Ndugu zangu Kuna upendo kweli hapa?

Mahari sio mahali huwa hailipwi yote, tunapunguza tu maisha yanaendelea tunamaliza mahari ikitokea mke kafariki tu otherwise hadi maisha yanaisha bado tunatunza deni ili kuwe na sababu ya kuwasiliana na wakwe! Kama mke ndo anashinikiza yasiyomuhusu kuna tatizo hapo na huenda ana cha juu
 
 
 
Nina swali kwa wale wazee wa kuoa bikira,,,ivi kwa mwanamke kama huyo hatakama ni bikira anafaa kuolewa!??????.........
 
Ila Binti ana dharau, imagine anamwambia jamaa amwambie mama ake amtafutie mke 😂😂😂. Jamaa Kai hukulia poa hii kauli ila ni nzito saana
Sijui hata akili ya kuanzisha uzi kaitoa wapi!! Hiyo ni bonge ya red flag 🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Sawa mkuu shukrani Tayari nimepiga chini takataka hii
Hongera sana kama umefikia uamuzi huo,ameonyesha redflag mapema mno,tatizo huwa tunadharau kufuatilia hizi ishara

Nilifikir ungekamatika na bikira kama baadhi ya wajinga humu wanavyoziabudu,,haya umemtoa bikira na bado anataka muachane,je hapo bikira yake ina manufaa gani?

Mwanamke akikupenda atakuwa wa kwanza kukutafutia unafuu wewe mwanaume wake ili mtimize lengo lenu,lkn huyo ndio kwanza anakuwa kikwazo kwako

Halafu ogopa mwanamke anayeweka demand ili umfanyie jambo fulani,basi tambua ungetimiza hili takwa lake,ungekutana na demand nyingine nyingi tu

Kwanini baadhi ya wanaume wanapoteza mamlaka kwa wake zao? Ni kutokana na mambo kama haya,leo atataka hili kesho lile na mwisho wa siku yeye ndio anakuwa juu yako

Kama kweli umempiga chini hongera ila kama unatuongopea ili uonekane una msimamo hapa juu ya jukwaa,hilo ni tatizo lako na utajifunza in a hard way
 
Shukran sana kamanda
 
 
Hongera sana expert wangu,,,,ebu chek jibu lake eti "sawa"

Angekuwa anakupenda kweli lazima angekuwa kwenye mshtuko baada ya hiyo text yako

Hongera sana kwa kuligundua hili mapema,hata akijirudi baada ya siku siku chache zijazo,huyu sio mtu wa kuanza nae maisha trust me

Utampata mwingine tu expert wangu
 
Iyo 1 milion subiri jumapili tafuta odds 10 i swear utakuja kunishukuru
Apo ushalipa mahali na mtaji milion 7 mfukoni
 
Mkuu naomba kukuweka sawa.
Hiyo sms ndefu ni sms yake yeye baada ya mm kumuambia ukweli kuwa simuhitaji mana Kuna siku nilimwambia kama Mungu amepanga tuwe wote basi atatupa majibu yeye akajibu hiyo Mimi nikajibu sawa.
 
Mkuu naomba kukuweka sawa.
Hiyo sms ndefu ni sms yake yeye baada ya mm kumuambia ukweli kuwa simuhitaji mana Kuna siku nilimwambia kama Mungu amepanga tuwe wote basi atatupa majibu yeye akajibu hiyo Mimi nikajibu sawa.
Asante kwa kuniweka sawa,shukran
 
K
Kataa ndoa bro tafuta pesa hivyo viumbe havieleweki
 
2.6 M ni fair sana!
 
Sioni future yoyote nzuri hapo, kama mwanaume niliyeona mengi nakushauri kaza moyo mwanangu huenda ukapata mtu sahihi mnaendana hapo baadae, nikushauri kitu, kitu chochote kinachohusiana na Mali au zawadi kama vile pesa nk ni vizuri kufungua milango yako yote ya fahamu kuweza kujua upande uliojificha wa mwenzako....mambo ya pesa yakiingia ni rahisi kujua usichokijua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…