Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Juzi nimeota niko dukani nanunuliwa viatu ila mara ya kwanza muuza duka aliniletea viatu vidogo namba 5 havikunitosha, akaleta namba 7 vikawa vikubwa wakati ameenda kunitafutia namba 6 nikawa nimeondoka yale maeneo.

Jana nikaota nimepewa viatu vizuri sana kama zawadi lakini ni vikubwa. ... Nini maana ya hizi ndoto. ?

Pia nimeota naendesha gari dogo automatic, ila kila nilipokuwa naweka D ili niondoke gari likawa linarudi nyuma kwa kasi. ...Nikajitahidi kulisimamisha likawa linaendelea kurudi mpaka nilipokuwa fence, nikagota hapo....Then nilipoanza kuendesha tena likakubali kwenda mbele bila shida. ..Naomba tafsiri Mkuu. ..
 
Ukiota mala kwa mala unawaona simba madume wengi wako mbuga za wanyam hawakuzuru maana yake ni nini mcheza karate
 
Nina mtindo as kuota watu nilioanza nao Maisha na wengine walionitangulia wananifanyia madudu! wengine tunakwaruzana kibiashara mpaka nikaamua kujitenga! Lakini kuwaota hakuishi! msaada nn kifanyike!

Na wanaotufanyia mambo ya ajabu always hawatoki mbali mkuu!

Umejitenga nao kimwili sio kiroho ndo maana bado unawaota manaake bado kuna link kiroho!

Ss omba toba kwanza coz ndo itifaki ya kwenda mbele za Mungu, then vunja na jitenge na maagano yyt ambayo umewahi kuingia nao,kwa kujua au kutojua yamkini walikuingiza bila ww kujua!
Teketeza kabisa madudu yao na kinachowaunganisha,then achilia ulinzi wa bness/mali zako kwa Damu ya Yesu!
#sorry km sio christian,hapa mwisho nisije kuwa nimekukwaza#

Hutawaona tena
 
mimi naota nashindana na mtu/watu au kitu
ila kikiwa na mashambulizi sana
namimi napata nguvu gafla nakiteketeza ,au wakati mwingine najitolea kuangamizwa badala ya wengine mfano labda jini liniangamize mimi badala ya wengine lakini nakua nalikemea sana mpk nashtuka nalishinda..
wakati mwingine naweza kukikimbia kitu kwa kupaa angani...

ndoto zinanirudia mara nyingi
nashindana na vitu ila navishinda mfano: wakati mwingine hata nyoka nashindana nae lakni namshinda..

maana yake nini

Mshukuru Mungu unashinda!
Lkn lzm uendelee kusima neno na maombi ili kuwa na nguvu za Mungu zaidi!

Kujitolea kuangamia kwa ajili ya watu wengine !

Umebeba kitu kwa ajili ya watu , muulize Mungu kusudi/umebeba nn?

Qn, we mzaliwa wa ngapi kwnye familia mkuu?
 
Na wanaotufanyia mambo ya ajabu always hawatoki mbali mkuu!

Umejitenga nao kimwili sio kiroho ndo maana bado unawaota manaake bado kuna link kiroho!

Ss omba toba kwanza coz ndo itifaki ya kwenda mbele za Mungu, then vunja na jitenge na maagano yyt ambayo umewahi kuingia nao,kwa kujua au kutojua yamkini walikuingiza bila ww kujua!
Teketeza kabisa madudu yao na kinachowaunganisha,then achilia ulinzi wa bness/mali zako kwa Damu ya Yesu!
#sorry km sio christian,hapa mwisho nisije kuwa nimekukwaza#

Hutawaona tena
Uko sawa
 
Mshukuru Mungu unashinda!
Lkn lzm uendelee kusima neno na maombi ili kuwa na nguvu za Mungu zaidi!

Kujitolea kuangamia kwa ajili ya watu wengine !

Umebeba kitu kwa ajili ya watu , muulize Mungu kusudi/umebeba nn?

Qn, we mzaliwa wa ngapi kwnye familia mkuu?
wa mwisho
tuko watatu mimi na kaka zangu
ila mama aliwahi kuzaa watoto wa wawili kabla ya sisi watatu
mmoja alikaa miezi 11 akafa
mwingine akamzaa miaka mingine akakaa miezi 9 akafa
sasa sijui mimi ni wa 5 au wa3?? ila ni wa mwisho
 
wa mwisho
tuko watatu mimi na kaka zangu
ila mama aliwahi kuzaa watoto wa wawili kabla ya sisi watatu
mmoja alikaa miezi 11 akafa
mwingine akamzaa miaka mingine akakaa miezi 9 akafa
sasa sijui mimi ni wa 5 au wa3?? ila ni wa mwisho

Ok
Ni wa mwisho tu!

