Dada divine naomba uiangalie hii na nitakuja PM pia.
Nimeota mara nyingin nakimbizwa na n'gombe mweusi mkubwa sana ana pembe Kali mno.
Mara nyingi nimekuwa nikimkimbia sana sana na pia siku moja aligeuka na kuwa kijana wa kiume simfahamu akaanza kunirushia mishale mikali mingi sana lakini haukunipata hata mmoja yani. Alirusha mara nyingi sana approximately mara 20 kisha akaja bibi mmoja rafiki yake na bibi yangu akasimama akamuangalia akaacha kurusha mishale akapotea .(mazingira ni kwetu kijijini)
Mara nyingine nimeota ng'ombe hiyo akitaka kuniingilia ( mazingira hapa sijajui)
Baada ya kuota mara nyingi juzi nimemuota huyo ng'ombe mweusi amekuja akiwa anajipanga kuanza kunikimbiza nikachukua fimbo ya ufagio nikampiga hadi akatoka kichwa minofu inadondoka chini.
Ndoto nyingine naota nakimbizwa na nyoka
Mszingira siyafahamu kabisa
Kuna siku mtoto wangu alikuwa amekaa ghafla nikaona nyoka mdogo kaja nikamkata yule nyoka!
Tena nikaona nyoka mwingine amekomaa hadi ana manyoya anapita pale pale nikataka kumzuru kwani mwanangu yuko pale ila akapita, wkt name gang as nikaona nyoka mwingine amejibanza pembeni nikamuangalia tu..
Vipi kuota marehemu mzazi kbs anaumwa sana yupo hoi alafu usafiri wa kumfikisha hospitali ni changamoto?
Mara marehemu anelala nyumbani anaumwa
Mara nyingine naota MTU ambae bado hajafa namuota amekufa
Kuna siku nimeota kuwa binti yangu amekufa kwa kuangushwa chini na dada wa kazi na nilipomuuliza akawa kiburi tu kujibu ndio hataki.
Naota nakula minyama mimi na binti yangu..
Naomba unitafsirie kwa uwezo ulionao. Najua nipo vitani na nine shanks finish a YESU awe bwana wa jeshi langu.
Sent using
Jamii Forums mobile app