Ndugu zangu upande wa baba wanainua vita kali juu yangu

Wapotezee fanya kama vile hauna ndugu maisha yaendelee kipenzi changu
 
Kimbia mkuu, hao wamepanga kukumaliza.
 
Wafungie vioo wanakusaidia nin kwenye maisha yako?
Huyu jamaa atakuwa mtu wa kusikiliza sana na kufuatilia mambo ya nyumbani kwao kama sio kijijini kwao. Kwa hiyo kila kinachosemwa anachukua. Hivi ukifunga vioo ukadeal tu na wazazi wako na hao wazazi ukawaachia wenyewe mambo ya kijijini kwao, utasikia wapi hizo shida?

Ndio tunavyofanya wengine, ujinga ujinga wa kijijini hauna nafasi na hakuna kuruhusu informers. Watasema wee wanakuta no reactions kwa sababu sina habari kabisa. Sasa shida kama hizi zinawakuta watu wapo mjini, lakini sikio lipo kijijini
 
Chakorii zingatia hii.
 
Halafu jingine Chakorii inaonekana unapenda sana vita vya maneno kwa sababu umejipata nakushauri kama Kaka/Mdogo wako achana nao usijibizane nao maana wao wapo wengi na wewe uko pekee yako huwawezi watakuvuruga sana na utajikuta unafanya mambo yatakayo kugharimu wewe mwenyewe. Wapotezee kabisa na usijibizane nao. Control your tongue 😝
 
Anaonekana anapenda sana maneno na majibizano huyu kwa sababu ameshakuwa somebody na hii itam cost yeye mwenyewe
 
Kuna muda ndugu huwa wanazingua kinoma yani !
Hapo huna kosa lolote ukute wanavoona wivu tu kwani walifurahia anguko na utengano wa wazazi wako na hawapendi mafanikio yako!
Ubarikiwe sana hakuna kipindi huwa napata amani kama kipindi ambapo nawajali wazazi!

Cc Smart911
 
Huyu kayakanyaga Mwenyewe kwa sababu ianonekana anapenda kurushiana nao maneno lazima wamvuruge tu. Mpaka anakuja humu washamvuruga abadirike aache kujibizana nao hiyo ndio last solution's
 
Manyanza sio maneno ya kuambiwa mkuu.nimemsikia mwenyewe kwa masikio yangu sijasimuliwa na akawataja ndugu zake wengine ambao wako pamoja nae.

Naweza kusema kuwa ni Mungu ndie aliyesababisha nimsikie kwa kinywa chake maana nisingeamini kama ningesimuliwa na mtu.

Nilikuwa nawapanda wote
 
Huyu kayakanyaga Mwenyewe kwa sababu ianonekana anapenda kurushiana nao maneno lazima wamvuruge tu. Mpaka anakuja humu washamvuruga abadirike aache kujibizana nao hiyo ndio last solution's
Sasa ndugu yangu naona unaanza kunibandikia maneno kinywani.ikikupendeza uache kuniwekea maneno kinywani si ndio mkuu.shukrani sana
 
Pole kama umekwazika na sio dhamiraĺ yangu kufanya hivyo.
Sijakwazika mkuu isipokuwa niliona unavyoandika ni kama tunaishi wote kila siku so ukawa unajua fika Napenda kurushiana maneno.

naona ulikuwa umeng’anga’ana na tuhuma tu mkuu

Nashukuru kwa ushauri pia
 




Hapo mkuu, hakuna VITA yoyote Ila kilichopo ni hao ndugu zako kuwa negative na wewe kuwa negative


Kuhusu kukuombea mabaya.

Kwanza unabidi kujua hakuna jambo lolote linaweza kukupata baya linalotokana na maombi mabaya.

Nini ufanye.

Hakikisha unakuwa positive usimchuke MTU yeyote , maana unavyowachukia watu maana yake wewe ndo utaishi maisha magumu ,na ukiwaombea mabaya hayo mabaya yatakupata wewe.

Mbinu za kutumia.

Wapende wazazi wako wote na ndugu zako na wasaidie unapoweza , na pia wana ukoo wako ambao unahisi wapo negative tumia kanuni inaitwa "Love from a distance" wapende Ila kaa nao mbali.

Kuhusu kurogwa.!

Kurogwa ni level ndogo Sana kiroho na uchawi hauna nguvu yoyote.

Unafanyaje usirogwe.?

Hakikisha unakuwa innocence , (Unyong'ofu ) usikubali kuwa na kinyongo ,chuki, wivu, n.k

Na mwisho.

Jifunze kufanya Gratitude jambo lolote linalokutokea shukuru ukishukuru unakuwa unaruhusu nguvu chanya au nishati chanya kuyatawala maisha yako.

Zingatia Detachment and Attachment unapoona jambo linakuumiza lisamehe na lishukuru detachment na litaondoka na utakuwa na Amani Sana.

Maombi Prayer /rituals
Unapoomba waombee watu wote kuanzia hao unaohisi hawakupendi waombee Amani na maisha yenye Afya na Mungu awajaze hekima hii itakusaidia Sana.


Elimu, Exposure

Fahamu na. elewa watu wengi hasa watu weusi hawajawa civilized hivyo habari mbaya zako ndo habari nzuri kwao na hii sio kwako ni nchi nzima Hi yo unapofanya mambo mazuri jitahidi MTU asijue ikiwemo wazazi wako.


All the best.
 
Sijakwazika mkuu isipokuwa niliona unavyoandika ni kama tunaishi wote kila siku so ukawa unajua fika Napenda kurushiana maneno.

naona ulikuwa umeng’anga’ana na tuhuma tu mkuu

Nashukuru kwa ushauri pia
Leo jumatatu kuna Mwanasaikolojia TBC Taifa ana kipindi kuanzia saa 4 na robo usiku mpaka saa 6 msikilize utapata namna ya kudili na hii situation yako
 
Mkuu nilikuwa ninasubiria comment yako sana.

Ninakushukuru mno.
Nitafanya kilichosahihi.ubarikiwe🫶🫶🫶
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…