Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

hahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahah aisee binadamu tupo wawili wawili nakumbuka hata mimi nlishawahi ota hicho kitu kama ilikua kwenye kisiwa hibi jeshi lilivamia niliwaona hadi marafiki zangu wamekamatwa mateka ila mimi nilifanikiwa kujificha kwenye jumba bovu huku nawashuhudia rafiki zangu wakiwa wametekwa. hii ndoto ina maana mungu anakutetea katika ubaya watu waliopanga kukufanyia ila zidisha maombi ndugu maana kuna watu wanataka kukuangamiza hasa wachawi
Ndoto zingine bhaana, iyo itakua movi umeangalia sasa unakua unaiota. movi zingine zakutisha mjiepushe kuwa mnaziangalia.
 
Nimeota mtu kaingilia dirishani akanikuta nimelala kifudifudi akanikalia mgongoni na kuniita kwa jina langu akafanya kama anainivunja mabega anayabinua kurudi nyuma, tena kaniita kwa kuanza na WE! nikashtuka na kutetemeka sana, ni nini hiki?!
 
Hii nimeiota leo hii hii,
Nimeota kuna mtu anagonga mlango huku akiita jina langu kwa sauti, tena sauti ya kike akitaka nimfungulie.ghafla nikashituka na sikusikia ile sauti,nikafungua mlango sikuona mtu lakini tangu muda ule sauti yangu imekauka haitoki vizuri,hii ina maana gani?

Omba sn kwa ajili ya ulinzi!
Unafikiri wachawi wanachukuaje watu!hiyo ni styl mojawapo!

Kila ndoto yenye maana huwa inaachilia kitu!.
Ss cha mhimu omba Mungu aondoe kila kilichoachiliwa kupitia hiyo ndoto!
 
Msaada mimi naota naokota Pesa nyingi na ndoto hii inajiludia sana karibu mara mbili hadi tatu kwa wiki na nizaidi ya miaka tano sasa msaada tafadhari.

Hali yako ya kifedha/uchumi ikoje?
Coz mara nyingi ukiota hivyo manaake unapoteza
 
NDOTO

Ndoto ni mlango wa kiroho ndani ya mtu, au unaotumiwa na Mungu kusema na watu!
Ayubu 33:14-18
Daniel 2:45
N.k
~si kila ndoto inatoka kwa Mungu.
~Ndoto inaweza kutumika kupitisha adhabu kutoka kwa Mungu au miungu!
~Ndoto zote za uhakika zina tafsiri yake.

VYANZO VYA NDOTO
1 zinazotoka kwa Mungu
Matendo ya mitume,2:17.

Kwa ajili ya kusema na watu juu ya jambo fulani lijalo,lillilopita au linaloendelea ktk ulimwengu wa roho...
Mf,ulikuwa unaomba juu ya jambo fulani na Mungu anaweza akakujibu kupitia ndoto.

2 Ndoto zinazotoka kwa adui,shetani
kumbukumbu 13:1-4

3 zinazotokana na shughuli nyingi,mawazo,uchovu.nk
Mhubiri 5:3

4 zinazotokana na hali ya kiroho ya mahali ulipolala.
Mwanzo 28:10-17.

#changamoto ni kuwa wengi wetu hatujui kutofautisha ndoto hii ni ujumbe kutoka kwa Mungu au laa!#
Cha mhimu ombea mlango wako wa ndoto usitumiwe na adui,kupitisha vitu vyake hiyo ndo njia rahisi#
 
Khabari zenu wakuu,

Hii mada ya ndoto ni nzuri kwa kweli na waotaji ni wengi na tukiwa hatujui nini maana ya ndoto hizo, na mimi nitaungana kwa wanatakajua maana manake huwa naota sana pia ila hukosa kujua maana ya ndoto hizo.

Mimi nimeota hivi tukiwa tumekwenda picknic mimi pamoja na familia ya mke wangu, tumefika sehemu ambayo tumeamua kukaa sehemu ya majabali makubwa. Sisi vijana tukaamua kupanda sehemu ya juu ya jabali lakini mama wa mke wangu yeye tuliamua kumueka sehemu iko tambarare kidogo, si kama tujuavyo jabali mara nyingi haliko tambarare liko umbile lisokaa sawa, kwa kweli mama wa mke wangu yeye ni mgonjwa wa miguu sasa tuliamua kuweka hapo sehemu tambarare ya jabali ambayo hakua sehemu ya juu kama tulivyo sisi vijana tumepanda juu sana.

