Ndugai: Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uendelee, Dkt. Magufuli alishauriwa vibaya

Kuna watu fahamu zinaanza kurudi- ile Kinga yako ya kutokushitakiwa ameshauriwa vibaya?
Hapa sio fahamu kurudi bali ni fahamu kuhama. Yaani Bagamoyo iendelezwe kwa sharti bandari Dat, Tanga, Mtwara etc zisiendelezwe na mwekezaji apewe lease 99 years. TZ inafaidika au inaliwa? Au aliyeuidhinisha huo mradi kabla kajipenyeza kwa hiyo kamati na Ndugai wake akijua wanamwogopa bado?
 
Wekeni mkataba wazi acheni uhuni wa presentation,sisi inatusaidia nini hiyo presentation?,mnaahidiana mipesa kutuibia sisi ili mpitishe mikataba ya wizi,huu ni upumbavu wa hali ya juu kabisa!
 
Namshangaa Dr Abas bado anaishi kwenye kivuli cha mzee Magu ashtuke mapema vingnevyo atavuna mabua Kama mihimil mikuu inabadil msimamo akae chonjo

Lakn hapa nawaza tu kidarasa la chekechea B KWEL ILE SAFARI YA WAZIR WA CHINA ILIKUWA YA HERI JAMANI HEBU TUISHI HUMU HUKU TUKITAFAKARI UJIO WA YULE WAZIRI
 
Mkuu haya mambo yalikuwa wazi kabisa. Ndungai ni mchumia tumbo tena kilaza wa kutupwa. Magufuli alikuwa anapenda watu kama hawa. Kichwani hamna kitu tumboni kuna tani mbili. Alidhani kina Lissu ni maadui kumbe walikuwa watu wema sana na wanataka kumsaidia afanye vizuri. Ohooo. mbona kila alichoasisi Magufuli kinasambaratika kwa kasi ya ajabu namna hii! Wale waliokuwa wanamsifia mchana kutwa ndiyo wamegeuka wapondaji. Haki watu wangekuwa wanarudi kutoka kaburini Magufuli asingeamini kinachotokea sasa hivi.
 
leo ndio nimeona wanasiasa hawawezi kuiona pepo kwa unafiki wao,huyu huyu ndugai aliwekwa pale na mzee leo anaongea haya kweli
Unga ulipokuwa mashariki, aliufuata kwa mapambio, ikiwemo kutaka kutekeleza harakati za kumwongezea mungu mtu muda. Leo unga unaelekea magharibi, anaufuata.
Kumbuka huyu ni mkuu wa mhimili. Poor Ndugai
 
Ndugai ungeoneka wa maana ungeshauri wkt jiwe lipo. Sasa hv hata fote bado mnagawana fito
 

Mama Samia kaa chonjo kuna kundi la wezi wanataka kurudi hewani kwa spidi ya mwewe hata arobaini haijaisha

Walifungiwa kwenye banda la mifugo sasa wanatoka kwa kasi kurudi kula mazao shambani

Wanaanza kukunjua mikucha yao mchana kweupe hata bila haya

Mzee Ndugai na uzee ule rushwa hata kweli anafanya decision kuwa mradi mzuri kwa kuangalia presentation ya mchina !!! Nimekubali CCM tunaingiza baadhi ya watu wenye upeo mdogo bungeni Ndugai akiwemo.
 
Watanzania tunapenda kuchonganisha sana, huo ndio ulikuwa msimamo wa Ndugai from day na alishatoa hiyo story yake ya China before.

Nani sahihi kati ya Ndugai na Magufuli wabunge badala ya kuburuzwa ku support au kupinga kitu ambacho awakijui in details wangeomba ushahidi utakaowasaidia na wao kuamua.

Ndugai apeleke proposal ya mradi bungeni ijadiliwe ili maamuzi ya wabunge yawe kutokana na information sahihi sio kutumia opinion zao kulazimisha agenda.
 
Du! Tujifunze kuweka akiba ya maneno, "mkono wa chuma" kafa leo Ndugai anamgeuka kweli wanafiki ndani ya CCM wapo wengi
 
Ila hasa watu jamani [emoji848]

Kitu inaitwa aibu huwa hawana asee

Kabla jogoo hajawika mara tatu ni raia zimemkana
 
Ndiyo maana tulikuwa tunalilia uchaguzi huru. Haya ni matokeo ya Magufuli kuokoteza mabaki huku na huko.
 
Du! Tujifunze kuweka akiba ya maneno, "mkono wa chuma" kafa leo Ndugai anamgeuka kweli wanafiki ndani ya CCM wapo wengi
Hao ndio watanzania wala usishangae, we jiulize una marafiki wangapi ambao ‘piga, uwa’ lazima wawepo.

Kama una marafiki ishirini basi mmoja au wawili tu siku nyumba yako ikijaa maji na mafuriko ndio watakufungulia mlango ujibanze na familia yako.

Tuna associates in life but not friends.
 
Ndio maana kwenye maisha yangu kamwe simtumaini wala kumtegemea mwanadamu mwenzangu.
Ina maana Ndugai amepata maono mengine mapya?
 
HApo kwenye bold....inaanzia kwenye familia, mtaani, makazini hadi TAiFA
Ajabu walioshauri mradi usijengwe ndiyo hao hao wanashauri mradi ujengwe.

Hiyo ndiyo rangi halisi yetu wabongo😇
 
Ni ngumu sana kuuwa legacy ya Magufuli na uzuri jamaa alikuwa anasema hadharani watanzania wanajua.


Ndiyo maana mpinga legacy ya Magufuli hatajibiwa na Magufuli wala watoto wa Magufuli mbali atajibiwa na watanzania.


Kama Ndugai anasema Magufuli alishauriwa vibaya itabidi atueleze huo mkataba unasemaje tofauti na aliyosema Magufuli.

Watakaohoji haya ni watanzania.


Ni kama waliojaribu kuuwa legacy ya Nyerere huwa wanatapa upinzani mkali hadi leo wakati Nyerere alishafariki zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Watu huwa wanarejea hotuba tu.

Maneno huiishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…