Uchaguzi 2020 NEC yafafanua Timu za Kampeni baada ya Tundu Lissu kuhoji ushiriki wa Kassim Majaliwa katika kuzunguka nchi nzima

Waziri mkuu anatumia rasilimali za kiserikali kufanya kampeni kwa ajili ya Magufuli

Misafara anayotembea nayo Kassim Majaliwa kwenye kampeni ikiwemo walinzi, muda, madereva vyote hivyo ni mali ya serikali havipaswi kutumika kwa ajili ya kumkampenia Mtu maana vinampa mgombea wake unfair advantage dhidi ya wagombea wengine na wote ni Watanzania!
Unaweza kuthibitisha kama ni mali ya selikali?

Vipi kama ccm ndio inatoa hela za vyote hivyo?
 
Ratiba zipi?

Hivi hizo ratiba zinaonesha hadi majina ya wana timu ya kampeni?

Hivi Majaliwa akiwa Kagera na Magu yuko Iringa, Majaliwa akisema niko kwenye timu na ratiba ya mgimbea ubunge wa jimbo husika utakuwa na la kuhoji?
Kwenye jimbo pia kuna timu, kwahiyo Majaliwa yuko kwenye timu ya majimbo yote?
 
Kwani kuna shida?

Ndio maana tunawambia wengi humu mmeanza kufuatilia siasa baada ya Lisu kutoka ubelgiji.

Lowasa alikuwa na kampeni ya nguvu sana 2015 kuna timu zilijigawa kila kanda.

Mbowe, Lema na kina Msigwa wote waliacha majimbo yao na kuzunguka huku na huko kumnadi EL.
.
Safari hii chadema haina hela ndio maana unaona Lisu kabaki ana hangaika peke yake, usifikiri anafuata kanuni za uchaguzi hapana ni hela hana, angekuwa nazo kama EL 2015 ungeona timu za kampeni kila kona.
 
Unaweza kuthibitisha kama ni mali ya selikali?

Vipi kama ccm ndio inatoa hela za vyote hivyo?

CCM ndo inampa rasilimali MUDA?

Waziri mkuu badala ya kutumia muda wake ofisini kufanya mambo ya nchi tunayomlipa mshahara kwayo kila mwezi, yeye yupo anatuibia muda wetu wa kazi kufanya mambo ya chama!

Hata kama CCM ndo ingekuwa inamuwezesha kwa kumgharamia, alipaswa kufanya mambo ya chama nje ya muda wa kazi!

Wananchi wanashindwa kupata huduma za waziri mkuu kwa sababu yuko kwenye kampeni za siasa tena za mtu mwingine!
 
CCM ndo inampa rasilimali MUDA?

Waziri mkuu badala ya kutumia muda wake ofisini kufanya mambo ya nchi tunayomlipa mshahara kila mwezi, yeye yupo anatuibia muda wetu wa kazi kufanya mambo ya chama!

Hata kama CCM ndo ingekuwa inamuwezesha kwa kumgharamia, alipaswa kufanya mambo ya chama nje ya muda wa kazi!

Wananchi wanashindwa kupata huduma za waziri mkuu kwa sababu yuko kwenye kampeni za siasa tena za mtu mwingine!
Kwahiyo hata Magu nae anapaswa kukaa ofisini kufanya shughuli za selikali aachane na kampeni azifanye muda wa ziada?
 
Kwani kuna shida?

Ndio maana tunawambia wengi humu mmeanza kufuatilia siasa baada ya Lisu kutoka ubelgiji.

Lowasa alikuwa na kampeni ya nguvu sana 2015 kuna timu zilijigawa kila kanda.

Mbowe, Lema na kina Msigwa wote waliacha majimbo yao na kuzunguka huku na huko kumnadi EL.
.
Safari hii chadema haina hela ndio maana unaona Lisu kabaki ana hangaika peke yake, usifikiri anafuata kanuni za uchaguzi hapana ni hela hana, angekuwa nazo kama EL 2015 ungeona timu za kampeni kila kona.
Naona unajitahidi sana kutetea usichokijua! Usingechangia chochote kwenye uzi huu
 
NEC: TIMU ZA KAMPENI

Timu ya kampeni ni kundi la watu lililoundwa na mgombea wakati wa mchakato wa uteuzi au uchaguzi kwa lengo la kumnadi na kumsaidia mgombea huyo katika kampeni za uchaguzi (Kifungu 7(3)).

