Ninavyoambiwa kwa kabila langu, ndoto ya kifo ni kuwa umeshiba sana, nyoka ni maisha marefu, harusi ni msiba hivyo usiwe na wasi wasi ila hayo mambo ya ibada sijui.
Watu wanapenda kumtumia Mungu kutisha wenzao wakati hakuna aliyeishasikia wala kumwona Mungu. Natamani hawa watu wamwone simba au chui tuone kama watabaki kuomba kwa jina la------ ili akimbie au asiwale.
Mbona wanakemea vitu wasivyoviona tu. Huyo Pepo ana sura gani???? Mbwa mwenye kichaa atokeze hakuna mchungaji atakayepiga goti kuomba wote ndukiiii. Check umekula nini au ulikuwa katika maono gani kabla ya kwenda kulala. Try to say your prayers lakini siyo zile za kujitangaza. Mungu yupo rohoni mwako sirini. Maji ya baraka kama wewe Mkatoliki ni kinga sana kama unaamini siyo lazima.