Usiku utumie masaa 11? Mchana utatumia mangapi sasa?
Mbona sioni utofauti wowote?
Endesha kwa tahadhari mkuu, usiku advantage yake ni tochi hakuna hivyo unaweza piga 80-150km/hr bila taabu.
Lakini matuta yako palepale, na kwenda spidi zaidi ni hatari kubwa sana kwako.
Moja ni malori yaendayo polepole na hayana taa nyuma, na mbili gari zilizo haribika pembeni.
Hizi ajali mbaya hutokea hasa kama kuna gari mbele, na limekupiga full light.
Majuzi karibu nipate mzinga mzito saa saba usiku pale Mikumi.
Kulikuwa na mbogo kama sita barabarani, rangi yao sawa tu na rangi ya lami usiku.
Sikuwa spidi kali lakini kusimama ilibidi kuchuna breki.
Mmoja karibu anigeukie lakini mchuno wa breki, taa na kusimama karibia mita 15 ilisaidia na wakakimbia.
Usiku spidi zako tu lakini chukua tahadhari.
Miaka ile, hakuna tochi , malori wala matuta, stretch hiyo ilikuwa 8-9 hrs, tena kwa pick up.