#COVID19 Ndugai: Chanjo ni hiyari ila hauna hiyari kuambukiza wenzako

#COVID19 Ndugai: Chanjo ni hiyari ila hauna hiyari kuambukiza wenzako

Bungeni hakujawahi hata kulazimika kuvaa barakoa au kujitenga kwa kukaa mbalimbali ili kuepusha maambukizi ila ajabu et wanafanya ulazima wa chanjo et ili wasiambukizane corona.
 
Ndomaana huwa nasema hakuna hata moja la kweli ambalo CDM mmewahi kulipigiania , mara zote huwa mmetanguliza masilahi yenu na sio Taifa.

Hivi watu mnaolilia utawala wa sheria, unawezaje kushadadia swala la wabunge kulazimika kusupport kitu kwakua Rais kafanya? BUNGE NA Rais wapi na wapi?

Upuuzi mtupu, watcha mnyooshwe kabisa.
Huyu USSR Ni CCM labda Kama wewe Ni mgeni hapa JF..tena Ni wale CCM wa matusi
 
Wakuu soon tamko la katibu wa bunge kwenda kwa wabunge wote wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa lazima wachanjwe la sivyo hawataruhusiwa kuingia bungeni mwenzi ujao .

Wabunge watatakiwa kuwasilisha kadi za chanjo kwa walinzi ili kuruhusiwa kuingia bungeni.

Wabunge wanatakiwa kuwa mifano ya jamii na chama Cha mapinduzi na kumuunga mkono mh. Rais ambaye tayari amesha chanjwa.

MY TAKE. Msimamamo wa gwajiboy na poleople utaonekana hasa wakigoma kuingia bungeni

USSR
Wewe ni miongoni mwa masikini walioshambulia Chadema kwa kujitenga baada ya wabunge kadhaa kupukutika kwa corona , eti leo unasapoti Chanjo ! ama kweli njaa haina baunsa .
 
Kwa lugha nyepesi ni kwamba Job analazimisha wabunge wachanje. Na kama patatokea Mbunge ambae hajachanja, basi Mbunge huyo hato ruhusiwa kushiriki ndani ya mbunge kwa kisingizio cha atawaambikiza wengine.
Anyway..... Wakubwa tumemuelewa vyema Mh 🔉 Job
Askofu Rashid na Comrade Polepole
 
Hili jukwaa kwa sasa lina mkono wa mabeberu na mawakala wao.

Nyuzi kama hizi zinazoleta taharuki ya corona ndizo zinazopendwa sana hata kama ni za kutunga.
Hii Vita Ni ya kiroho Sasa.Na Vita yetu so just ya damu na nyama no juu ya pepo wabaya Katika ulimwengu wa wa Roho .Wao wanatujia kwa jina La chanjo na jina La mzungu na vyeo sisi tutasimama na Mungu .Tuone Nani atashinda

Ninachojua wapinga Chanjo wataibuka washindi.muda si mrefu na dunia itashangaa

Mungu aliyetushindia kipindi Cha Magufuli kwenye hili la Corona atatushindia Tena na hao wazungu watajua Tanzania Ni nchi tofauti kuliko Nchi yeyote duniani pamoja na kuwa imo dunia hii hii.Watatutuamkia shikamoo.Tanzania sio ya kuyumbishwa na kitu kirogo Kama kichanjo pepo Cha Corona
 
Wakuu soon tamko la katibu wa bunge kwenda kwa wabunge wote wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa lazima wachanjwe la sivyo hawataruhusiwa kuingia bungeni mwenzi ujao .

Wabunge watatakiwa kuwasilisha kadi za chanjo kwa walinzi ili kuruhusiwa kuingia bungeni.

Wabunge wanatakiwa kuwa mifano ya jamii na chama Cha mapinduzi na kumuunga mkono mh. Rais ambaye tayari amesha chanjwa.

MY TAKE. Msimamamo wa gwajiboy na poleople utaonekana hasa wakigoma kuingia bungeni

USSR
Kwa sheria ipi? kinachotakiwa ni kupimwa pale langoni unapoingia mjengoni na si vinginevyo, kuchanja ni hiari.
 
Kwa lugha nyepesi ni kwamba Job analazimisha wabunge wachanje. Na kama patatokea Mbunge ambae hajachanja, basi Mbunge huyo hato ruhusiwa kushiriki ndani ya mbunge kwa kisingizio cha atawaambikiza wengine.
Anyway..... Wakubwa tumemuelewa vyema Mh 🔉 Job
Askofu rashidi achague moja, achanje aingie bungeni apate posho au asichanje abaki kwenye godown lake aendelee kufufua misukule.
 
H
Wakati kukiwa na mjadala wa baadhi ya wabunge kuhusu chanjo ya corona inayoendelea kutolewa nchini, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema pamoja na chanjo kuwa hiari, haimfanyi mtu kuwa na hiari ya kuambukiza wengine.

Kauli hiyo imekuja kukiwa tayari kuna wabunge walioonyesha wazi kupingana na mpango huo wa chanjo wakieleza kuhofia usalama wake kwa afya ya anayechanjwa.

