Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Mi niliota eti kuna sehemu nilikuta shilingi mia mia nyingi nikaanza kuokota hadi nikajaza mfuko, yaani nikitembea kidogo naona sh. Mia naiokota. Hii ndoto ina maana gani?
ndugu yangu. utapatwa na wakati mgumu sana kiuchumi, ukiona unaokota sarafu(sio noti), ni ishara kuwa utapitia kipindi kigumu kiuchumi, na mambo yako mengi hayatoenda
 
Mie mke wangu aliota anasex na jamaa mwingine yaan mpaka wakapasua vyombo ndani afu et nikawafumania kwenye ndoto.japo huyo mtu aliyekuwa anasex naesimjui. Sasa je ina maana gani?
haina maana kuwa mke wako anachepuka, ila kuna hali ya kutoelewana itatokea baina yako na mtu wako wa karibu kama kazini, jirani au ndugu,
 
Mkuu mke wangu yupo Chuo amepanga chumba. Majuzi kaota ametoka Chuo ile anafungua kitasa akaona ghafla mlango unafunguliwa na mwanaume hamjui alikuwa ndani, ghafla mwanaume yule akapotea. Ila pia mara nyingi huota anaoga na mwanaume asiyemfahamu
ni dalili mojawapo ya roho wachafu, majini wanataka kumwingia na kushiriki nae, pia mahusiano yenu yataanza kuyumba, hasa yeye mwenzio ataanza matatizo na kuleta hali ya kutoelewana.
 
kuna dhana mbili hapo, ila kwa kuwa hujafafanua nashindwa kukueleza kwa kina,
1. eneo unaloishi kuna sehemu inafanyika kutaniko la kichawi, ktk vikao vyao.
2. kuna kundi la wachawi wanaendesha mkakati wa kukudhuru, ila inawapa wakati mgumu kufanikiwa,

karibu tena mama.



Dah nimepata shock kwakweli, nashkuru sana kwa ufafanuzi.. Sasa nifanye nn exactly maana hizi ndoto sizipendi kbsa
jaribu kutafuta suluhisho kwa mambo hayo mawili niliyokueleza
 
Saafi...
Mara nyingi sana naota napaa kama ndege muda ungine nakua nakimbizwa nikianza kukimbizwa tu napaa au hata muda ungine bila kukimbizwa najikuta napaa kama nimeota mbawa hii ina maana gani wandugu...
Hizi ni ndoto ambazo hutokea pale roho yako inapokuwa ktk hali ya hatari, kuna roho mbaya ya wachawi huwa wanataka kukudhuru na huwa inafanikiwa kukimbia na kukuacha salama.
 
Mara nyingi hua naota nipo karibu na watu mashughuri kama vile mastar wa music wa hapa na nje na mastar wa football. Maana yake iko vipi.?
 
Habari kwa anae ota sana mala kakutana na simba wengi na hawamfanyi usumbufu wowote ndoto hii huwa inajirudiarudia ktk siku tofauti maana yake n nn
 
Ndoto ikijirudia mara kwa mara hiyo ndoto usiipuzie ina maana Mungu anaongea na ww kwa njia ya ndoto bt note kuwa sio ndoto zote ni za Mungu. Ukiota mara nyingi ndoto ujue kuna kitu so kuwa makin kama ni kuomba omba kwa Mungu akuambie nn maana yake
Asante sana! nitafanyia kazi ushauri wako.
 
kutafsiri ndoto ni elimu pana sana ndugu, sio kama unavyodhani. Kuna mawili hapo. Kuna ndoto unazoota kwa kurejea kumbukumbu za mchana, huweza kujirudi kutegemeana na shughuli na fikra za mambo ya mchana.

Kama ndoto sio ya mrejesho wa shughuli za mchana, basi ni ya kiroho, hapo sasa lazma ujue ndoto uliotaje, kuna sababu nyingi sana ya kujirudia ndoto kutegemea na kile mtu alichoota.

Karibu sana rofejo ndugu yangu
Asante sana , sasa wewe unawezaje kutafsiri ndoto unafanyajefanyaje?
 
Habarini wakuu,

kwa siku za karibuni nimeona thread nyingi humu watu wakiwa na kiu ya kutaka kujua maana ya ndoto mbalimbali, lakini imekuwa ngumu kwao.

Wengi wamekimbilia kutisha wakiamini kuwa ndoto zote zina uhusiano wa uchawi, mashetani na ulozi, jambo ambalo si kweli.


Leo nataka nitoe somo la bure hapa. Ila kwa kuwa ndoto ziko nyingi nami nimeona kila mwenye uhitaji aniulize nami nitamjibu ktk thread hii hii.

