Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Sisi kwetu ukiota umekufa inamaana siku hiyo ulishiba sana na ukiota harusi ujue kuna msiba unakuja
 
Habarini wakuu,

kwa siku za karibuni nimeona thread nyingi humu watu wakiwa na kiu ya kutaka kujua maana ya ndoto mbalimbali, lakini imekuwa ngumu kwao.

Wengi wamekimbilia kutisha wakiamini kuwa ndoto zote zina uhusiano wa uchawi, mashetani na ulozi, jambo ambalo si kweli.

Leo nataka nitoe somo la bure hapa. Ila kwa kuwa ndoto ziko nyingi nami nimeona kila mwenye uhitaji aniulize nami nitamjibu ktk thread hii hii.

Asanteni na karibuni sana..
 
Mie nataka tu uniambie je mtu akiota ndoto na ikajirudia mara kwamara kwa siku tofauti zaidi ya mara ishirini inamaanisha nini?
 
Mie nataka tu uniambie je mtu akiota ndoto na ikajirudia mara kwamara kwa siku tofauti zaidi ya mara ishirini inamaanisha nini?
Kutafsiri ndoto ni elimu pana sana ndugu, sio kama unavyodhani. Kuna mawili hapo. Kuna ndoto unazoota kwa kurejea kumbukumbu za mchana, huweza kujirudi kutegemeana na shughuli na fikra za mambo ya mchana.

Kama ndoto sio ya mrejesho wa shughuli za mchana, basi ni ya kiroho, hapo sasa lazma ujue ndoto uliotaje, kuna sababu nyingi sana ya kujirudia ndoto kutegemea na kile mtu alichoota.

Karibu sana rofejo ndugu yangu
 
Habari ukiota adui yako yupo na mke wako tena chumbani kwako ulipofika ukampiga yule adui sana mwisho yule adui yako akasema nimetumwa na baba ila naenda. Hapo ina maana gani?
 
Habari ukiota adui yako yupo na mke wako tena chumbani kwako ulipofika ukampiga yule adui sana mwisho yule adui yako akasema nimetumwa na baba ila naenda. Hapo ina maana gani?
Binadamu ktk ulimwengu wa roho kuna wakati roho huwa inaishi na kufanya matukio hata pale unapokuwa umelala.

Inaonyesha roho ilikuwa inapambana na roho mbaya. Ila roho yako ilishinda ktk vita hiyo, na roho mbaya ilitumwa na mshirika wake.

Hii kusema kama majini yalitumwa kwako(mke) ila roho(mwenye mke) yako ilifanikiwa kuyadhibiti na hivyo ikalazimu kujitetea kuwa alitumwa na baba yake(mwanadamu)
 
Habari, naomba kuuliza hivi ukiwa unaota kama unaelea angani au unapaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine hii maana yake nini? Na inasababishwa na nini?
Asante!
 
Habari, naomba kuuliza hivi ukiwa unaota kama unaelea angani au unapaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine hii maana yake nini? Na inasababishwa na nini?
Asante!
Hilo sio tatizo ndugu, wengi hudhani ni ulozi. Kumbuka roho huwa haina limit ya muda, umbali nk, kuna wakati huwa roho inazunguka ktk maeneo mengine ila bila kuacha mwili, hivyo unajiona unapaa, kuruka nk.
 
IYO
Habari, naomba kuuliza hivi ukiwa unaota kama unaelea angani au unapaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine hii maana yake nini? Na inasababishwa na nini?
Asante!
IYO
NDOTO INA MAANISHA UENDA UKAPATA SAFARI YA MBALI, EITHER UTAKUJA KUPATA MAFANIKIO YA KIMAISHA BAADAE KTK KUANGAIKA KWAKO KUTAFUTA , ,,,trust god
 
Naota napita sehemu ninayo ifahamu lakino mwisho napotea kwa kutokea sehemu nisiyoifahamu
Ndoto inajirudia miaka kumi sasa
 
Hivi ikiwa nimeota nakimbiza bata nina maana ya bata co tafsiri nyengne ,wakati namkimbiza huwa najitahidi sana kumkaribia lakini simpati na nguvu ya mm kukimbia inapungua sana. Je, hii ina maana gani?
 
Mara nyingi naota nafanya mapenzi na msichana mwenzangu wakati mwingine nimetoka kufanya na mume wangu nikipitiwa na usingizi naota nafanya na msichana mwenzangu Mara nyingi niwaota marafiki zangu, msaada hapo.
 
Hivi ikiwa nimeota nakimbiza bata nina maana ya bata co tafsiri nyengne ,wakati namkimbiza huwa najitahidi sana kumkaribia lakini simpati na nguvu ya mm kukimbia inapungua sana jee hii ina maana gani

Ina maana achana na starehe sio wito wako. Shinda na familia yako nyumbani mkuu
 
Je, ukiota unatumbukia shimoni tena shimo kubwa ,je hiyo ina maana gani?
 
Naota napita sehemu ninayo ifahamu lakino mwisho napotea kwa kutokea sehemu nisiyoifahamu
Ndoto inajirudia miaka kumi sasa
Kuna jambo linaendelea, na kuna mipango inapangwa dhidi yako, bila wewe kujua. Tena ni watu wako wa karibu(njia) Huenda mwisho wake hautokuwa mzuri kwako.(njia usioyoijua)
 
Mara nyingi naota nafanya mapenzi na msichana mwenzangu wakati mwingine nimetoka kufanya na mume wangu nikipitiwa na usingizi naota nafanya na msichana mwenzangu Mara nyingi niwaota marafiki zangu msaada hapi
kuna mapepo huwa yanaharibu ndoa/mahusiano nk. Tazama, kuna pepo baya linakuja kuleta mgogoro ktk ndoa yako.
 
Hivi ikiwa nimeota nakimbiza bata nina maana ya bata co tafsiri nyengne ,wakati namkimbiza huwa najitahidi sana kumkaribia lakini simpati na nguvu ya mm kukimbia inapungua sana jee hii ina maana gani
tazama, shughuli zako za kiuchumi zitayumba, na matumizi ya pesa hayatokuwa sawa. Kuna roho chafu imekuandama inakurudisha nyuma ktk mafanikio.
 
Mara nyingi naota nafanya mapenzi na msichana mwenzangu wakati mwingine nimetoka kufanya na mume wangu nikipitiwa na usingizi naota nafanya na msichana mwenzangu Mara nyingi niwaota marafiki zangu msaada hapi
Utakuwa una jini mahaba wa kike anaitwa msalibianil kwa ushauri zaidi ni pm nikusaidie
 
Sigmund Freud first argued that the motivation of all dream content is wish-fulfillment, and that the instigation of a dream is often to be found in the events of the day preceding the dream, which he called the "day residue." In the case of very young children, Freud claimed, this can be easily seen, as small children dream quite straightforwardly of the fulfillment of wishes that were aroused in them the previous day (the "dream day").

In adults, however, the situation is more complicated—since in Freud's submission, the dreams of adults have been subjected to distortion, with the dream's so-called "manifest content" being a heavily disguised derivative of the "latent" dream-thoughts present in the unconscious. As a result of this distortion and disguise, the dream's real significance is concealed: dreamers are no more capable of recognizing the actual meaning of their dreams than hysterics are able to understand the connection and significance of their neurotic symptoms.
 
Back
Top Bottom