Ndugulile: Kama hauna uhakika na taarifa usipost, usiretweet, ku-like wala kukomenti

Bongo muda mwingine sijui huwa wanafikiri kwa kutumia miguu hoja zao ni kiboko hata mateja hawawezi kutoa matamshi ya hovyo kama haya ya kuwakamata wasioweka umeme na kununua magari haijapoa imekuja ya ku like...
 
Haya mambo yote yaenfanayo na Sheria za uhalifu mtandao ya 2015 hayatekelezeki. Hiki alichoongea Dr Ndugulile ndiyo hakiwezekani kabisa Ila ni tisha toto tu.

Kweli Serikali inaweza kamata watu watatu au 4 lakini siyo rahisi kuwa tia hatiani kwa Sheria zetu. Kuna mwanafalsafa alisema kwa kiingereza;

“The closer is the collapse of an empire, the crazier are its laws.”

au kwa Latin

" Quod propius est ruina imperium, et sunt leges pertoccavi. "

Hizi ni dalili kama alizokabikiwa nazo Nebuchadnezzar kabla dola yake haijasambaratika
 
Nafikili Kama kinachofanyika huko hawapendi kuona au kusikia, wafunge account zao,Kama mh president Kinyatta,vinginevyo kitakua kituko kingine
 
Kashindwa kupambana na makampuni ya simu, kabaki kubweka tuu kama kafungiwa gatini
 
Hizi nguvu zote wangeziweka kwenye kupambana na korona badala ya kujitahidi kuificha. Maradhi hayafichiki. Kwenye yale maombi wanayotaka tuombe hatutaitaja korona tu iondoke bali na wanaojitahidi kuificha tutapeleka shauri.nao waondoke.

Haiwezekani sisi tunapambana kufyeka vichaka adui awe peupe wengine wanajitajidi kumficha. Sasa tutakichoma kichaka na wenyewe wakiwa humohumo.
 
Mjinga sana huyu Ndugulile.
 
Watasababisha tuwe na email account zaidi ya moja na kurejister mitandao hiyo kwa emails tofauti na twende anonymous zaidi!
 
Sheria ya matumizi ya mtandao iko wazi. Anayesambaza na ku like habari za upuuzi, jeshi la polisi litamkamata na kumfikisha mahakamani ambako atahukumiwa kwenda kunyea debe miaka mitano. Dr Ndungulile anawakumbusha kutii hiyo sheria. Kama unabisha jeshi la polisi litaanza na wewe pamoja na wachache wanao ku support ili uwe mfano kwa wengine.
 
Kiufupi,,keep kwayat
 
Kazi ipo !
 
Wewe ni wa kuhurumiwa tu
 
Kazi ipo !

Dalili zote Mkuu tunaelekea huko, wanataka kudhibiti majukwaa yote.

Walianza na majukwaa ya siasa, wakaenda vyombo vya habari /media, vyama vya kitaaluma, vyuo vikuu wameshamaliza.

Sasa wanatafuta kuungwa mkono kwa vitisho ndani ya nyumba za ibada.

Tundu Lissu alituasa wakimalizana na "sisi", wakakwenda na sehemu zingine kujaribu kuwanyamazisha na kuwatisha.
 
Mwisho wa ubaya ni aibu, Ndugulile anatapatapa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…