Ndugu zangu upande wa baba wanainua vita kali juu yangu

Kama ni Mkristo nenda kanisani Kaombe misa hata isomwe siku tatu mfululizo wote watatawanyika maana huna baya na MTU, sijui kwa imani nyingine wanafanyaje.
Asante mno mkuu.ubarikiwe
 
Nimerudia kusoma uzi mara tatu nione sehem ndugu zako walipokufanyia ubaya sijaona, punguza kuwafikiria watu vibaya umejihami kiasi kwamba kila mtu unamuona mbaya
Sawa mkuu hakuna shida.asante
 
Nafikiri niwapuuzie tu mkuu.kuwaleta pamoja sidhani Kama itatokea
 
Asante sana.
Ninashukuru kwa ushuhuda pia
 
I’m a woman mkuu.

Mimi nitakuwa wa kwanza kuwa na maisha marefu.

Hallelujah.

Nakushukuru sana kwa comment yako mkuu
 
Kwanza pole sana Mkuu, ndio Walimwengu walivyo na ushauri wangu ni huu.
1. Acha kuwa na roho ya huruma wazingatie watu wanaokuhusu
2. Wakali mwingine punguza sana hofu ya mambo mabaya kukutokea
3. Ishi vizuri kwa kuzingatia kanuni za imani yako.
4. Punguza kuwaogopa maana unaitengenezea akili yako hali kuwaona ni kama adui zako.
5. Imani yako ifuate kwa asilimia zote iwe ni Kanisani au Msikitini
6. Wapende Baba na Mama yako maana has ndio miungu yako hapa duniani hao ndugu wa Baba yako achana nao ikiwezekana wapige marufuku na wakizidi kukughasi wachukulie hatua za kisheria.
Nikutakie wakati mzuri japo kuna mambo mengi hujafunguka na ndio maana nimeshindwa kutokea ushauri wa moja kwa moja
 
Kumbe wanakuombea, Mimi nikajua labda kuna mtu amekukata mkono au Miguu hapo lingekuwa suala lingine, ndugu yangu kuombewa mabaya siyo wewe peke yako unayepitia hiyo Hali.


Wewe mtegemee Mungu na endelea kufanya lililo HAKI , pengine Mungu amekubariki basi usitumie pia uwezo wako kuadhibu wengine maana huwa ina backfire, ugomvi WA wazazi achana nao wanajijua wenyewe, huenda kuna namna wazazi wako au Baba alikwaruzana na ndugu zake , sasa badala ya yeye kurudi kwa ndugu zake kuomba msamaha analazimisha ionekane kuwa anaonewa, hiyo haipedezi na ugomvi hautokoma.


Vita ya wazazi waachie wenyewe usichochee Moto, unachoweza kufanya ni kuwaunganisha kupitia viongozi wa Imani either Masheikh au wachungaji waone namna gani ya kuondoa tofauti zao ili maisha yaendelee.


Maisha ni mafupi Sana kuendelea kuishi kwa chuki .
 
Sasa kwanini nimeleta uzi huu ni kuwa ile vita iliyoanzishwa kwa wazazi imenigeukia mimi. Baba wadogo na mashangazi wananiombea maanguko, magonjwa hatarishi na hata kifo jamani!
[emoji3064][emoji3064][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…