Ndoto ya Marekani kuivamia Urusi sasa yatimia

Angalau ww umeweza kunishawishi nielewe ulichoandika.

Ila hawa warusi wengine wa mwananyamala kwa manyanya wengi wanakimbilia kunilaumu muandikaji badala ya kupingana na fact kupitia facts.
 
jeuri ya Putin ipo kwenye nyuklia kwamba akiona maji ya utosi anabonya batani tufe wote ila ubavu wa kupamba na marekani hana na hatowahi kuja nao
 
Sasa wewe unafikiri hao magaidi wanaweza kuanzisha ugaidi ndani ya ardhi ya nchi kubwa kama Russia bila kuwa na support ya Mmarekani nyuma yao.

Wewe unafikiri hizo drone walizipata wapi?
Na ziliweza kuingiaje nchi Urusi?
Ni ngumu sana kumdhibiti binadamu kwa 100%.. Kumbuka. September 11 Marekani pia alifanyiwa ugaidi mkubwa sehemu nyeti ndani ya marekani. Hata mke wako au kipenzi chako hautaweza kumdhibiti 100% ili asichepuke🀣🀣
 
Pale Vietnam walikimbia kaka, hawakuteka hata kijiji... hata Japan walitumia nuclear weapons.. je urusi atumie nuclear weapons?

USA hajawahi pigana vita ya peke yake akashinda? Hata hii amawatanguliza Nato na Ukraine, mpka leo Ukraine wamepoteza 20% ya ardh. Sasa US ana msaada gani?
 
Ni ngumu sana kumdhibiti binadamu kwa 100%.. Kumbuka. September 11 Marekani pia alifanyiwa ugaidi mkubwa sehemu nyeti ndani ya marekani. Hata mke wako au kipenzi chako hautaweza kumdhibiti 100% ili asichepuke🀣🀣
Ni kweli ni ngumu kumdhibiti binadam, lkn lile tukio la Sep 11 lilipangwa na Marekani wenyewe wakishirikiana na CIA mwenzao wa kiarabu aliejipa jina la Osama bin Laden, ili wapate uhalali wa kwenda kuzivamia nchi za kiarabu zenye rasilimali za mafuta na mihadarati kwa kisingizio cha kumtafuta Osama kwenye nchi hizo.

Ndio maana mwanzo mwanzo vijana wengi (hasa wakiislamu) waliokuwa hawajajua kinachoendelea kati ya Osama na Marekani walikuwa wanafurahia na kuona kweli kwamba jamaa kawaweza Marekani na kamwe hawatoweza kumdhibiti nk.

Ila duniani hakuna lililo la siri ambalo mwisho wake hugeuka kuwa la dhahiri, baadae wenye akili wakaanza kugundua kwamba Osama na genge lake walikuwa ni ma CIA wa Marekani waliotumiwa kama chambo kwa taifa hilo kubwa duniani lenye mbinu mbali mbali za kijasusi kuzivamia nchi walizozilenga kwa mipango mahsusi.

Ndio maana toka kitangazwe kilichoitwa kuwa ni kifo chake mpaka leo hakuna mwananchi au hata mwanandishi habari wa kitaifa au kimataifa aliwahi kushuhudia mwili wake au kaburi lake kama ilivyo kwa wale waliokufa vifo vya kweli kina Saddam Hussein, Gadafi na wengine wa aina hiyo. Just unganisha dot utaelewa ninachoandika hasa pale Osama mwenyewe alipoanza kuwaandaa watu kisaikolojia kwamba eti wako kina Osama wengi wanaofanana, hivyo hata akifa yeye wasishangae watapomuona mungine anaefanana na yeye.

Osama hakuuwawa na Marekani kama tulivyoaminishwa, bali yupo zake Marekani akila bata na watu wakikutana nae njiani pengine akiwa kanyoa au kapunguza urefu wa ndevu wanakumbuka ile kauli yake kwamba alisema yeye akifa kuna wengine watakuwepo kama yeye ili watu wasishtuke kuwa jamaa yupo hai salama bin salmini akila zake burger, tende na nyama choma kwa kazi nzuri aliyoifanyia Marekani.

Si unaona siku hizi hata wale vijana waliokuwa wanajifanya ni itikadi kali duniani wameshapungua, baada ya kugundua kuwa Alkaida sijui Islamic state nk ni vitengo vya CIA vilivyopandikizwa huko yanapopatikana mafuta kwa kazi maalum.
 
Marekani alitumia tukio hilo la September 11 kuivamia Afghanistan. TUnakubaliana hapa kuwa ule uvamibi wa NATO kuwa ni batili??
 
jeuri ya Putin ipo kwenye nyuklia kwamba akiona maji ya utosi anabonya batani tufe wote ila ubavu wa kupamba na marekani hana na hatowahi kuja nao
Ya ni kweli mkuu, ila ogopa sana watu wanaoitwa CIA. Hawa kadri siku zinavyokwenda, vita vinavyozidi kupiganwa ndivyo na wao wanavyozidi kujisogeza karibu na maeneo muhimu na watu muhimu huko Russia kimya kimya.

