Nashukuru sana kwa ushauri wako, lakini miasha yangu yana stori complicated kdg kuhusu haya mambo ya kiroho.
Maana kuna wakati huwa naota kama naongea na mtu lkn yupo kwenye taswira na umbo la duara kama jua na anatoa mwanga mkali sana mweupe, mara nyingi anayoniambia hutokea kama alivyonielekeza.
Mfano mwezi wa 11 mwaka jana nilitakiwa kwenda safari na watu furani mkoani na tulipanga kuondoka jioni, Cha ajabu siku ya safari kuna mazingira yalitokea tu baada ya kumaliza kula mchana nikapitiwa na usingizi (nilikuwa nyumbani).
Alipokuja usingizini (huyu mwenye taswira ya duara) aliniambia sitakiwi kwenda safari ile na sitakiwi kabisa kusafiri siku ile na kweli sikwenda,
Sasa kilichoenda kutokea kwa wale wenzangu walipata ajari mikumi na hakuna aliyepona wote wanne walipoteza maisha..
Basi,mtoto Samweli akamtumikia BWANA mbele ya Eli,Na neno la BWANA lilikuwa adimu siku zile ;hapakuwa na mafunuo dhahiri.
2.Ikawa wakati huo,Eli alipokuwa amelala mahali pake (tena macho yake yalikuwa yameanza kupofuka, hata asiweze kuona),3 na taa ya Mungu ilikuwa haijazimika bado,na Samweli alikuwa amelala katika hekalu la BWANA,palikuwa na sanduku la Mungu;4 basi,wakati huo BWANA akamwita Samweli;naye akasema, Mimi hapa.
5.Akamwendea Eli kwa haraka ,akasema,Mimi hapa;kwa maana uliniita. Akasema ,Sikukuita;kalale tena.Naye akaenda, akalala tena.
6.BWANA akaita mara ya pili,Samweli!Samweli! Akaondoka akamwendea Eli,akasema,Mimi hapa;kwa maana uliniita, Akajibu, Sikukuita, mwanangu;kalale tena.
7.Basi Samweli alikuwa hamjui BWANA bado,na neno la BWANA lilikuwa bado halijafunuliwa kwake.8. BWANA akamwita Samweli mara ya tatu, Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa;kwa maana uliniita, Ndipo Eli akatambua ya kuwa BWANA ndiye aliyemuita yule mtoto.
9.Kwa hivyo Eli akamwambia Samweli, Enenda, kalale;itakuwa ,akikuita, utasema, Nena,BWANA;kwa kuwa mtumishi wako anasikia.Basi Samweli akaenda akalala mahali pake.
10.BWANA akaja, akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli Samweli! Ndipo Samweli akasema,Nena ,BWANA ;kwa kuwa mtumishi wako anasikia.
11.BWANA akamwambia Samweli ,Angalia, nitatenda tendo katika Israeli ,ambalo kila atakayelisikia masikio yake yatamwasha.
(1Samweli 3:1-11).
Ndoto yako jibu lake liko hapo.
Bila shaka umemjua huyo anayekuja kwa mg'ao sawa na Ufunuo wa Yohana 1:16 Naye alikuwa na nyota Saba katika mkono wake wa kuume;na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake;na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.
Samweli aliitwa mara 3 pasipo kuijua sauti ya Mungu ndipo mara ya 4 akaitika sawa sawa na Mungu alivyotaka aitike baada ya kufunuliwa na Eli.
Umekuwa ukimuota huyo mtu ila hukumjua ni nani mpaka ulivyokuja kuuliza hapa, sasa umeshamjua kwahiyo kazi kwako kufuata maelekezo yake maana ana ujumbe wako.
Unaota unafunga ndoa na una watoto wawili.
Uko kwenye kifungo ambacho hujajua ni upande wa Mungu au wa shetani. Hapa inaonyesha kila upande unakutaka uutumikie, kwahiyo ni wewe kujinasua kutoka kwenye hilo agano au kujua ni agano lipi umefungwa nalo.