Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Ndoto tunazoota na tafsiri zake

No Maisha yangu yako poa sana, pengine yako ndio yako vuluvulu, km sio mtaalamu wa ndoto ukaelewa MTU ameeleza mini, kunyamaza sio ujinga ila ni busara kubwa.
Kwa hiyo wewe pia huna busara kubwa maana ungenyamaza tu.
 
[emoji28] [emoji28] [emoji28]

Nisamehe dada yangu. Wakati mwingine natumia maneno bila kufikiri ila nia haikuwa mbaya. Unaweza kuwa na maisha mazuri kwa maana ya uhakika wa kuishi - unavaa na kupendeza, kulala pazuri na nini lakini kisaikoljia ukawa huna utulivu. Unakuwa na ombwe kwenye nafsi ambalo na kupelekea misururu ya ndoto. Siyo wewe lakini. Umeshaliweka sawa.
 
ndoto hiyo inakuhusu wewe mwenyewe, maisha ya mwanadamu hapa duniani ni safari yake tangu anazaliwa hadi anakufa! hiyo ndoto inahusu maisha yako! jaribu kukaa chini , andika mipango yako yote ya maisha , mipango ya muda mfupi kama mwaka mmoja na mipango ya muda mrefu miaka mitano na kuendelea, andika nini unakitaka katika maisha yako na hujakipata mf mke mzuri, gari zuri , kazi nzuri, nyumba nzuri ,watoto wazuri, pesa za maana na tafakari namna utaifanikisha hiyo mipango, kisha andika kina nani watakusaidia kuifanikisha uwagande kiakili bila wao kujua na andika kina nani wanakukwamisha ( watu unaogambania nao usafiri) na kukukatisha tamaa uanze kukata mazoea nao hata kama ni marafiki zako na unawapenda sana! kisha angalia nyenzo (bus) unazohitaji kuwin na unazipataje, na angalia changamoto ( watu unaogambania nao usafiri in dream means changamoto) zote na utafakari utazikwamuaje! kumbuka hutakiwi kushare na mtu yoyote mambo haya utakayoandika! ni siri yako tu!
Aandike bila kuomba Mungu awagande watu bila kumshirikisha Mungu?
 
kuna elimu za aina mbili, kuna elimu ya dini ambayo ofcourse unamhusisha Muumba katika kila kitu na kuna elimu dunia, hii ni kutafsiri ndoto tunazoota kwenye maisha yetu bila kuangalia suala la dini, nimejibu kupitia elimu dunia , nilivyomuelewa he is very ambitious person na anahitaji mikakati na zana za kufikia malengo yake, hicho tu.
Ok
 
Mtumeee!!! Kama umejibiwa PM nifowadie majibu. Nilikuwa nikiota joka lenye rangi nyeusi juu, nyeupe katikati na njano mkiani likinitimua. Na ndoto moja ilifanana kabisa na hii yako. Alipokuwa akinikimbilia kuna watu walikuwa wanampiga mawe halafu yale mawe yananipata mimi ila hayaumi - aliponikaribia aligeuka kuwa kaka ninayemfahamu. Siku zote nilizoota ndoto ya kupambana na hilo joka mazingira ni kijiji nilichokulia, kando ya mtoto penye majani mazuri na miti. Kuna siku bwana nikamkuta katikati ya barabara. Amegawa barabara katikati kama ile mistari ya kutenganisha leni. Alikuwa mrefu sioni kichwa wala mkia. Nikasema huyu kichwa kitakuwa mbali sana acha nimruke nivuke zangu. Lahaula! Ghafla joka liliniinukia na domo kubwa lenye ute ute na meno makali usoni kwangu. Nilishtuka usingizi nikiwa nimetota jasho natetemeka hatari. Nilibaki na hofu mwezi mzima. Nilikuwa shallow sana sijui hata kuomba. Mama yangu ndo akawa ananiombea. Siku moja nikaota nimelikuta mahali limepondwa limekufa. Sijawahi kuota tena. Miaka mingi imepita ila natamani kujua maana ya lile joka, zile rangi na yale mashambulizi.

