Uchaguzi 2020 NEC yafafanua Timu za Kampeni baada ya Tundu Lissu kuhoji ushiriki wa Kassim Majaliwa katika kuzunguka nchi nzima

Uchaguzi 2020 NEC yafafanua Timu za Kampeni baada ya Tundu Lissu kuhoji ushiriki wa Kassim Majaliwa katika kuzunguka nchi nzima

Pia hiki nikipindi Cha kuomba kura Kuna vitu ukivifanya kwa kulazimisha Kuna makundi yatakunyima Kura kwa kuona unatumia madaraka yako kujinufaisha kwa mfano watu wa Dini wanahuburi haki sasa kama hutendi haki kwa vitendo tayari unapoteza kura kwenye makundi yanayotetea haki.
 
NEC: TIMU ZA KAMPENI

Timu ya kampeni ni kundi la watu lililoundwa na mgombea wakati wa mchakato wa uteuzi au uchaguzi kwa lengo la kumnadi na kumsaidia mgombea huyo katika kampeni za uchaguzi (Kifungu 7(3).

Mgombea atakayekuwa na timu ya kampeni anapaswa kuwasilisha majina ya watu wanaounda timu yake ya kampeni siku mbili kabla ya kuanza kwa mchakato wa uteuzi au siku saba baada ya uteuzi, kama ifuatavyo:

1. Mgombea Urais anapaswa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi hamsini (50). (Kanuni 17(1)(a)

2. Mgombea ubunge katika eneo la Tanzania Bara anapaswa kuwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi ishirini (20). (Kanuni 17(1) (b);
Huu ndio "ufafanuzi"? Mbona hawasemi vifungu allivyotaja TL kama havihusiki katika haja yake ya kupinga ushiriki wa PM Majaliwa ktk kampeni za JPM?
 
NEC: TIMU ZA KAMPENI

Timu ya kampeni ni kundi la watu lililoundwa na mgombea wakati wa mchakato wa uteuzi au uchaguzi kwa lengo la kumnadi na kumsaidia mgombea huyo katika kampeni za uchaguzi (Kifungu 7(3).

Mgombea atakayekuwa na timu ya kampeni anapaswa kuwasilisha majina ya watu wanaounda timu yake ya kampeni siku mbili kabla ya kuanza kwa mchakato wa uteuzi au siku saba baada ya uteuzi, kama ifuatavyo:

1. Mgombea Urais anapaswa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi hamsini (50). (Kanuni 17(1)(a)

2. Mgombea ubunge katika eneo la Tanzania Bara anapaswa kuwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi ishirini (20). (Kanuni 17(1) (b);

Kama hivi ndivyo kwanini basi kutunga kanuni 2 zinazokinzana??? moja inaeleza majina 50 ya timu za kampeni lakini haikufafanua kama mawaziri wanaweza kuingia kwenye timu za kampeni lakini kanuni nyengine INAKATAZA mgombea kwenda kupiga kampeni nje ya eneo lake isipokuwa mgombea urais peke yake.

Nadhan hili bado halijakuwa jibu rasmi na Tundu Lissu akija kujibu kihoja hichi kwanza ataanza kusema ni majibu ya kijinga ambayo yametolewa.
 
Wajua ma ccm ushabiki unawapa upofu kweli. Waziri mkuu anakampeni kama mgombea mwenza, mbona anatuma cheo cha waziri mkuu kufanya ziara za kampeni? Yeye no mgombea wa jimbo.
Ndo maana tunasema ccm ni chama cah matepeli kwelikweli. NEC haina kauli wala jibu, mkurugenzi wa NEC anakigugumizi kwa hili. Hii tume ipo kwaajiri ya ccm tuu. Ila mudawao umewadia kupigwa chini.

SASA HAPO TUME WAMEJIBU NINI MLETA MADA???
 
Japo mengi mnakosa kuelewa hadi hapo unashindwa kuelewa? Je majaliwa ni mgombea ubunge nani amemruhusu azunguke majimbo ya wenzake ?
Nimeshaelewa kwa nini waalimu wa primary school wanalazimika kutumia fimbo.
 
Waziri mkuu anafuata ratiba gani? Je kwenye timu moja wanaweza kuwa na ratiba tofauti..

Waache upuuzi..
NEC: TIMU ZA KAMPENI

Timu ya kampeni ni kundi la watu lililoundwa na mgombea wakati wa mchakato wa uteuzi au uchaguzi kwa lengo la kumnadi na kumsaidia mgombea huyo katika kampeni za uchaguzi (Kifungu 7(3).

