Nehemia Mchechu na Lawrence Mafuru warejea ulingoni, January Makamba awateua Wajumbe wa Bodi ya TANESCO

Nehemia Mchechu na Lawrence Mafuru warejea ulingoni, January Makamba awateua Wajumbe wa Bodi ya TANESCO

Naona makamba amewakumbuka vijana wenzie.Hao Mafuru na Mchechu ni CEOs waliong'ara sana na kuleta mapinduzi kwenye taasisi walizo wahi kuendesha. Sema siasa pia iliwaingilia mno kiasi wakashindwa kuhimili,na kuathiriwa na uadirifu
Dah... Waliong'ara ? ....Dah 😂😂😂🤭
 
Hapo kuna kama majina manne makubwa yananitia mashaka sana na uadilifu wao kuanzia Mchechu,Mafuru,Maajar na Mzee Gachuma naona kama ni watu wa fursa zaidi,najua huyo mtoto wa Bakhressa hana njaa na hao wengine siwajui sana.
Gachuma ni tajiri mkubwa ana njaa gani?,maajar ni wakili mkubwa sana na mwenye kipato kikubwa ana njaa gani?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Enzi za msoga dynasty Hadi mtu Kama mwakyembe alishaanza kutengeneza kampuni yake ya mfuko ya kufua umeme wa nguvu za upepo sijui aliishia wapi nayo[emoji1][emoji1787]
Hahahahahah jamaa aligunduliwa ni mkolomije ila Tapeli tu 😅
 
Mama alipohamua kumteua January kuongoza wizara nyeti na ya kimkakati kama ya NISHATI ametoa boko kubwa mno!![emoji34][emoji34][emoji34][emoji22][emoji22][emoji22].

Mama tuonee huruma watanganyika ingawa wewe huna cha kupoteza huku bara.

Katiba mpya muhimu sasa kuliko wakati mwingine wowote .
#FreeMbowe japo anaitaka katiba mpya kwa maslahi yake binafsi.

Uchaguzi wa 2025 CCM lazima tuiondoe mama wa kizenji arudi nchini kwao kula mafao ya kustaafu.

Akina mama wa kitanganyika chagueni kutetea jinsia huku mkiwaachia nchi ya taabu na dhiki kuu watoto waliotoka matumboni mwenu au chagueni raisi bila kujali jinsia. Yaani raisi atakaye waandalia watoto wenu maisha bora yasiyo na mateso.
Mkuuu tatzo wizi nao kwenye sanduku la kura ?
 
Acha kujiaibisha na chuki zako kwa kikwete! Na Ndo mana mnazidi kuonekana washamba! Kazi kudharau tu wanawake! Mnamdharau Samia kana kwamba yeye hana akili au hawezi kuongoza wajinga nyie.

Samia anachagua timu yake yeye anayoona inafaa kwa utashi wake na ushauri anaopewa na vyombo!

Huyo Magufuli unayemsifu hapa ndo ameiua National Housing. Tangu aingie miradi yote ya kawe, Morroco na kugamboni ilisimama na kufa kisa chuki zake na kijana mchechu!

Yeye alipenda kujenga na kupeleka miradi chato tena bila bajeti! Hela alikuwa anataka kuchukua kwenye mashirika na Ndo mana hakuendana na watu wenye misimamo na akili Kama Prof Assad, Nehemia Mchechu na Mafuru!
Rudi shule bata mzinga ww cyo kugomboni ni KIGAMBONI
OVA
 
Kwamba Tanzania haina watu wengine zaidi ya hao. Wameshatolewa kwa ubadhirifu wanarudi tena. Nchi hii mbovu sana na inakera sana. Rais ajue anatengeneza hasira sana kwenye mioyo ya watu hajui tu.
Wametolewa kwa ubadhirifu gani? Weka ushahidi hapa wa Mahakama iliyowahukumu kwa huo ubadhirifu.

Acheni chuki wana chato!
 
Hahahahahaha yani safu ya wapiga dili imerudi mchezoni kwa aina yake 😅 hapo Makamba anaenda kupiga hela ndefu sana ndani ya muda mchache mno!

Hawa watu huwa wana circulate tu kama vile hakuna watu wengine wenye akili zaidi yao nchini! Leo NHC mara katumbuliwa kesho yupo NSSF mara kachomolewa keshokutwa yuko TPA mara kang’olewa anakuja kuibukia TANESCO! Je, hawa watu ni miungu ama? Don’t we have any new heads za management humu nchini ni lazma wawe hao hao akina Dau, Mchechu?
Dili gani walipiga? Mbona hamkuwapeleka Mahakamani Kama mlikuwa na ushahidi?

Acheni chuki zenu
 
Acha upumbavu wewe, ina maana hao jamaa pekee ndio wanaojua management sana kuliko wengine? Mbona kuna watu wako exposed na wana ma elimu makubwa tu ni Diaspora kwanini wasitafutwe hao kama hatuviamini vichwa vyetu vya UDSM?

Kiufupi hapo kitakachofata ni upigaji tu sawa na mbwa kumteua fisi na simba kukabidhiwa ulinzi wa bucha! Subirieni mgao na bei ya luku kupanda kwa sababu za ajabu ajabu. Sahizi wameanza na kisingizio cha kuweka nguzo za zege najua tutafikia ambako umeme unakatwa tu kwa kisingizio mabwawa yamekauka hayana maji y kutosha wakati mvua zilikuwa nyingi tu ili watu wauze majenereta na kukaribisha kampuni za mfukoni za kufua umeme.
Wataje hao watu wenye exposure na elimu kubwa ili wazingatiwe. Kama unaishia kubwabwaja na wewe ni wale wale tu!
 
Hii reshuffle na sura zinazoingia dhamiri yangu inaniambia kitu kingine kabisa.

After six months kuna kampuni mpya inayojihusisha na Nishati huenda ikasajiliwa au itapata tender TANESCO.
Shamba la Bibi.. Most likely hiyo kampuni itakuwa ya SSB... Kuishi kwingi ni kuona mengi.. Kazi iendelee
 
Hahahahah jiandaeni na powercuts kwa kununua majenereta kabla nchi haijaanza kukaukiwa na mabwawa ya Mtera na Kidatu kama ilivyokuwa 2009-2011 😅
Naona unapiga ramli sio! Hakuna cha Mtao wa umeme wala nini! Nyie mlipoanza kukata umeme hovyo ili kumfanya Mama aoneoane hafai ilikuwa nini ile? Mmegunduliwa na kutolewa Nishati na Tanesco ndo mnaanza maneno! Hamna akili nyie mmejaa ushamba na chuki tu
 
Back
Top Bottom