Ukimwi usikie tu kwa watu... lisikukute
Kuna wakati fulani, miaka kadhaa nyuma, kipindi cha utawala wa mkwere awamu ya pili, nikiwa na miaka 18 Tu... sintokuja sahau maishani kwangu
Nakumbuka ile siku, kuna bimkubwa mmoja nilimtania tu kuhusu game...mimi nikijua n utani kumbe kwa bimkubwa alidhan nilimaanisha, muda tulio kubaliana akafika eneo la tukio.. sina hili wala lile naelekea zangu ghetto mara huyu hapa... kile kiwewe, ndio first time ilikua, ghetto kuna condom box zima wajomba walinunua, nikaogopa kuchua hata ka pact kamoja.. nikaenda mchampa peku viwil... first time experience, nikatoka pale mwepes
sasa kimbembe kama masaa mawili baada ya tukio, alinipiga simu akaniuliza "Hivi Dan ulivyokua unafanya vile ulikua unategemea nini" moyo ukapiga paa.. nikauliza, G, unamaanisha nini, wacha anipe jibu konki "Subiri muda ukifika utanielewa" akakata simu akazima... mai weee, nikajua nimeenda na maji... yaan mara moja tu nakufa hivi hivi... Dan Pol nimekufa kizembe namna hii, kweli mgambo n mgambo... nililia acha tu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] nilisoma kila kitu kuhusu ukimwi, nikasubir muda ukafika(miez mitatu) kwenda kupima naogopa, huku na huko nikapata demu, condom hataki, nikiwa nafikiria cha kumjibu akaniambia unafikiria nn, kwa lugha nyingne namaanisha tukapime... maiweeee, nilikua mdogo ghafla, ilikua jumapili, akasema twende juma nne nikasema hapana twende alhamis, lengo nipate mda wa kuji cancel kidogo [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] achana na hii kitu bana
siku imefika, kutoka hospital ilipo na nilipokua na naishi ni mwendo wa dakika 10.. it was the longest journey of my life, nikifika tukauliza sehemu ya kupima, tukapelekwa kwenye chumba namba 10....ilikua jua la utosi ila nilikua nina vibrate balaa.. mbaya zaid nilikaa usawa wa dirisha la dawa, nilipoona watu wanaokuja kuchukua dawa... nilihisi kufa kufa tu, hawafanani hata kidogo na waathirika... muda ukawadia tukapima, ile hali niliyokua nayo ilikua haielezek, yaan kama mtu angenishtua kwa kupiga tu hata makofi, nahisi ningekufa
Neno nalokumbuka kutoka kwa yule nesi kauli yake yake ya KWASASA NYIE WOTE NI WAZIMA, akashaur shaur pale sikusikia neno hata moja ... ile tumeruhusiwa kutoka tu nilimshika mkono dem wangu mbio, kama kakosea asijesema rudin hapa nimekosea kusoma
Tokea siku hiyo mpaka leo hii, hata mwanamke awe mzuri vipi, kama sina condom na hatujapima, simgus kwa namna yeyote ile, hata nikilala kitanda kimoja na avue nguo zote.. sigusi
Sent using
Jamii Forums mobile app