Mgombea atakayekuwa na timu ya kampeni anapaswa kuwasilisha majina ya watu wanaounda timu yake ya kampeni siku mbili kabla ya kuanza kwa mchakato wa uteuzi au siku saba baada ya uteuzi, kama ifuatavyo:

1. Mgombea Urais anapaswa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi hamsini (50). (Kanuni 17(1)(a)

2. Mgombea ubunge katika eneo la Tanzania Bara anapaswa kuwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi ishirini (20). (Kanuni 17(1) (b);
 
Kwa hiyo wenye shida na rais nao wasemeje?

Waziri mkuu alikuja huku Rombo majuzi tu hapa na msafara wake ulikua unatumia magari ya serikali na ving'ora juu huku yeye akikazana kumkampenia huyo dikteta wenu uchwara alafu unasemaje hapa!? Kama waziri mkuu yupo kwenye kamati kuu basi ilitakiwa awe kwenye msafara wa rais inayotumia magari ya chama na si vinginevyo umesikia wa CCM?.
 
Je, Mgombea anaweza kuwa kwenye timu ya kampeni ya mgombea mwingine?
Lakini pia sheria yasemaje kuhusu utendaji kazi wa hiyo timu ya watu 50, wataruhusiwa kutembea na mgombea wakimnadi au kila mtu anaweza pita apitako anakotaka kufanya kampeni? Kama ni ndio, kuna haja gani ya Tume kuwa na ratiba ya mgombea tu, kwann isiwepo hadharani ya ratiba ya timu yake?

Lakini pia sheria yasemaje kuhusu ushiriki wa mawaziri kwenye kampeni?
 
Weka hapa hiyo sheria,
Kama ni hivyo basi hata wagombea ubunge ambao ni mawaziri wasifanye kampeni
Majaliwa anapaswa kuwa sehemu alipo Makamu wa Rais MAMA SAMIA au alipo MAGUFULI.

Sio azunguke mwenyewe kama anagombea urais yeye.

Na hakuna ratiba ya Majaliwa kuzunguka peke yake nchi nzima.
 
Ina maana bingwa wa sheria hakuzisoma kanuni hizo. Uzuri amejaliwa kukosa aibu.
Yaani we umeona tume hapo imejibu sawia kabisa? Kweli bure kabisa😂
Je mgombea wa nafasi yeyote anaweza kuwa katika campaign team ya mgombea mwingine? (Hili ndilo lilipaswa kutolewa maelezo na si kwa mgombea kuwakilisha majina ya team yake campaign)
 
Dah! Boss! Amini una kichwa kigumu! Hilo la waziri tena limetoka wapi? Au lisu kaleta swali la nyongeza?
Majaliwa afanye kampeni jukwaa moja na Mama Samia au Magufuli hapo atakuwa sawa kisheria.

Sio Pombe yuko Iringa yeye Majaliwa yuko Tanga... anagombea nini huko Tanga?

Anatumia magari ya serikali kupiga kampeni halafu NEC wanakenua meno hapa
 
Hahahhaha.. Washabiki wa Lisu ni wajinga sana aisee!

Sheria zipo na Lisu anaejifanya kujua sheria hatukutegemea kuhoji swali la kipopoma kama hilo

Ratiba ya Majaliwa ipo huko NEC au kwa msajili?
Je, unaweza kuiweka hapa tuione??
 
Jibu unalotafuta hapo ni lile la wanafunzi wa darasa la pili. Aliyeko la saba anaelewa sana, ukimuuliza baba yako ni nani, akisema huyu ni mume wa mama inatosha. Yaonekana Lissu hakujua hilo na hakuitumia nafasi hiyo kwa uzembe. Sijui kwa nini hakujiuliza 2015 waliomsindikiza Lowasa walikuwa wanatafuta nini!
Kwani miongozi mwa waliomsindikiza Lowassa 2015 alikuwa waziri?.Hivi unafikiri hoja za Lissu zinajibika kirahisi rasihi hivyo?.
 
Lakini pia sheria yasemaje kuhusu utendaji kazi wa hiyo timu ya watu 50, wataruhusiwa kutembea na mgombea wakimnadi au kila mtu anaweza pita apitako anakotaka kufanya kampeni? Kama ni ndio, kuna haja gani ya Tume kuwa na ratiba ya mgombea tu, kwann isiwepo hadharani ya ratiba ya timu yake?

Lakini pia sheria yasemaje kuhusu ushiriki wa mawaziri kwenye kampeni?
Mkuu sio kama ni hivyo, kiufupi hakuna hiko kitu cha wengine kupita huku na huko wakimnadi mgombea urais vinginevyo NEC ingetoa ratiba zao. Team inapaswa iambatane na mgombea full stop, CCM wakifanya ni sawa na mataga hayo wanayafukia. Upumbavu mkubwa huu
 
Kanuni 17(1)(a) - Mgombea Urais anapaswa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi hamsini (50). Kati hao hamsini anaweza kuwamo na aliye kuwa waziri mkuu.
Kumbe sio waziri kwa sasa ...
 
Back
Top Bottom