Hii ya kuota marehemu ndo sisemi. Mtu hata kama sijawahi kumuota akishakufa tu lazima atanihusu kwenye ndoto. Kuna kaka ni ndugu tu wa ukoo alikufa. Sikuwa nimewahi kumuona maisha yangu yote. Baada ya maziko nikamuota. Baadae kwenye ulimwengu halisi nikaja kuona picha yake sura ni ile ile niliyoiona ndotoni. Hii hali ilizidi kunitisha. Majuzi nimeota nauguza watu mahututi ambao tayari walishakufa! Ina maana mimi ni marehemu ila sijijui au ????!
Umekuwa na adui (huyo nyoka). Adui huyo kapanga hila za kukuangamiza(mabaka ya nyoka hizo rangi ni hila kwako). Umetegwa njia zote upitazo(kumuona barabarani). Mungu kupitia maombi kakuepushia mauti (kumuona kafa baada ya mama kukufanyia maombi). Simamia imani iliyokuokoa.
 
mimi kunandoto nishaotaga mara mbili ambapo huwa naota ni mida ya usiku nataka ningie ndan wakat huo mlango upo kama niliuwacha wazi nikaondoka kwenda misele alafu anatoka mtoto kama wa miaka 13 alaf huwa naingia hofu alafu na mkemea ktk jina la Yesu ila yeye anasimama nikitamka damu ya Yesu anakimbia akicheka kwenye hiyo nyumba ni nyumba ambayo walikuwa wanaishi babu na bibi ambao washafariki ila zamani nishalala huko ila sasa hv silali huko lakn naota nalala huko
 
Ahsanteni kwa tafsiri za ndoto, nimejifunza vitu vingi kupitia uzi huu
 
Kuna nguvu unayotaka kuvishwa ya maagano ilishatanguliwa na wahenga wako. Vunja kwa sala za mfungo tu siku tatu utaharibu kila kitu.
 
Divine... Mimi niliota ndoto ya ajabu siku ya jumamosi kuamkia jumapili. Niliota nimetangazwa mshindi wa tuzo ya billion moja. Lkn nikapewa milioni 700 na kitu, ile nyingne ya juu nikaambiwa imetumika kuwezesha sherehe na mchakato wa kunipa hyo tuzo.
Na napitia wakati mgum kiuhalisia kwasasa, sina kazi na natafakari namna ya kutoka. Hiyo ndoto niliiota ucku wa manane. Na ktk ndoto hiyo bada ya kupata tuzo hiyo ilikuwa kama nimefanikiwa kutoboa maisha.

Sasa sijaelewa hiyo ndoto ina maana gani labda?!
 
Angalia 110
Kiongozi usiku wa kuamkia leo nimeota nipo sehemu na nina njaa mda kidogo akapita mtu na mkungu wa ndizi,ikabidi nimuombe kutokana na njaa niliyokuwa nayo lakini jamaa akaniambia ndizi mbichi na nikweli ndizi karibu zote zilikuwa zinaonekana ni mbichi.Ikanibidi niutazame kwa makini sana ule mkungu wa ndizi na bahati nzuri nikaiona moja imeiva na kumuonyesha jamaa na akanichumia sasa kilichotokea ni kwamba baada ya kunipa ile iliyoiva za nyuma ya ile ndizi nyingine zikawa zinaiva ananipa yaani hali ikawa ndio hivyo hivyo akinichumia ndizi za mbele za nyuma yake ambazo zilikuwa mbichi zinaiva.
TAFASIRI PLEASE
 
Kula matunda ni ishara ya kuwa utapata neema fulani muda si mrefu ila unahitaji kufungamana na Mungu wako (kubanana kwa ndizi) na kuwa mwaminifu.
 
Kula matunda ni ishara ya kuwa utapata neema fulani muda si mrefu ila unahitaji kufungamana na Mungu wako (kubanana kwa ndizi) na kuwa mwaminifu.
Kuna siku niliota nipo na wanafunzi niliosoma nao shule ya msingi nilikuwa nao nyumbani nikawa nawagawia maembe yaliyoiva sana yale madogo ambayo watu hunyonya....
Nini tafsiri ya hii ndoto?
 
Kuna siku niliota nipo na wanafunzi niliosoma nao shule ya msingi nilikuwa nao nyumbani nikawa nawagawia maembe yaliyoiva sana yale madogo ambayo watu hunyonya....
Nini tafsiri ya hii ndoto?
Ni ishara ya wewe kuwa sehemu ya baraka kwa wengine (kujiona unawagawa wengine matunda).
 
Back
Top Bottom