Ndugai: Nasisitiza hakuna cha bure lazima tuvuje jasho

Ndugai: Nasisitiza hakuna cha bure lazima tuvuje jasho

Anaweza akagombea uwenyekiti wa ccm mkoa au hata wilaya. Huko nako ni siasa.
Labda,ila utoke uspika,ubunge ukagombee tena uenyekiti Chama mkoa au wilaya,mbona kama ni kurudi chini?
 
Angetulia alinde heshima yake ndogo alionayo
Aaah wapi, kwani shida yake nini hapo Alichoongea!?

Ni uwongo kwamba hakuna cha dezo? Hata tukikopa bado sio cha bule, Ila tu ni maumivu kurudisha riba badala ya viongozi kuwa wabunifu na kubana matumizi ya hovyo, wao wanaona bora wakope ili tuu vitu vyao viwe pale pale na walipaji ni wewe unayeshupaza shingo kukataa uhalisia wa Mungu!
 
Sijaona alipotaja siasa
Ni kwa sababu mods wamebadilisha clip nilivyoiweka awali, ambapo ilikuwa inaanzia hapo hapo kwenye mada husika... mods hawajui watu hawana bundle wala muda wa kusikiliza video yote kwa yaliyo nje ya mada...
 
Awe muwazi, anajifichaficha kitu gani sasa, si yupo huru wakati huu, au bado anategemea kuteuliwa?
 
Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania amesisitiza kauli yake ya lazima tuwe watu wa kujitafutia kwa kujibana wenyewe kwa sababu hayupo jirani, ndugu ama shangazi wa kutupa vya bure.

Amesema hayo aliposhiriki Ibada ya ubarikio wa gari la Kanisa mojawapo la Anglikana huko mkoani Dodoma.
Mi nilidhani kayazungumzia bungeni, kumbe ni huko uchochoroni?
Hopeless kabisa.

Anashindwa nini kusimama na kuzungumza aliyonayo moyoni watu wamuelewe!
 
Kufanya kazi na kuheshimu matumizi mabaya ya pesa ni kitu muhimu sana katika maisha, Ndugai yupo sahihi hoja yake kwa level zote induvidually, nationally and internationally.
Hawa wanasiasa wote ni wanafiki na wa binafsi. Ndugai alikwenda India na mabillioni ya fedha za wananchi je hayo yalikuwa matumizi mazuri ya fedha za umma.?
Wanasema tu lakini hawaishi yale wanayohubiri!!
 
With all due respect, yeye mbona anashindwa kujitegemea, kachota pesa za "WANYONGE" kujitibu India.

Ikiwa yeye binafsi anashindwa kujitegemea basi na serikali (yake) itaachaje omba omba. Hakuna kitu kama hicho kujitegemea huo ni msemo tu ukiwa na maana usikae ukategemea kitakuja bila ya kuvuja jasho. Kitafute kwa nguvu zako zote, palipobakia utaomba ujaliziwe!
 
Yuko sahihi kabisa, hakuna alipokosea..

Hivi ni lini Tanzania iliwahi kujitegemea toka uhuru?.... Ni vizuri naye akayaishi anayoyasema.

Shida ya Watanzania ni wepesi sana kusema sema huku na kule lakini wenyewe hawayaishi wanayoyasema..

Utawala uliopita Ndugai alikuwa Spika wa Bunge, lakini utawala huo tunaambiwa ndio umekopa sana kwa miaka 10 tu...
 
Kama nawaona wana CCM (wenye nchi yao) wanajadili namna watakavyo mteka na kumng'oa makucha na meno kisha kumtupa bahari ya Hindi akiwa kwenye kiroba😱 CCM daima haipendi kuambiwa ukweli, wanataka kuboronga tu na kuliibia taifa, ukiwakosoa wanakuandalia magunia ya kukutupia baharini.
 
Nchi hii ni balaa, yaani mpaka wacheza sinema wapo 'mahali patakatifu.'
 
Kama nawaona wana CCM (wenye nchi yao) wanajadili namna watakavyo mteka na kumng'oa makucha na meno kisha kumtupa bahari ya Hindi akiwa kwenye kiroba😱 CCM daima haipendi kuambiwa ukweli, wanataka kuboronga tu na kuliibia taifa, ukiwakosoa wanakuandalia magunia ya kukutupia baharini.
Duh !!
 
Back
Top Bottom