Asanteni na karibuni sana.
MIMI NIMEOTA NAKIMBIZWA NA VIUMBE VYA AJABU,MBELE YANGU NIKAONA NYUMBA NA MLANGONI AMESIMAMA KAKA YANGU AMBAYE NI MAREHEMU AKAWA ANANIITA NIKAINGIA NDANI AKAFUNGA MLANGO VILE VIUMBE VIKANIKOSA.MAANA YAKE NN?
 
ni kundi la wachawi walikuja kukudhuru ila walikushindwa, na hakuwa mwanamke, ni mwanaume, ktk ndoto za namna hvyo huwa unaona opposite, natumai umenielewa, karibu
MKUU MIMI NILIOTA MTI MKUUUBWA SANA MKUBWA MNO.JUU KABISA PANAPOTENGANISHA SHINA NA MAJANI KUNA SHIMO.YUPO NYOKA MKUBWA SANA AMEJIVIRINGA KUZUNGUKA KINGO ZA SHIMO,KALALA KWA UTULIVU MKUBWA.KWA JUU YAKE KIDOGO KUNA NDEGE JAMII YA NJIWA AU KUNGURU.CHINI YA MTI KUNA MTO WA MSIMU YAANI ILE IJAAYO MAJI KWA NYAKATI.ILI KUUKATIZA MTO KULIKUWA NA KINJIA KINAUKATIZA MTO,AKAWA ANAPITA MWANAJESHI KUUVUKA MTO.LILE JOKA NI KUBWA MNO LILIPOMWONA KWA SPIDI KALI SANA LIKATEREMKA MTINI KWA KASI SANA KUMWELEKEA MWANAJESHI.NA MWISHOWE LIKAMDHURU NA NAHISI LILIMUUA.HIYO NI NDOTO YANGU KARIBU MKUU
 
Khabari zenu wakuu,

Hii mada ya ndoto ni nzuri kwa kweli na waotaji ni wengi na tukiwa hatujui nini maana ya ndoto hizo, na mimi nitaungana kwa wanatakajua maana manake huwa naota sana pia ila hukosa kujua maana ya ndoto hizo.

Mimi nimeota hivi tukiwa tumekwenda picknic mimi pamoja na familia ya mke wangu, tumefika sehemu ambayo tumeamua kukaa sehemu ya majabali makubwa. Sisi vijana tukaamua kupanda sehemu ya juu ya jabali lakini mama wa mke wangu yeye tuliamua kumueka sehemu iko tambarare kidogo, si kama tujuavyo jabali mara nyingi haliko tambarare liko umbile lisokaa sawa, kwa kweli mama wa mke wangu yeye ni mgonjwa wa miguu sasa tuliamua kuweka hapo sehemu tambarare ya jabali ambayo hakua sehemu ya juu kama tulivyo sisi vijana tumepanda juu sana.

Sisi tukiwa juu ya jabali tunatizama upoange wa chini kidogo ya jabali ambalo yuko mama wa mke wangu, wakati tunatizama chini namuona mke wangu akimkumbatia mama ake yaani kama mama na mwana kujifariji vile wakati huo yule mama wa mke wake wangu akiwa kaa kwenye kitu cha kulala, mke wangu katika kumkumbatia inabidi amuinamie mama ake pake kwenye kiti cha kulala sasa na kile kiti kiko upembeni mwa jabali, kutokana na uzito ulo ambao mke wangu anamkumbatia mama ake kiti kikaanza kusota pembeni mwa jabali yule bibi akaporomoka kuelekea upande wa pili wa jabali sisi kwa vile tuko juu na tunaona tukio lote lile, kuwa yule mama wa mke wangu ameanguka na kile kiti kuenda upande wa pili wa jabali.

Mimi na shemegi yangu, ambae ni ndugu na mke wangu, tukateremka kwa kasi ya ajabu kumfata mama wa mke wangu kule chini, katika kuenda mwendo wa kasi kuyaruka majabali tukienda chini shemeg yangu alikua na kasi zaidi na kafika mwanzo chini kule, mara yule mama wa mke wangu tuwa tumemtia kwenye machera kama mtu asokua na fahamu muda ule, ghafla yule shemeg yangu akatoweka nikajiona mm peke yangu namburura mama wa mke wangu pamoja na watoto wadogo wanainsaidia kuburura, baada ya hapo nikashtuka .
hapa sijui maana ya ndoto hii kwa kweli...
 
Hilo sio tatizo ndugu, wengi hudhani ni ulozi. Kumbuka roho huwa haina limit ya muda, umbali nk, kuna wakati huwa roho inazunguka ktk maeneo mengine ila bila kuacha mwili, hivyo unajiona unapaa, kuruka nk.
...mi naota sana hizi ndoto za kupaa,hasa nikizingirwa na maadui na kukosa upenyo wa kusevu huwa napaa zangu juu kabisa!
...dah,ganja kweli tiba!
 
Mimi kuna ndoto huwa naiota,sijui maana yake,yaani nikiijiwa tu na wachawi ndotoni huwa nachukuaga fimbo mfano wa bua la mtama,hilo bua nikilishika tu linaninyanyua juuu na kuanza kupambana na wachawi hao,nikizidiwa nguvu,bua linaanza kufukuzana kwa kasi kubwa mpaka wachawi wanachoka,likiwadi nguvu linawafukuza mbaya,siku moja lilinibeba na kumfukuza bibi mmoja hadi akateguka miguu akawa anatembelea magoti mpaka alipotoka eneo la ajali akapotea,nini tafsiri yake hii ndoto wadau,na inanirudia sana,na huwa napendezwa saana nikiiota hii ndoto maana ni starehe kweli ukiwa unaiota
 
Msaada mimi naota naokota Pesa nyingi na ndoto hii inajiludia sana karibu mara mbili hadi tatu kwa wiki na nizaidi ya miaka tano sasa msaada tafadhari.
 
Back
Top Bottom