Itafika kipindi Putin atabonyeza akijua anabonyeza kitufe cha nyuklia ili tufe wote, kumbe anabonyeza toy tu huku kitufe chenyewe original kikiwa kimeshachukuliwa muda mrefu na Marekani kupitia hao hao vijana wa Putin kwa njia za kijasusi.

Let's say mfano jasusi wa Putin analipwa M10 kwa ajili ya kutembea na betri au funguo za kitufe hicho, afu mzee Biden amauahidi jasusi huyo kuwa atampa M500 na nyumba, magari na uraia wa kudumu tena wa hadhi ya heshima wa Marekani. Atakataa?

Unafikiri Saddam alipatikana vipi huko shimoni alipojificha kama sio hela zilitumika kwa baadhi ya walinzi wake tena aliowaamini?
 
Marekani alitumia tukio hilo la September 11 kuivamia Afghanistan. TUnakubaliana hapa kuwa ule uvamibi wa NATO kuwa ni batili??
Nakubaliana na wewe kuwa vamizi zote za NATO kuanzia mwaka 2000 hadi leo huko Iraq, Afghanistan, Libya nk zilikuwa batili.

I mean zilikuwa ni za kimasilahi tu.
 
Putin alisema yeye Magaid hana cha mswalie mtume anawawahisha ahera wakapate mademu 60.
 
Ndio maana nikakwambia kuwa Marekani anapigana vita ya kimkakati, ambayo haimpi hasara kubwa kifedha na kijeshi.

Marekani haogopi vita kamili, maana ni wazi kuwa akiingia mzigoni kwa vita kamili bado atashinda tu mchana kweupe.
Sema kinachofanya Marekani asipigane vita kamili ni kwa sababu hataki uchumi wake uanguke kutoka kuwa taifa namba 1 tajiri hadi kuwa taifa namb 2, 3 au 5.

Kitendo cha yeye kutumia nchi kama Ukraine ambayo iko mlangoni mwa Russia kupigana vita vyake sio cha kitoto kinahitaji fedha, mbinu, mikakati na maarifa ya hali ya juu.

Urusi iliwahi kujaribu kufanya hivyo kwa Cuba lkn kilichotokea mpaka leo mnakiona. Vikwazo vidogo tu vimesababisha raia wengi wa nchi hiyo kukaribia kula nyasi.

Mpaka leo hakuna tena nchi iliyojirani na Marekani inaweza kufanya mzaha ule.
 
Watu mnasahau kwamba Russia walishapigwa na hayo ma patriot zamani sana na huyo mmarekani.
Ndio uchumi wote ukadondoka pwaa.
Sasa leo Putin atavalishwa kibwebwe tu achezeshwe mdundiko.
Na hiyo vita haipo.
 
Hayo ni mawazo yako kulingana na upeo wako. Kama ingekuwa hivyo unavyofikiri marekani hasingekuwa anahaha hapo Ukraine
 
Nakubaliana na wewe kuwa vamizi zote za NATO kuanzia mwaka 2000 hadi leo huko Iraq, Afghanistan, Libya nk zilikuwa batili.

I mean zilikuwa ni za kimasilahi tu.
Sasa kwanini kuna vilio vingi sana Russia anapofanya mambo kwa maslahi yake??
 
Putin alisema yeye Magaid hana cha mswalie mtume anawawahisha ahera wakapate mademu 60.
Ashachelewa mkuu. Magaidi wakishafanikiwa kutoka katika mpaka hadi katika capital city yako basi ujue hapo ni kwisha habari yako.

Maana tayari washajichanganya na raia, sana sana utauwa hata wasiohusika kisa wamefuga ndevu.
 
Mimi naona hapo Ukraine marekani anapata hasara sana kijeshi na kifedha. Kwasasa serikali ya Ukraine inafadhiliwa na NATO na jumuiya ya ulaya.

Na kijeshi anapata hasara sana kwa maana kila silaha anayopeleka inadhibitiwa na Russia mpaka mfumo wake wa ulinzi wa anga aliokuwa anajimwambafai naa umeweza kutandikwa. Hali hiyo inamwalibia sana kwenye biashara yake ya silaha
 
Mkuu amka usije ukakojolea kitandani.
 
Kuna thread inayohusiana na vita hii. Mkuu nakukaribisha kwenye thread hiyo ili uje upate uelewa zaidi wa vita hii. Achana na ushambenga huu!!
 
Sasa kwanini kuna vilio vingi sana Russia anapofanya mambo kwa maslahi yake??
Inategemea na aina ya masilahi. NATO na Marekani wanavamia kwa lengo la kujipatia tu rasilimali za nchi husika kama vile mafuta, madini nk.

Lakini Urusi inavamia kwa lengo la kuteka na kuchukua ardhi ya wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…