Ngiri (Warthog ): Naomba wataalamu watueleze Kwa kina kuhusu huyu Mnyama

Ngiri (Warthog ): Naomba wataalamu watueleze Kwa kina kuhusu huyu Mnyama

Ukisikia boda anakwambia, hapa ni mwendo wa ngirii, mkia juu achana naye. Huyo jamaa anapita katikati ya kundi la simba hadi simba wanatawanyika wanabaki wanashangaa nini kimepita hapa.
Sema akishikwa anapiga kelele unaweza muonea huruma
Jamaa ana confidence sana haogopi kitu
 
Kwa siku za Hivi karibuni ukipita kwenye mitandao ya kijamii utakuta huyu Mnyama anasema Kwa utani hasa speed yake.

Sasa Kuna wimbo wake sijui ni kabila Gani na una maana gani Kwa anayejua anaweza kutuambia maana ya =>Kasongo yeyeeeee mombali nangai, kasongoooo mbona weooo songa limala
oooohhh yeyeyeee. Kasongo mbona weooo, mbona weeeeooooooo.😀😀.

Pia Kuna baadhi ya page wanasema Hivi👇👇😹😹😹

When scientists were ranking animals, the warthog was in his holes so they ended up crowning the wrong guys. King of the jungle title went to the lion and fastest went to the cheetah but both titles belong to the hog.

Third title for the warthog is for reverse parking. Dude can reverse into a hole in the middle of a high speed chase 😂🤣 acceleration from zero is like a race car and brakes are instant.. i think its time we crown the right champions with all fairness.. if a cheetah can chase a hog and fail to catch it then we have a new champion, the V16 bi-turbo 6.5L AMG engine 🤣

Sasa ukweli ni upi? Nahitaji kujua zaidi kuhusu huyu Mnyama.

Nimewaona sana Kisarawe Pwani

View attachment 3124447wanasema Kwa Sasa ndoThe king of the jungle 😂😂View attachment 3124449Binafisi nafurahi sana pindi niliona clip zake jinsi anavyokimbia!!

Nimewawekea na clips
Ngiri ndiye mwanzilishi wa klabu za joging'i Tanzania wakati huo akiishi Gongolamboto, Pugu na Kisarawe alkokua analima mihogo. Wale wanachama wa Mzimuni Joging'i Klabu mnatakiwa mumpe heshima zake.
 
Wanyam wawili ninaopenda kuangalia clips zao ni huyo worthog na Honey burger a.k.a Mr die harder...
Screenshot_20241014_094815_Google.jpg

Huyu naye shoo yake sio ya kitoto..
Sio tuu hafi kinyonge, huko kumuwinda tuu ujipange, asilimia kubwa atakuacha na ngeu, yeye akitokomea kusikojulikana..
Wewe kiumbe ambaye chakula chake kikubwa ni Nyoka hasa Black mamba na Cobra unamchukuliaje..
Screenshot_20241014_095007_Google.jpg
 
Wanyam wawili ninaopenda kuangalia clips zao ni huyo worthog na Honey burger a.k.a Mr die harder...View attachment 3124487
Huyu naye shoo yake sio ya kitoto..
Sio tuu hafi kinyonge, huko kumuwinda tuu ujipange, asilimia kubwa atakuacha na ngeu, yeye akitokomea kusikojulikana..
Wewe kiumbe ambaye chakula chake kikubwa ni Nyoka hasa Black mamba na Cobra unamchukuliaje.. View attachment 3124491
Kweli kabisa huyu nae mtiti wake sio wa kitoto. Wanasema hata panga ukimkata haiingii. Pia nasikia akifika kwenye mzinga akiachia ushuzi tu nyuki wote wanalewa anajilia asali atakavyo. Anaitwa nyegere kiswahili kama sijakosea
 
Ngiri ndiye mwanzilishi wa klabu za joging'i Tanzania wakati huo akiishi Gongolamboto, Pugu na Kisarawe alkokua analima mihogo. Wale wanachama wa Mzimuni Joging'i Klabu mnatakiwa mumpe heshima zake.
Kisarawe walikuwepo wengi sana sijui Kwa sasa. Siku ya kwanza nilikuta meno yake na baadhi ya mabaki ya mifupa nikayachukua nikauliza wenzangu wakasema huyo ngiri kafa miaka mingi sana. Wakasema huko kwetu bara ni diri ila huwezi peleka ukikamatwa maisha!!
 
