Uchaguzi 2020 NEC yafafanua Timu za Kampeni baada ya Tundu Lissu kuhoji ushiriki wa Kassim Majaliwa katika kuzunguka nchi nzima

Naam sisi wenye shida naye ofisini tunashindwa kumuona kupata ufumbuzi wa matatizo yetu kwa sababu yuko kwenye kampeni kumpigania mtu mwingine.

Kila tukienda tunaambiwa subiri waziri mkuu arudi ofisini, yuko kwenye kampeni za kumnadi Magufuli
Kwa hiyo wenye shida na rais nao wasemeje?
 

Walimteka ili apite bila kupingwa
 
Sheria hazimruhusu waziri, mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya kupiga kampeni kwa chama chochote.

Tuliza kichwa utaelewa.
Weka hapa hiyo sheria,
Kama ni hivyo basi hata wagombea ubunge ambao ni mawaziri wasifanye kampeni
 
Rais yeye ni mgombea anatafuta kura zake, na kanuni zimempa leeway kubwa kuliko mawaziri, wakuu wa mikoa na watendaji wengine wa serikali
Waziri mkuu ni mgombea ubunge kule kwake!

Sasa huko kukosekana kwake ofisini kunakuwepo akiwa kwenye majimbo mengine tu?

Alafu unaposema waziri anakosekana ofisini si kuna wasaidizi? Suala linalohitaji maamuzi yake si simu zipo au unafikiri bado tupo miaka ya 1930?

Hukuona kipindi cha corona watu wanafanyia kazi majumbani? Na nchi nyingine mpaka leo watu wanafanyia kazi nyumbani. Waziri mkuu popote anapokuwa ni ofisi.
 
Walimteka ili apite bila kupingwa
Sanduku la kura litatoa majibu, maana kama kuna wapiga kura 700, na alitegemea 600 baada ya kuwa peke yake, basi atapata 100, hapo ndo ajiulize kama anapendwa hizo 600 zilienda wapi.
 
Kama ni timu na iliwasilishwa tume siku 2 kabla ya uteuzi, kwa nini haikuwekwa kwenye ratiba ya Tume? Na kwa sasa hiyo timu inatumia ratiba gani?
Unaweza kuwek kifungu cha sheria anayokiuk waziri mkuu?
 
So

Si umeambiwa ni timu ya kampeni au hjaelewa
Team maana yake ni kuwa pamoja, uliona Wapi Kagere, Chama, Boko na wachezaji wingine wa Simba Wakicheza kivyao, mfano ratiba ya ligi kuu ni mchezo kati ya Simba vs Ruvu JKT uwanja wa Taifa halafu wachezaji hao peke yao bila hata kocha wao wakacheza na Kagera Sugar Kaitaba Bukoba kwa muda ule ule kwa jina la Simba? Kama Majaliwa yuko kwenye team ya Magufuli ni lazima aambatane naye kwenye msafara, siyo Mmoja anaendesha kampeni Dodoma, Mwingine Ruvuma
 
Team maana yake ni kuwa pamoja, uliona Wapi Kagere, Chama, Boko na wachezaji wingine wa Simba Wakicheza kivyao, mfano ratiba ya ligi kuu ni mchezo kati ya Simba vs Ruvu JKT uwanja wa Taifa halafu wachezaji hao peke yao bila hata kocha wao wakacheza na Kagera Sugar Kaitaba Bukoba kwa muda ule ule kwa jina la Simba? Kama Majaliwa yuko kwenye team ya Magufuli ni lazima aambatane naye kwenye msafara, siyo Mmoja anaendesha kampeni Dodoma, Mwingine Ruvuma
 

Kuna baadhi ya mambo hayaamuliwi na wasaidizi bali yeye mwenyewe.

Akiwa hayupo kwenye kituo cha kazi lazima ziwepo sababu za msingi za yeye kutokuwepo kwenye kituo cha kazi tena kwa ruhusa maalum ya kiprotokali za kazi kama vile.

1. Awe yuko jimboni kwake anatafuta kura maana akienda jimboni ataondoka ofisini kwa ruhusa maalum.

2. Anaumwa yuko hospitali atakuwa na ruhusa maalum
3. Ana likizo atakuwa na ruhusa maalum

Na vitu vya aina hiyo ambavyo vinatambulika kisheria

Siyo eti hayuko ofisini kwa sababu yupo kwenye kampeni za kumnadi John Magufuli, ni barua gani ya kikazi utaandika kuwa hauko kazini kwa ajili ya kumnadi Magufuli!!!

Waziri mkuu anatuibia muda wetu wa kazi.
 
Mbona watu wanalazimisha kwamba tuamini Lissu anajua sheria zote! Hii mbona hakuijua? Au alikuwa busy (bize)! Au hazijui sheria ipasavyo.
 
Ina maana bingwa wa sheria hakuzisoma kanuni hizo. Uzuri amejaliwa kukosa aibu.
Japo mengi mnakosa kuelewa hadi hapo unashindwa kuelewa? Je majaliwa ni mgombea ubunge nani amemruhusu azunguke majimbo ya wenzake ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…