Hata hivyo, juzi katika mahojiano yake na BBC, Rais Samia Suluhu Hassan aliendelea kuwahakikishia Watanzania kuwa chanjo hiyo ni salama, kinyume na hapo yeye asingehatarisha maisha yake kwa kuwa wa kwanza kuchanjwa

“Nashukuru sasa hivi Watanzania wengi wameelewa na wanaulizia chanjo, nalazimika kutuma maombi kwa nchi wahisani wanaosaidia chanjo waiangalie Tanzania wakati na sisi tukiendelea na mpango wa kununua chanjo kupitia nchi za Umoja wa Afrika (AU),” alisema Rais.

Pamoja na kauli hiyo ya Samia na uthibitisho wa wataalamu wa nchini na kimataifa, baadhi ya watu, wakiwemo wabunge kadhaa, wanaeleza waziwazi wasiwasi wao dhidi ya chanjo hiyo.

Akinukuliwa na kituo kimoja cha runinga, Spika Ndugai ambaye amekwishachanja, alisema, “tuna mabanda tayari yameshajengwa, wapo wataalamu na chanjo za kutosha zipo, kwa hiyo kila atakayekuja kwenye Bunge lijalo…(hakumalizia).

Aliongeza, “Ni hiari. “Ni hiari” alisema huku akionyesha ishara ya alama za funga usemi kwa vidole.

Kisha, Ndugai akasema, “...lakini hiari hii haikufanyi uwe na hiari ya kuchukua risk ya kuambukiza wengine.”

Mwananchi lilimtafuta Spika Ndugai jana ili aeleze alichokuwa anamaanisha, ambapo alifafanua zaidi kuwa vikao vya Bunge lijalo litakaloketi Agosti 30, ofisi yake itatoa mwelekeo huku akiwasisitiza wabunge wote kuchanja.

“Kuanzia Jumatatu (Agosti 16), wabunge wote watakuwepo (Dodoma) na uchanjaji utakuwa mkubwa. Tunaanza kwa kuhakikisha huduma zinakuwepo maana hata ukisema unachukua hatua, lazima huduma zipatikane, wenyewe ndiyo washindwe kwenda kuzipata. Natoa wito kwa wabunge wote kuchanja,” alisema Ndugai.

Miongoni mwa wabunge walioonyesha msimamo dhidi ya chanjo hiyo ni pamoja na aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, ambaye kwa sasa ni mbunge wa Kuteuliwa, Humprey Polepole.

“Ni muhimu sana watu wetu wakumbushwe tena na tena namna ya kujenga kinga ya mwili, ikiwemo elimu ya chakula na lishe bora kama hatua ya msingi ya kukabiliana na magonjwa na maambukizo yanayoweza kuzuiwa na kinga imara ya mwili. Kuchanja ni hiari lakini si kila kitu, mimi nitaimarisha kinga ya mwili na chanjo kwangu hapana,” aliandika Polepole kwenye ukurasa wake wa Instagram na kupongezwa na baadhi wafuasi wake, huku wengine wakimshukia.

Naye mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima mara kadhaa ametamka hadharani kuwa hatachanjwa chanjo hiyo kwa kuwa hana uhakika na usalama wake.

“Chanjo ni hiari anayependa aende, ila hapa hachanjwi mtu, lazima kondoo wangu niwalinde kwa namna yoyote ile, siko tayari kondoo wangu hata mmoja aangamie. Wajibu wa kulinda afya yako ni wako, huwezi kuwekewa kitu mwilini bila kutaka. Sichanjwi na sitachanjwa,” alisema Gwajima, ambaye ni askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.

Mbunge huyo, kinyume na kauli za kitaalamu, alisisitiza kuwa hadi sasa hakuna tafiti za kutosha zilizofanywa na wataalamu wa ndani kuhusu chanjo hiyo inayotolewa nchini na kuwataka wataalamu kuweka wazi kemikali zilizomo kwenye chanjo hiyo.

Matamshi hayo yamemwibua Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka akisema msimamo wa chama hicho unaweka wazi kuwa chanjo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani yao kwenye kipengele cha utoaji wa huduma za afya kwa Watanzania.

“Kwa hiyo sisi ukituuliza CCM msimamo wetu, tunasimama na Rais kwamba lazima tuwakinge Watanzania dhidi ya maradhi ya mlipuko, ikiwemo Uviko-19... tuna kanuni ya maadili, hii inawamulika viongozi wote ambao mienendo yao haiendi vizuri, ikionekana kuna mtu amekiuka kanuni, misingi ya chama ipo na haibagui, hatua zinaweza kuchukuliwa kwa yeyote,” alisema Shaka.
Hawa mbona wanajichanganya tu! Chanjo ni hiari! Lazima wabaki wa dawa ikitokea wabunge wengine wanageuka mazombie😜!
Ndugai uzivuke mpaka, ohooh😡!
 
Askofu rashidi achague moja, achanje aingie bungeni apate posho au asichanje abaki kwenye godown lake aendelee kufufua misukule.
Acha upungu ww, hachanjwi na bungeni anaingia vilevile! Si wanakaaga 1m apart!?
 
Back
Top Bottom