Hii ni misconception iliyotokana na kujua ķuwepo kwa nguruwe pori. Watu wanafikiri nguruwe pori ndiyo ngiri.

Ukweli ni kuwa ngiri (Warthog) sio nguruwe pori. Na Boar (nguruwe pori) sio ngiri. Boar ukigoogle picha zake, utaona ni nguruwe kabisa.
Acha ubishi huyo ni nguruwe pori tuliomla tunajua ngozi sio pana sana ,nyama mpk harufu ya nguruwe na mafuta anayo
 
Kisarawe walikuwepo wengi sana sijui Kwa sasa. Siku ya kwanza nilikuta meno yake na baadhi ya mabaki ya mifupa nikayachukua nikauliza wenzangu wakasema huyo ngiri kafa miaka mingi sana. Wakasema huko kwetu bara ni diri ila huwezi peleka ukikamatwa maisha!!
Mpaka miaka ya 80 walikuwa wanaonekana Gongolamboto maeneo ya kiwanda cha KILITEX na kule kwenye machimbo ya Pugu, sasa hivi wapo Saadani Bagamoyo mitaani, usiwaogope ukipishana nao wao wako bize wanajogi.
 
Acha ubishi huyo ni nguruwe pori tuliomla tunajua ngozi sio pana sana ,nyama mpk harufu ya nguruwe na mafuta anayo
Sawa jomba. Nimeacha ubishi.
Nyama ya khanga na ya kuku zinafanana, kwa hiyo khanga ni kuku pori.
Chimpanzee anafanana na binadamu, kwa hiyo chimpanzee ni binadamu pori.
Mende akichomwa moto hutoa harufu kama ya kumbikumbi, basi kumbikumbi ni mende wa kwenye kichuguu
 
Kweli kabisa huyu nae mtiti wake sio wa kitoto. Wanasema hata panga ukimkata haiingii. Pia nasikia akifika kwenye mzinga akiachia ushuzi tu nyuki wote wanalewa anajilia asali atakavyo. Anaitwa nyegere kiswahili kama sijakosea
Honey badger nasikia hata haja kubwa huwa hajisaidii hovyo,kama ni Temeke ni huko huko,hata akibanwa akiwa Kimara anaweka furushi la majani kuziba isitoke anarudi Temeke kujisaidia,ukitaka kuprove hili nenda sehemu anapojisaidia lazima ukutane na mafurushi ya majani yaliosokotwa...
 
Kuhusu Hilo sijui ila najua anaye fanya hivo Mnyama fln anaitwa fungo.
 
Mang'ati na wasukuma kule pwani walikuwa Wana waua Kwa mbwa lakini walikuwa wanatumia hasa mikuki mara kadhaa nimewasadia kumbeba Hadi kambini wateja wanakuja kuchukulia pale.
Ili mbwa aweze kum'mudu huyo Mwamba ni lazima mbwa wawe wengi halafu na huyo mwamba awe ameshachoka sana. Vinginevyo hilo timbwili ni la kiwango cha lami.
 
Ili mbwa aweze kum'mudu huyo Mwamba ni lazima mbwa wawe wengi halafu na huyo mwamba awe ameshachoka sana. Vinginevyo hilo timbwili ni la kiwango cha lami.
Nahisi hivyo mara zote walikuwa na kundi la mbwa na mikuki.

Niliona nyani kamwaga utumbo wa mbwa kama utani asee zile kucha na meno ni hatari sana akiwa anatetea uhai wake.
 
Back
Top Bottom