Sisi tukiwa juu ya jabali tunatizama upoange wa chini kidogo ya jabali ambalo yuko mama wa mke wangu, wakati tunatizama chini namuona mke wangu akimkumbatia mama ake yaani kama mama na mwana kujifariji vile wakati huo yule mama wa mke wake wangu akiwa kaa kwenye kitu cha kulala, mke wangu katika kumkumbatia inabidi amuinamie mama ake pake kwenye kiti cha kulala sasa na kile kiti kiko upembeni mwa jabali, kutokana na uzito ulo ambao mke wangu anamkumbatia mama ake kiti kikaanza kusota pembeni mwa jabali yule bibi akaporomoka kuelekea upande wa pili wa jabali sisi kwa vile tuko juu na tunaona tukio lote lile, kuwa yule mama wa mke wangu ameanguka na kile kiti kuenda upande wa pili wa jabali.

Mimi na shemegi yangu, ambae ni ndugu na mke wangu, tukateremka kwa kasi ya ajabu kumfata mama wa mke wangu kule chini, katika kuenda mwendo wa kasi kuyaruka majabali tukienda chini shemeg yangu alikua na kasi zaidi na kafika mwanzo chini kule, mara yule mama wa mke wangu tuwa tumemtia kwenye machera kama mtu asokua na fahamu muda ule, ghafla yule shemeg yangu akatoweka nikajiona mm peke yangu namburura mama wa mke wangu pamoja na watoto wadogo wanainsaidia kuburura, baada ya hapo nikashtuka .
hapa sijui maana ya ndoto hii kwa kweli...

Mkuu we na mkeo/familia huwa mnaomba?

Muombe Mungu,mwambie akusemeshe kwa lugha ambayo utaielewa na itajirudia kwa njia rahisi
 
Ingine hii hapa
Naota napanda mlima mrefu kwa shida sana kama nataka kuanguka yaani nipo hatarini kweli kweli nikiangalia chini mbalii mala ghafra naamka huku moyo ukienda mbio sana ...nisaidieni tafsiri yake wandugu..

Kupanda mlima ni jaribu,au kuna jambo gumu unapitia,au linakuja utalipitia! Na ni hatari kweli,so
Omba Mungu akuvushe kwny hilo jambo/jaribu salama.

Na Mungu akikuvusha utaona kabisa utaota umepanda huo mlima mpk juu!
 
Mimi naomba kusaidiwa tafsiri ya ndoto hizi maana zimekuwa zikijirudia nmara kwa mara ndoto moja huwa naota nipo mazingira ya chuo either darasani au hostel nawakati nilishamaliza chuo kitambo tu.
ya pili naota nyumba yaani nimejenga nyumba ila haijaisha kwa ktk ndoto zingine nilikuwa nikipotea wakati naelekea huko site nazunguka kweli mwisho ndio napaona juzi nimeota sasa nimeshahamia kwenye nyumba yangu japo haijaisha vizuri. nini maana ya hizi ndoto.

Mkuu Mungu amekuletea ujumbe mara mbili lkn una maana moja!
.kuota uko darasani,au hujamaliza nyumba, manaake kuna hatua unataka kupiga lkn umekwama mahali!

Mungu anajitahidi kukwambia ,bado hujavuka anakurudisha drsn, au umeona nyumba haijaisha,manaake kuna hatua Mungu anataka akusogeza lkn anaona bado so kazana kuomba!

Lkn bora ww una matumaini, ht ushahamia kwny nyumba japo bado haijaisha vzr!(ktk ndoto)
Kazana Mungu anakuvusha mahali!
#cheki maisha yako ya kawaida wapi umekwama,na ss unaendeleaje#
 
Kupanda mlima ni jaribu,au kuna jambo gumu unapitia,au linakuja utalipitia! Na ni hatari kweli,so
Omba Mungu akuvushe kwny hilo jambo/jaribu salama.

