Khabari zenu wakuu,
Hii mada ya ndoto ni nzuri kwa kweli na waotaji ni wengi na tukiwa hatujui nini maana ya ndoto hizo, na mimi nitaungana kwa wanatakajua maana manake huwa naota sana pia ila hukosa kujua maana ya ndoto hizo.
Mimi nimeota hivi tukiwa tumekwenda picknic mimi pamoja na familia ya mke wangu, tumefika sehemu ambayo tumeamua kukaa sehemu ya majabali makubwa. Sisi vijana tukaamua kupanda sehemu ya juu ya jabali lakini mama wa mke wangu yeye tuliamua kumueka sehemu iko tambarare kidogo, si kama tujuavyo jabali mara nyingi haliko tambarare liko umbile lisokaa sawa, kwa kweli mama wa mke wangu yeye ni mgonjwa wa miguu sasa tuliamua kuweka hapo sehemu tambarare ya jabali ambayo hakua sehemu ya juu kama tulivyo sisi vijana tumepanda juu sana.
Sisi tukiwa juu ya jabali tunatizama upoange wa chini kidogo ya jabali ambalo yuko mama wa mke wangu, wakati tunatizama chini namuona mke wangu akimkumbatia mama ake yaani kama mama na mwana kujifariji vile wakati huo yule mama wa mke wake wangu akiwa kaa kwenye kitu cha kulala, mke wangu katika kumkumbatia inabidi amuinamie mama ake pake kwenye kiti cha kulala sasa na kile kiti kiko upembeni mwa jabali, kutokana na uzito ulo ambao mke wangu anamkumbatia mama ake kiti kikaanza kusota pembeni mwa jabali yule bibi akaporomoka kuelekea upande wa pili wa jabali sisi kwa vile tuko juu na tunaona tukio lote lile, kuwa yule mama wa mke wangu ameanguka na kile kiti kuenda upande wa pili wa jabali.
Mimi na shemegi yangu, ambae ni ndugu na mke wangu, tukateremka kwa kasi ya ajabu kumfata mama wa mke wangu kule chini, katika kuenda mwendo wa kasi kuyaruka majabali tukienda chini shemeg yangu alikua na kasi zaidi na kafika mwanzo chini kule, mara yule mama wa mke wangu tuwa tumemtia kwenye machera kama mtu asokua na fahamu muda ule, ghafla yule shemeg yangu akatoweka nikajiona mm peke yangu namburura mama wa mke wangu pamoja na watoto wadogo wanainsaidia kuburura, baada ya hapo nikashtuka .
hapa sijui maana ya ndoto hii kwa kweli...