza kupitia hivi! kwaiyo havina maana kama hatuta mfuate Mungu na kuitambua damu ya Yesu kristo iliyo mwagika pale msalabani!
 
NENDA KAPIME MALARIA.
 
Nina ndoto mbili ya kwanza nimeota naendesha Rolls Royce nyeupe na nimevaa suti nyeupe, nyingine nimeota mtu amenipa rupia hela za kizamani akaniambia nenda kachenji utapata hela, halafu huyo mtu alivyonipa akawa kama ana haraka fulani hivi alinipa huku anaondoka. Je, hii ina maana gani nayo?
 
Msese,nami nasikia saana hiyo,jamaa ana maisha marefu sana,ukiota sherehe ni mbaya sana hiyo ndoto,
 
Mie nataka tu uniambie je mtu akiota ndoto na ikajirudia mara kwamara kwa siku tofauti zaidi ya mara ishirini inamaanisha nini?
Ndoto ikijirudia mara kwa mara hiyo ndoto usiipuzie ina maana Mungu anaongea na wewe kwa njia ya ndoto bt note kuwa sio ndoto zote ni za Mungu. Ukiota mara nyingi ndoto ujue kuna kitu so kuwa makin kama ni kuomba omba kwa Mungu akuambie nn maana yake.
 
Mimi huwa naota napigana either na rafiki yangu au na mtu mwingine ambaye simfaham pia sometimes huwa naota nakimbizwa na kundi la watu wenye siraha nawakimbia najificha hawanion then naamka au huwa naota tunakimbia tupo wengi mno halafu wanajeshi wanatukimbiza na silaha then mimi najifichaga kwny jumba bovu wanapita wanatafuta hanioni au nakimbilia kwenye nyumba nafunga mlango tena ndoto ya hivi huwa yanijia mara kwa mara.
 
Na mimi naomba unitafsirie ndoto yangu. Ndoto iko hivi, naota naruka juu angani kisha natua then naruka tena huku nikifurai sana.
 
Mi nimeota nilikuwa na shamba kubwa la mpunga then gafla likaungua moto, tena moto wa kasi kama wa petroli huku mpunga ukiwa umefikia kuvunwa. Nini maana ya ndoto hii?
 
hahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahah aisee binadamu tupo wawili wawili nakumbuka hata mimi nlishawahi ota hicho kitu kama ilikua kwenye kisiwa hibi jeshi lilivamia niliwaona hadi marafiki zangu wamekamatwa mateka ila mimi nilifanikiwa kujificha kwenye jumba bovu huku nawashuhudia rafiki zangu wakiwa wametekwa. Hii ndoto ina maana mungu anakutetea katika ubaya watu waliopanga kukufanyia ila zidisha maombi ndugu maana kuna watu wanataka kukuangamiza hasa wachawi.
 
Habari ukiota adui yako yupo na mke wako tena chumbani kwako ulipofika ukampiga yule adui sana mwisho yule adui yako akasema nimetumwa na baba ila naenda. Hapo ina maana gani?
Duh! Hiyo kali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…