Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Hotuba yenye hekima kubwa.
Ukweli ni kwamba tawala za kidikteta za mashariki ya kati zinachukiwa sana na wananchi wake, bali wananchi hawana la kufanya kutokana na ushetani mkubwa wanaofanyiwa na watawala wao, yakiwemo mauaji ya yeyote anayeinuka na kutaka mabadiliko. Tawala hizo hazina tofauti na utawala wa CCM nchini mwetu ambao unateka na kuua kila anayehoji na kutaka mabadiliko kwenye mifumo ya utawala.
Iran kabla ya utawala wa kidikteta, ilikuwa inaonekana kuwa ni Ulaya ndani ya mashariki ya kati, kutokana na kiwango cha maendeleo iliyokuwa imeyafikia. Leo imekuwa ni miongoni mwa mataifa machache ya mashariki ya kati ambayo wananchi wake wanaishi kwa mateso ya umaskini wa kupimdukia. Pamoja na utajiri wote wa mafuta, 31% ya wairan wote wanaishi chini ya mstari wa umaskini (acute/abject poverty), sawa na wale maskini wa kupindukia, kusini mwa jangwa la Sahara..