Ndugu yako akisoma hizo course jitahidi kumuandalia bodaboda kama backup

Hiyo 6 kuajiriwa na kujiajiri rahisi Sana Kama umechangamka kichwani na unajichanganya na watu mikoa ya kibiashara mfano Dar, Mwanza, Arusha, Dodoma, ...
Namba 7 fursa za ajira na kujiajiri zipo nyingi.
Kifupi akili yako tu na kujituma.
Kweli akichanganya na digital marketing anakua mzuri sana
 
Ni kweli lakini nimesema akiisoma vizuri na akaielewa, akijitahidi kupitia source mbalimbali kwasababu lecture wa kibongo jau sana, lakini asipokomaa na kusoma Kwa bidii na kujiongeza aaah lazima kuchoma movie imuhusu.
Sasa hasipo ielewa atafaulu vipi.
 
Sasa hasipo ielewa atafaulu vipi.
Mkuu computer science ni zaidi ya darasani Ili mwanafunzi awe programmer (full stack developer) lazima ajue fronted na backend lazima ajue language zisizopungua 10, HTML, CSS, JAVASCRIPT, JAVA,RUST,GO,PHP, PYTHON, SQL N.K vyuo vyetu havikufundishi wewe kujua yote hayo vinakupa basic tu, data science lazima ajue SQL, python, power bi, advanced Excell, machine learning chuo Gani kinachofundisha complete Kwa vitendo ? Cyber security napo mambo ni mengi mno unaona?
 
Mimi degree yangu ya kwanza ni Uhasibu,nina CPA lakini kazi nayofanya ni HR na mshahara wangu ni zaidi ya 28milion kwa mwezi,kwa hiyo unaposema HR haina maisha sijui haina kazi nakushangaa sana.
Wakati nikiwa chuo sikutegemea kabisa kama nitakuja kuwa HR,ila baada ya kuingia sokoni huku Corporate nilikuja gundua kazi za siasa/kazi za kuonhea ndo zinalipa huku maofisini...yaani kuna Mainjinia sijui madokta huwa nawacheki mpaka nachekea chooni maana sio kwa hali yao ngumu,ingawa sio wote
 
Tatizo wengi wa vijana wanasoma Kwa kufuata mkumbo yaani hawajui wanachokitaka kabisa mfano walimu wengi wamesoma hiyo kozi kisa kupata mkopo mkubwa au uhakika wa kazi, what a fuc*king nonsense...Yaani kama mtu kamaliza Hadi form six na hajui anataka nini sasa huyu kweli si Hana chake maana atapoteza muda weee Hadi kushtuka tayari ana familia na umri umeenda...Mimi Nadhani Kwanza tuwafundishe vijana wetu kujitegemea kiakili na kuwakomaza Kwanza kifikra, halafu tunawaacha wachague wenyewe wanachotaka watajua nini cha kufanya ili kutoboa, maana hata umchagulie kozi nzuri still bado Hana uhakika wa kupata kazi, kwanini tusiwajengee vijana wetu uwezo wa kujiajiri wenyewe Kwa kile wanachopenda na sio kufuata hot passion of the day?
 
Computer science unasubiri ufundishwe kwa vitendo kweli? Yaan kuna tutorials theory na practical kibao YouTube, kuna Udemy bila kusahau huko Torents kuna tutorials kibao, unacho hitaji PC na software basi,ambazo ni free. Broo best coder duniani ni wale self learner.Halafu code sio lazima ujue language zote, unaweza ukajua hata tatu, basi zikakuingizia hela ndefu tu,achana na akili ya kutaka kufundishwa kila kitu darasani,halafu ukimaster language moja nyingine kuzielewa ni easy,ukijua function kwenye C++ msingi wake ndio ule ule unautumia kwenye Python, Java kinacho tofautiana ni syntax.Online kuna materials kibao ni wewe kuwa tayari, Udemy kuna course nzima unaisoma kwa elfu 30 tu, wewe upo dunia ipi hebu grow up acha lawama.
 
Hahaha hicho ulichokiandika kimenikuta Mimi 100%
 
No. 2, 4, 6, 8 na 9 kwa ulimwengu wa sasa ni kozi nzuri za kijasiriamali kama unajua kujiongeza
 
Mimi broo sio developer ni data engeneer, but nimekuelewa mno binafsi GitHub na torrents ndio zinanisaidia.
 
Unachokisema kina ukweli ndani yake mkuu. Ukizingatia Degree imekuwa kitu cha kawaida sana mtaani kazi hakuna ila watu wana vyeti ndani.Binafsi nilipiga BAF nikaona haina tija safari ya kuitafuta cpa sio mchezo bora niwahi kujiajiri kwenye logistics
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…