Na Mungu akikuvusha utaona kabisa utaota umepanda huo mlima mpk juu!
Mimi siku kama 8 zimepita nimeota nakimbia tuko wawili na mwingine ni kama wa kike hv ila sikumuelewa,na nyuma yetu kulikua na watu si wengi sana wala wachache sana kama wanatukimbiza na tukawa tunaogopa tunazidi kukimbia,lakini mpaka wakatupata na nikaona tena kama hawana time na sisi tukawa tunakimbia wote,na sikujua tuliishia wapi tena.sijui ni nini kile
 
Habarini wakuu,

kwa siku za karibuni nimeona thread nyingi humu watu wakiwa na kiu ya kutaka kujua maana ya ndoto mbalimbali, lakini imekuwa ngumu kwao.

Wengi wamekimbilia kutisha wakiamini kuwa ndoto zote zina uhusiano wa uchawi, mashetani na ulozi, jambo ambalo si kweli.

Leo nataka nitoe somo la bure hapa. Ila kwa kuwa ndoto ziko nyingi nami nimeona kila mwenye uhitaji aniulize nami nitamjibu ktk thread hii hii.

Asanteni na karibuni sana..
sasa mimi nshapata taarifa tofaut sana lakin hii ndoto huwa inajirudia yaana huwa naota natembea kuelekea maali lakin humo njia kama si lift huwa napanda gar kuelekea nindako kabla ya kufika huwa nakumbana na vutisho mara gari kuaribika baadae ndo nafika lakin kwa taabu sasa hii inamaanisha nn ?
 
Habarini wakuu,

kwa siku za karibuni nimeona thread nyingi humu watu wakiwa na kiu ya kutaka kujua maana ya ndoto mbalimbali, lakini imekuwa ngumu kwao.

Wengi wamekimbilia kutisha wakiamini kuwa ndoto zote zina uhusiano wa uchawi, mashetani na ulozi, jambo ambalo si kweli.

Leo nataka nitoe somo la bure hapa. Ila kwa kuwa ndoto ziko nyingi nami nimeona kila mwenye uhitaji aniulize nami nitamjibu ktk thread hii hii.

Asanteni na karibuni sana..
nambie hyo ndoto inamaanisha nn
 
Nimeota mtu kaingilia dirishani akanikuta nimelala kifudifudi akanikalia mgongoni na kuniita kwa jina langu akafanya kama anainivunja mabega anayabinua kurudi nyuma, tena kaniita kwa kuanza na WE! nikashtuka na kutetemeka sana, ni nini hiki?!
Watu Wa Giza wanataka kukuchukua mateka. Na hiyo ni taarifa kwamba yatatukia ikiwa hautazikemea ipasavyo hila hizo za maadui.
 
Mimi siku kama 8 zimepita nimeota nakimbia tuko wawili na mwingine ni kama wa kike hv ila sikumuelewa,na nyuma yetu kulikua na watu si wengi sana wala wachache sana kama wanatukimbiza na tukawa tunaogopa tunazidi kukimbia,lakini mpaka wakatupata na nikaona tena kama hawana time na sisi tukawa tunakimbia wote,na sikujua tuliishia wapi tena.sijui ni nini kile

Huyo wa kike hukumuelewa?

Japo hujafafanua vzr kwa huyo mwanamke,
Lkn omba kwa ajili ya ulinzi wako!
Kukukuta wakakuacha inawezekana Mungu kakutetea!

Na km ina maana zaidi lzm itajirudia!

Ayubu 33:14-18
 
Nina mtindo as kuota watu nilioanza nao Maisha na wengine walionitangulia wananifanyia madudu! wengine tunakwaruzana kibiashara mpaka nikaamua kujitenga! Lakini kuwaota hakuishi! msaada nn kifanyike!
 
mimi naota nashindana na mtu/watu au kitu
ila kikiwa na mashambulizi sana
namimi napata nguvu gafla nakiteketeza ,au wakati mwingine najitolea kuangamizwa badala ya wengine mfano labda jini liniangamize mimi badala ya wengine lakini nakua nalikemea sana mpk nashtuka nalishinda..
wakati mwingine naweza kukikimbia kitu kwa kupaa angani...

ndoto zinanirudia mara nyingi
nashindana na vitu ila navishinda mfano: wakati mwingine hata nyoka nashindana nae lakni namshinda..

maana yake nini
 
Back
Top Bottom