Lkn ww ni lango kiimani!
Umebeba kusudi la kuwasaidia wengine
 
Ok
Ni wa mwisho tu!

Lkn ww ni lango kiimani!
Umebeba kusudi la kuwasaidia wengine
halafu leo usiku pia nmeota
nilikua na wenzangu siwajui ila kama wa4
tukawa tumekaa mahala
kuna mama mmoja alikua na pesa sana yani dizaini kama pedeshee
akaanza kutugawia hela
wenzangu wakapewa hela ,mimi nikaja kuangalia kumbe kile changu sio kibunda cha hela
ila ni dizaini kama kadi za mwaliko wa harusi sijui...
nikakasirika nikaondoka...
ila zile hela dizaini kama zilikuja kuwapa matatizo
sielewi maana yake nini
 
Mkuu juzi kati niliota nimepanda ndege baadae nikaamua niende chooni kukojoa na kujipiga selfie nikiwa chooni aliingia mmama mmoja akiwa na mtoto wake tukasalimiana mtoto wake alivyomaliza kujisaidia wakatoka, mule chooni kuna sehemu moja ilikua juu nyingne chini nikiwa natafta pozi la kujipga selfie ghafla ndege ilitikisika nikateleza kuelekea chini bahati nzuri nikajizuwia na chuma kisha nikainuka nikawa naangaika kurudi juu, nikaamua nipande sehemu niliyo telezea ila kila nikijitahidi nashindwa huku naogopa kwasababu ndege ilikua ina yumba yumba, nikaamua kupanda upande mwingine ila palikua parefu kuliko pa mwanzo nikajikaza nikapanda fasta bila matatizo nikatoka chooni nikarudi kukaa ktk siti yangu.Msaadat tafadhari
 
Nyie mnaoanzisha nyuzi za ndoto mojamoja, hebu wekeni hapa itakua nzuri zaidi
 
NDOTO NNE nimeziota zinanipa kuwaza sana,naomba msaada wa kunitafsria ndoto hizi...(1) katika ndoto ya kwanza niliota niko mahali na akaja mtu nisiyemjua akanipa tawi lenye matunda matatu na majani yake membamba.

Yalikuwa ni matunda yenye rangi ya dhambarau na madogo kama goroli. Nikaambiwa nile yale matunda kisha nile na yale majani.Yalikuwa matamu sana....nikaamka usingizini... Baada ya siku chache tena kupita,ndoto ingine ikaja.

Niliota napanda mlima mrefu sana,kulikuwa na njia imechongwa yenye uwezo kupita mtu mmoja tu,lkn kadri nilivyozidi kupanda ule mlima,ile njia ikaendelea kuwa ndogo zaidi.Na nilipokaribia kufika kileleni ilikuwa tabu sana kupanda nikatumia nguvu zaidi nikapanda juu kileleni,nikiwa pale kileleni ghafla nikaona nipo juu ya dari la nyumba halafu nikasikia sauti ikasema huo pembeni yako ni mtihani wako wa mwisho.

Nikayatazama yale makaratasi lkn ikaonekana kama nimeufanya ule mtihani na nimeongoza kwa watu wote...nikaamka usingizini...Ndoto hii pia haiondoki kichwani mwangu...Baada ya siku chache tena kupita...nikaota nipo safarini nimepanda ndege kubwa sana..ndani ya ndege kulikuwa na ngazi upande huu na upande huu...ilikuwa imepaa juu saaana angani na tulisafiri masaa mengi sana.Ilikuwa juu sana kwa namna ambavyo nyota nilikuwa nazitazama kwa chini...yaani ndege ilikuwa juu zaidi ya nyota ...

Tulipokaribia mwisho wa safari ndege ili ikawa imeteremka usawa wa chini ikijiandaa kutua,mimi na wenzangu wale tukaangalia saa zetu tukaona kwamba tumesafiri masaa tisa angani...

Tulitoka saa kumi na mbili na dakika kumi na mbili asubuhi sasa ni saa tisa na dakika kumi na mbili..sikuona tukitua lkn nikaona tupo tayari ktk ardhi.

Nikaamka usingizini...ndoto hii pia haiondoki kichwani mwangu.
 
Yapata miaka kumi na saba tangu nifiwe na mama yangu mzazi, nilikuwa bado mdogo kama miaka 6, sasa cha ajabu juzi nimeota amefariki na tupo msibani hali yakuwa alishafariki zamani sana!!! Je kwa anaejua hii inakuwa namaana gani?
 
Mama yako atakuwa alikuwa hajafa,atakuwa alichukuliwa kimuugiza!......pole sana mkuu!!
 
Mm naota xn ndoto nikiwa nafanya mapenz na mabint warembo. Je hii inamanisha nn?
 
Back
Top Bottom