Mgombea atakayekuwa na timu ya kampeni anapaswa kuwasilisha majina ya watu wanaounda timu yake ya kampeni siku mbili kabla ya kuanza kwa mchakato wa uteuzi au siku saba baada ya uteuzi, kama ifuatavyo:

1.Mgombea Urais anapaswa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi hamsini (50). (Kanuni 17(1)(a))

2.Mgombea ubunge katika eneo la Tanzania Bara anapaswa kuwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi ishirini (20). (Kanuni 17(1)(b));
We ndo umetoa ufafanuzi au tume. Basi kama ni tume Magufuli ameteua wasiofaa kwenye tume
 
Kwahiyo hata Magu nae anapaswa kukaa ofisini kufanya shughuli za selikali aachane na kampeni azifanye muda wa ziada?

Magu na Mama Samia ndo wagombea wenyewe wanasaka kura nchi nzima, hawa wana exception.

Sasa kwenye hierarchy ya serikali Waziri mkuu ni wa tatu, Sasa kama wale wawili wako Field kusaka kura, huyu wa tatu kwa nini asitulie ofisini kuendesha nchi ukizingatia kuwa anachokifanya hajitafutii yeye kura anatafutia wengine
 
Ndio sheria inavyosema au unataka iwe hivyo kwa busara zako tu?

Je, kuna shughuli yeyote ya selikali imeathirika kiutendaji sababu ya Waziri mkuu kuwa kwenye kampeni?
 
NEC: TIMU ZA KAMPENI

Timu ya kampeni ni kundi la watu lililoundwa na mgombea wakati wa mchakato wa uteuzi au uchaguzi kwa lengo la kumnadi na kumsaidia mgombea huyo katika kampeni za uchaguzi (Kifungu 7(3)).

Mgombea atakayekuwa na timu ya kampeni anapaswa kuwasilisha majina ya watu wanaounda timu yake ya kampeni siku mbili kabla ya kuanza kwa mchakato wa uteuzi au siku saba baada ya uteuzi, kama ifuatavyo:

1.Mgombea Urais anapaswa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi hamsini (50). (Kanuni 17(1)(a))

2.Mgombea ubunge katika eneo la Tanzania Bara anapaswa kuwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi ishirini (20). (Kanuni 17(1)(b));
Wamejibu wapi?
Lete barua....
 
Kwahiyo huwezi kutofautisha gari za serikali ( waziri) na gari za chama cha siasa (CCM).?
Kwahiyo unaweza kutuwekea ushahidi hapa wa kwamba waziri mkuu anatumia hari za selikali na si za ccm?
 
Jibu unalotafuta hapo ni lile la wanafunzi wa darasa la pili. Aliyeko la saba anaelewa sana, ukimuuliza baba yako ni nani, akisema huyu ni mume wa mama inatosha. Yaonekana Lissu hakujua hilo na hakuitumia nafasi hiyo kwa uzembe. Sijui kwa nini hakujiuliza 2015 waliomsindikiza Lowasa walikuwa wanatafuta nini!
2015 waziri gani alizunguka na Lowassa kwenye kampeni??
 
NEC: TIMU ZA KAMPENI

Timu ya kampeni ni kundi la watu lililoundwa na mgombea wakati wa mchakato wa uteuzi au uchaguzi kwa lengo la kumnadi na kumsaidia mgombea huyo katika kampeni za uchaguzi (Kifungu 7(3)).

Mgombea atakayekuwa na timu ya kampeni anapaswa kuwasilisha majina ya watu wanaounda timu yake ya kampeni siku mbili kabla ya kuanza kwa mchakato wa uteuzi au siku saba baada ya uteuzi, kama ifuatavyo:

1.Mgombea Urais anapaswa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi hamsini (50). (Kanuni 17(1)(a))

2.Mgombea ubunge katika eneo la Tanzania Bara anapaswa kuwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi ishirini (20). (Kanuni 17(1)(b));
Halafu eti Msaliti Lissu mnasema ni gwiji la sheria nchini kama ameshindwa hata kutafasiri vifungu hivyo!! Na chadema walikuwa wanashangilia kama ameongea kitu cha maana sana eti Waziri Mkuu Majaliwa na piga kampeni kama nani?
 
Back
Top Bottom