Ndugai: Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uendelee, Dkt. Magufuli alishauriwa vibaya

Sioni sababu ya kujenga bandari ya bagamoyo wakati ya Dar haijafanya kazi at full capacity na bado inaweza kupanuliwa...otherwise hiyo bandari iwe ni long term project ambapo tutatumia pesa za ndani......tumeshachoka na mikataba ya kiwizi.
 
Nimekusikia na kukusoma leo mkuu 'NONIYANG'WAKA' -(kitu kama ndege wa mwaka?)!

Huu utekaji kumbe unayo historia ya siku nyingi? - 2000, 2005....!

Huyo Dr Lukanima ajihesabu kuwa na bahati sana, vinginevyo naye angekuwa ni historia wakati huu, kama ilivyo kwa akina Ben Saanane?

Lakini nimekusoama, na pengine nitaendelea kukusoma zaidi huko mbeleni.
 
weeeh! Jpm wakushauriwa au aliusoma mkataba.
 
Huu uzi wako umekaa kichonganishi na kinafiki unaleta habari za miaka ya nyuma hapa
 
Duh!! Aayaaa bwana inanibidi nicheke tu sa nitafanyaje ndugu zanguu
 
Lakini inapaswa tuwaze mbali, kwa faida ya vizazi vijavyo

 
Kula like boss Leo umetema madini Sana.
 
Yetu macho na masikio
Ohoo, yenu macho na masikio? Kila mwananchi ana wajibu wa kushiriki kwenye kutoa maoni na ikibidi kushinikiza kujua faida na hasara za miradi kama hii. Ukiwa mtazamaji hasara ni yako.
 
Mara Paap Magufuli anafufuka kama Yesu, Mzee Mantonya (aka Ndugai) ataficha wapi sura yake?
 
Hilo ndilo tatizo lingine kubwa la nchi hii. Kukosekana kwa bunge huru.
Mkuu Yoda,

Naomba nami nipandie kwenye hoja yako hii ya "kutokuwa na Bunge Huru."

Naomba sasa tushirikiane kuwastua hawa wabunge wa CCM waliomo kwenye Bunge hilo.

Mfadhiri wao mkuu, KAONDOKA; hakuna tena anayewashikilia wasiweze kulifanyia haki taifa hili.

Kitu cha kwanza wanachopaswa kukifanya ni kusafisha takataka zilizoko huko Bungeni kwao kwa kuwaondoa katika ngazi za uongozi wapuuzi kama huyu Ndugai.

Ndugai bila ya mbeleko wa mtu mwingine (kama Magufuli), hana nguvu ya kumuyumbisha mtu yeyote. Huyu wamkatae asiwaongoze, wamwondoe haraka.

Wakishafanya hivyo, hapo ndipo itatakiwa wafanye kazi za wananchi ambao kiuhakika hawakuwachagua kwa hiari zao. Hapo watakuwa wamelifanyia taifa lao haki, na wartastahili kupewa heshima.
 
Thank you
 
Hawa si ni ''wachapa kazi '' wa Magufuli lakini? Si ndio alikuwa anawaamini na kusema wana uzalendo? Maskini mzee wa watu hakujua alikuwa amezungungukwa na mbwa mwitu. Alidhani kina Lissu ndiyo maadui zake kumbe walikuwa wazalendo na hawa kina Ndungai ndiyo maadui wa Taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…