Ndugai ashukiwa "kama Mwewe" na Mwenezi wa Njombe

Hii ndio aina ya watetezi wa Rais Samia?
 
Spika Ndugai ndie ameanzisha moto,lakini si hivi hivi nadhani kajipanga kwa lolote.
Hakosi volunteers wabunge ,akiamua kuiwekea kauzibe serikali ya Mama SSH,lazima itayumba kwa kiasi fulani kupitisha miswaada bungeni.Tatizo wabunge wengi wanamuogopa Ndugai.
Kwa upande wa Mama yetu yeye anao vigogo wenye ushawishi mkubwa ndani ya chama na nje ya chama.Ila hatutegemei kuona Speaker anaendelea kukwaluzana na Mkuu wa nchi siyo ishara nzuri kwa CCM.
 
Yaani hiki kinachoendelea kwa kweli sio ishara nzuri kwa Rais Samia ila ni ishara kwa UKOMBOZI wa nchi hii.Yaani hii nchi inavichekesho sana na sielewi kwa nini mama anapigwa fitna,hebu angali mpuuzi aliyemuandalia hotuba Rais ya desemba 31/12/2021 yaani ni Ugolo mtupu.Badala ya kuzungumzia hali tete ya ugumu wa maisha ya watu wanamuandalia Rais vitu vya hovyo visivyogusa maisha yao tena kwa wakati muafaka.
 
Kwani CCM haina vikao vya chama??!!, mbona mnaanika hadharani nguo zenu za ndani??!!🤣

..kwanini waongee mafichoni kwenye vikao vya chama?

..nadhani wakiweka hoja na misimamo yao hadharani ni jambo zuri.

..wananchi tutajua viongozi wana misimamo na malengo gani kuhusu masuala muhimu ya kitaifa.

Cc Tindo, Nguruvi3
 
Aiseee kwasasa nchini hii inashida, huyo dogo inawezekana anahoja ila anavyoifikisha sasa,nayeye anakuwa muharifu kabisa.......halafu huyu unakuta siku anateuliwa kuwa DC kwaakili hizi tunasafari ndefu.....Ndugai inawezekana katoa ya kweli ila sasa nani atamsikiliza kwasababu ya unafiki wake?
 
Katika suala la msingi ambalo afrika tunachelewa Safari ya maendeleo ni Kwenye matumizi ya ela.

Ndio maana hata Hii mikopo ni bora ukope sana lakini uone matokeo yake na kuwe na uwazi Katika matumizi kuliko kukopa kidogo na matokeo yawe sifuri watu wajigawie siku zipite
 

..wakati wa Mkapa tulikuwa tunalilia tusamehewe madeni.

..leo wanaibuka viongozi wanataka nchi ikope bila kuonyesha mikakati ya kulipa madeni yetu.
 
K gang wamepoteana, hamna anayewaunga mkono, sio CCM sio UPINZANI, na wasukuma halisi hawawataki pia, 2030 for January njia nyeupee
 
Huyu mwenezi inawezekana elimu yake siyo zaidi ya darasa la nne...hoja inawezekana anayo lakini uwasilishaji wake ni wa kiwango Cha chini kabisa...yasni kutaja mpaka kabila la Ndugai??! Maana yake Nini hads?! Yaani wagogo hawafai?!?! Dah...CCM ipo hatarini kabisa....CCM huwa inawaokota wali viongozi Kama Hawa?! Pengine alitoa kauli hi baada ya kunywa ulanzi...hovyo kabisa...
 
Huuu ni mwanzo tu, hii ni rasharasha Sheikh mzigo mzima uko njiani
 
Hahaha vipi kuhusu kibajaji na msukuma??
 
Kama huna bando ni hivi, Ndugai aliupata Uspika kwa fitna dhidi ya Mama Anne Makinda, Ndugai alitibiwa kwa mamilioni ya fedha ughaibuni na hajapona Bado, Ndugai ana tabia ya kuwachapa bakora wapinzani wake...
wakati ndugai anapata uspika anna makinda alishastaafu. Anna makinda alipata uspika ili kumpunguza kasi sitta.
 
We una roho na nafsi ya kichawi kabisa, ulitaka aende kwa sangoma au mganga wa kienyeji au ulitaka afe???
Ila hili swala la Ndugai kutibiwa kwa Tsh. 2B ni moja ya matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.
 
KIGOGO ANAASEMA ANADANGANYWA NA KINA OILCOM KWAMBA WATAMLIPIA ADA KUPIGANIA URAIS 2025,NDIO MAANA UFAHAMU UNAONDOKA
#SSH_2021-#2030.
*AMESHAPITA BADO KUAPISHWA TU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…