Ndoto ya Marekani kuivamia Urusi sasa yatimia

dah waafrika sisi
 
Hapana mkuu mimi ndio mwenye thread. Kwahiyo kuna mtu ulim quote ila na mimi nikataka kujua sababu ya kuoneshwa kushangazwa na uafrika wetu, mpaka ukaandika vile
aah! kuna myahudi mmoja kutoka huko simiyu bariadi kachafua koment mkuu
 
Boss, Umechambua kishabiki mno. Tunakosa la kujifunza kupitia uzi wako.
Ukisoma kwa umakini sana maelezo yake ni wazi hajui hata kilicho tokea leo, wala impact yake kwenye masuala ya mabeberu na Russia - mbona Russia wakati mwingine anavurumisha rockets na mabom babu kubwa kutifua concrete Bunkers walipo jificha baadhi ya majenerali wa US,Poland nk bunkers zinageuzwa vifusi kabisa - mpaka sasa maafisa hao wakuu wa jeshi imeshindikana kuwaokoa wamekufa kifo kibaya - sasa mbona hatujaona au kusikia US ikituma/vurumisha similar poweful missiles/bombs kuishambulia Urusi kama kulipiza kisasi - wapo kimya kabisa, badala yake wanawapatia jeshi la Ukraine vi drone vya (DIY) kwa lengo la kuwatia taaruki wakazi wajini Moscow ili BBCna CNN wapate cha kuandika. vi drone hivyo vinarushwa na ma terrorist waliyo penyezwa na Ukraine intel agency na CIA walipo ona plan "A" yao ime fail miserably ndio wakaja na plan "B" hii ya kuwatumia magaidi kama ilivyo kuwa huko Syria mpaka Russia ikapashwa kuingilia kati kumuokoa Assad asipinduliwe na kuuwawa na mabeberu kama Gaddafi.

Sasa swali ni: kama ni kweli US/NATO awaogopi Russia mbona anatumia Taifa lingine dhaifu kuendeleza mgogoro ambao hauna kichwa wala miguu - mwisho wa siku mabeberu wakiongozwa na Merikani wala hawataweza kuishinda/dhoofisha Russia kijeshi wala Kiuchumi -watabaki kuabika wao, angalio kinacho endelea huko Ulaya magharibi hivi sasa, vurugu tupu,hakuna kazi, viwanda vinafungwa ovyo - mpaka wanabaki wanajilahumu kwa ujinga wao kwa kufuata siasa za Merikani kama vipofu.
 
Kwani aliyeanzisha vita vya Ukraine ni nani kiongoi
 

Wewe umebeba kichwa kama mzigo, hujui kitu, nitajie vita hata moja Marekani amewahi shinda, taja moja. Kama hujui kitu, kaa kimya.
 
Wacha propaganda wewe. Kama Marekani ingekuwa na haja ya kuivamia Urusi ingefanya hivyo miaka ya tisini baada ya USSR kusambaratika na kuiacha urusi ikiwa maskini sana. Marekani iliisaida sana Urusi kwanza kupata silaha zote za Nyuklia zilizokuwa Ukraine, na pia kuipa mikopo mingi sana ya kufufua uchumi wake. Putin anapokosa ajenda anatengeneza maadui wa cold war kutisha raia wake na yeye kuonekana mtetezi wao.
 
Ina
Inasemekana.
 
Wewe umebeba kichwa kama mzigo, hujui kitu, nitajie vita hata moja Marekani amewahi shinda, taja moja. Kama hujui kitu, kaa kimya.
Wewe umemezeshwa maneno lkn kwa bahati mbaya waliokumezesha wamekuficha baadhi ya mambo.

Marekani kama Marekani huwa haiingii vitani hovyo hovyo, bali hupigana tu vita vya mikakati kama hizi unazoziona za mbali mbali, huku Marekani kwenyewe watu wakiendelea na shughuli zao za kimaisha, kimziki, burudani, watu wanaingia nchini na kutoka, biashara zinafanyika kama kawaida, nk bila hata watu kujua kama nchi hiyo ipo katika mikakati ya vita.

Lakini Marekani yenyewe kama inaamua kuingia vitani kwa style hii ya Urusi kwamba imeingia vitani hadi kukusanya wanajeshi wake wa akiba, vijana kulazimishwa kupigana nk, ujue hapo ni lazima yatokee ya Japan kitu ambacho dunia na Marekani yenyewe haitaki kukishuhudia.

Ukitaka kujua kama Marekani inapoingia kwenye vita kamili kama ya Urusi huwa inashinda au inashindwa iulize Japan na Vietnams kilichowakuta katika ardhi yao.
 
Russia wamesema drone, sio makombola kama unavyosema wewe. Na hizo drone zinarushwa na magaidi ambao wapo ndani ya urusi kinyemela
Sasa wewe unafikiri hao magaidi wanaweza kuanzisha ugaidi ndani ya ardhi ya nchi kubwa kama Russia bila kuwa na support ya Mmarekani nyuma yao.

Wewe unafikiri hizo drone walizipata wapi?
Na ziliweza kuingiaje nchi Urusi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…